MOROGORO: Rais Magufuli akabidhi kitita cha TZS Milioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule ya sekondari Mang'ula

Sasa ametoa milioni tatu sec hiyo alipo pita je sec iliyoko Namtumbo huko Ruvuma haina choo atatoa wap hiyo hela?nadhani rais aache kufanya maigizo kwa kutaka sifa zisizo za msingi.Tunachokitaka ni mpango mkakati na kutoa pesa kujenga vyoo nchi nzimz penye shda kama hiyo sio kutuletea maigizo.
Kwani Namtumbo haina watu waliotapakaa Tanzania nzima wenye kuweza kujenga vyoo vya shule zao?.

Kwa rais kusaidia ujenzi wa Choo ni alama ya utu na ukaribu kwa watu wake. Siku ya uchaguzi familia nzima ya huyo mtoto itapigia kura CCM, ni ubinadamu kwanza.

Punguza roho ya kwanini, itaendelea kukuweka kwenye umasikini mpaka siku yako ya kuondoka duniani.
 
Mheshimiwa Rais sipendi kukubeza na kitendo chako cha kumpa mwanafunzi wa kidato cha kwanza milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule. Kitendo ulichofanya ni kwanza hatari kwa yule mwanafunzi, mbili umemfanya yule mwanafunzi kuwa katika situation ambayo anaweza kuweweseka kwa kupata hela nyingi kiasi hicho mkononi katika maisha yake. Hatuwezi jua nini ni matokeo yake mwishowe yanaweza yakuwa mazuri au mabaya.

Lengo langu hapa ni kuangalia kwa nini shule nyingi Tanzania zina hali kama hiyo? Naomba tujaribu kujitathmini sisi wenyewe nini ni mafanikio ya elimu yetu mpaka hapa tulipo?

Tatizo ninalo liona hapa ni kukosekana kwa maarifa na nguvu ya kuthubutu vitu.

Watanzania hatuna ile spirit ya kujituma wenyewe kufanya vitu kwa mikono yetu na maarifa kwa manufaa yetu. Tunapenda sana kutoa lawama na kutaka serikali ifanye kila kitu. Nasikitika kusema haya, hata kama ina uma, haya ni matokeo ya sera ya mfumo wetu wa ujamaa.

Nchi yetu haina ile spirit ya utengenezaji wa vitu kwa maarifa. Watanzania wengi hatuna uwezo wa practical things. Tumekuwa wachuuzi zaidi kuliko utengenezaji.
Na hii yote ni kwa sababu ya mfumo mbaya wa elimu yetu. Elimu yetu ni ya kujua kusoma na kuandika vilivyo kwenye vitabu tu na sio elimu ya kuwafanya wanafunzi pindi wanapo maliza elimu yao kuweza kutafakari kutafuta jia za kutatua matatizo yao ya kijamii practically and technically. We are more consumers rather than manufacturers. Ndiyo msingi wa elimu yetu. Elimu yetu inahitaji mabadiliko. Tuna hitaji wataalam wa sayansi ya vitendo na sio ya vitabu. (Applied Sciences).

Kwa hali hiyo ningekuomba Rais mwenye PHD ya Chemistry jaribu kuangalia kwa kina hali ya elimu yetu ilivyo na tujaribu kuirekebisha kulingana na hali halisi ya maisha yalivyo kwa manufaa ya wananchi wote hata vijijini.
Ni jambo la kusikitisha sana kusikia shule ya sekondari haina vyoo na ni haibu kubwa sana kwa jamii na taifa letu kwa ujumla.

Rais Magufuli naomba nikuulize swali? Una uhakika kweli Tanzania itakuwa nchi ya viwanda wakati wanafunzi wanashindwa kuwa na hata vyoo?

Ujerumani inatawaliwa na Chancelor Merkel ni mwanamke na ana PHD ya Physics. Nchi yake ni kweli nchi ya viwanda. Na wengi wao ni wachapa kazi haswa. Na wana utundu wa kutatua matatizo yao ki-technic. Watoto wadogo wanajua toka majumbani kwao nini cha kufanya kukabiliana na matatizo ya maisha na hawana dhahabu wala madini mengine kama sisi. Ujerumani ilijaliwa kuwa na makaa ya mawe tu. Ajabu ni kwamba waliyatumia hayo makaa ya mawe kutengeneza chuma. Na wakati mimi nasoma sekondari nilipata kusikia katika somo la geography kuwa ujerumani ni watengenezaji wa wa chuma maarufu ulimwenguni japo kuwa madini ya chuma hawana.

Sisi tuna kila kitu lakini hatujui jinsi ya kutumia rasilimali zetu zikatuinua kimaisha na kuleta maendeleo ya wananchi wetu.

Rais Magufuli nina uhakika wewe binafsi una maarifa mengi na dhamira kubwa ya kutaka kuleta maendeleo kwa watu wako unao watawala, lakini kosa unalo lifanya uko selective mno. Katika uchaguzi wa watendaji kazi wako una Base sana na watanzania peke yao. Mtanzania aliyeishi Tanzania na kusoma humo na hata kwenda nje kwa ajili ya masomo tu na kurudi ni wachache wanamwamko wa kutumia utaalam walio ipata kiuadilifu. Kwa mara nyingine nakuomba tena kuangalia vizuri elimu yetu hasa ya shule ya msingi na sekondari.

Kitu ambacho hujajifunza utotoni huwezi hata ukiwa ukubwani ukakiweza. Ndiyo maana tuna ma-civil engineers kibao ambao hawajui hata kujenga madaraja na barabara. Watu wa nje ndiyo kutusaidia.

Nakubaliana na swali lako la daima; "Watanazinia tumelogwa na nani?"
Jibu lake ni watanzania tumelogwa na elimu yetu ya mfumo wa kijamaa! That is the biggest killer of our skill!

Mheshimiwa Rais hiyo spirit yako ya kufufua shirika letu la ndege na miradi mingine mikubwa ya standard gauge na umeme wa Stieglers gorge naomba fanya hivyo hivyo kwa miradi ya kuzalisha chuma na usafishaji wa dhahabu. Hata kama tutapata hasara, lakini tuna sehemu ya kuanzia.

Weite watanzania kutoka nje na uwasikilize. Kuna baadhi wana vichwa vya maarifa ya kuindeleza nchi yetu. Wawezeshe hao watatusidia sana. Watanzania peke yao hawata weza. Si unaona mwenyewe hata vyoo wanashindwa kutengeneza?

Hapo hapo ungemtimua huyo headmaster na msaidizi wake wa hiyo shule kama ni ya serikali.
Ni Headmaster asiye kuwa na mfano bora kwa jamii yetu. Mtu kama huyo anapewa jukumu la kusimamia elimu kwa watoto wetu? Haitaenda.
 
Hivi hizi shule zimekosa choo kipindi cha utawala wa tano. Ina maana rais kafanya kosa kutoa milioni tatu. Hapo kulikuwa na madiwani na viongozi wengi wa serikali. Huyo mtoto kazipokea hizo hela kuwakilisha shule yake ila zitachukuliwa na viongozi husika kwa ajili ya kujengea choo
 
Kuna watu wajinga by nature, hivi hizi shule zimekosa choo kipindi cha utawala wa tano. Mbona watu wapumbavu hivi. Inamaana rais kafanya kosa kutoa milioni tatu. Hapo kulikuwa na madiwani na viongozi wengi wa serikali. Huyo mtoto kazipokea hizo hela kuwakilisha shule yake ila zitachukuliwa na viongozi husika kwa ajili ya kujengea choo
Una uhakika gani kama choo kitajengwa?
 
Ulaya kuna wazungu ambao hawagawi hela ovyo majukwaani bali kila senti inayo tumika ni kwa mipango inayoeleweka.
 
Tumechoshwa na filamu zenu, jiwe akiskia kwenda ulaya tu kuonana na wawelezaji naskia anapata tumbo la kuharisha
Wawekezaji wa kujenga vyoo? Kwanza hao wazazi na waalim wa hiyo shule ni bure kabisa. Mambo ya harusi na sherehe wanapata fedha za kuchanga lakini inapokuja jambo muhumu kama hilo wanakimbia. Na mashabiki wao kama wewe unataka rais aende Ulaya kutafuta wafadhili.
 
Kwa ubahiri Wa chadema sidhani naona roho zitawauma wiki
Upo kwenye mgao wa buku7.
Hata hushangai mwanafunzi kupewa fedha za ujenzi vyoo. Hakuna DED, DC, WEO, VEO wote hao hawakuwa katika mkutano.
Zikipotea atashtakuwa huyo mwanafunzi
 
Kuna maninja kufanya misheni imposibo kwao ni kitu cha fahari!.. Jiwe anavyoonyesha mpunga alionao kwenye ndinga ohoo!!..
 
Naamini huyo kijana hela hakukaa nayo zaidi ya dakika mbili,
wakubwa waliichukua,na kitajengwa choo cha laki tatu,
kisha pesa ndo itakuwa imeyeyuka
 
Naamini huyo kijana hela hakukaa nayo zaidi ya dakika mbili,
wakubwa waliichukua,na kitajengwa choo cha laki tatu,
kisha pesa ndo itakuwa imeyeyuka
Tutapenda baada ya mwezi mmoja hivi tupate picha ya hivyo vyoo vilivyo jengwa na hizo hela.

Inapendeza sana.
 
Mambo mengine ni aibu!!! Shule haina vyoo!
Kwenye mkutano wa Raisi hakuna mwalimu, hata Mkuu wa Shule.
Mambo mengine ni aibu; aibu hata kusema mbele ya watoto.
 
Back
Top Bottom