Morogoro: Watu 11 wafariki kutokana mvua

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
WATU 11, saba wakiwa watoto, wamekufa kwa kusombwa na maji na wengine kuangukiwa na kuta za nyumba baada ya mvua kubwa kunyesha katika vijiji vya Pande na Konde vilivyopo mkoani Morogoro.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa , amesema majira ya saa saba usiku katika kijiji cha Konde , Kata ya Konde ,Tarafa ya Matombo wilaya ya Morogoro watu wanne wa familia moja walikufa kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao wakati mvua ikiendelea kunyesha.

Mutafungwa , aliwataja watu hao wanne wa familia moja waliokufa kuwa ni Godfrey Augustin (35) , Joyce Claud (38) Mariana Godfrey (10) mwanafunzi wa shule ya msingi Konde na Senorino Godgrey ambaye ni mtoto miaka mitano.

Kamanda Mutafungwa ,alisema miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya taratibu za maziko. Mbali na hao pia, alisema watu saba wengine wamekufa kutokana na kusombwa na maji katika kijiji na kata ya Pemba , tarafa ya Mvomero , wilaya ya Mvomero .

Mutafungwa aliwataja waliokufa katika tukio hilo kuwa ni Peter Ferdnand (66) ,Tumbo John (37), Kauva Peter (35), Jack Tumbo (6), Kadudu Fikiri (9), Madi Fikiri (14) , Mtupe John (8) .

Alisema, kati ya watu saba waliokufa , watano ni watoto wenye umri tofauti akiwemo mtoto mchanga wa kiume wa marehemu Kauva Peter ambaye alikuwa bado hajapewa jina.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa kuwa , mwili wa mtoto huyo mchanga haujapatikana. Mutafungwa , alisema miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

HabariLeo
 
R.i.p wale wote mliotutangulia na poleni sana wafiwa na majeruhi wote
 
Back
Top Bottom