nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 810
- 2,851
Hii ni habari ya kusikitisha kwa Wakulima na hujuma kubwa toka kwa Mkuu wa Mkoa, mtu aliyetegemewa kuwasaidia wananchi sasa amekuwa mkandamizaji kwa wananchi.
Kwa takribani mwezi sasa kumekuwa na juhudi toka kwa wafanyabiashara wahindi na madalali wao wa kuzuia mfumo wa stakabadhi ghalani kutumika katika Mkoa wa Morogoro katika zao la Ufuta.
Bodi ya Maghala Tanzania ilishaandaa mfumo kwa ajili ya kuanza kufanya kazi katika msimu huu. Lakini leo mkuu wa mkoa kasitisha mfumo huo kutumika akisingizia kuwa eti Elimu kwa Mkulima haijamfikia hivyo mfumo uanze mwakani.
Mwaka jana alisitisha mfumo kuanza katika wilaya za mlimba na Malinyi. Lakini mfumo ulifanyika na kufanikiwa sana katika wilaya ya Ulanga.
Cha ajabu Mkuu wa Mkoa, Ndugu Martin Shigela kasitisha zoezi kwa sababu eti wakulima hawajapata taarifa na elimu ya kutosha. Sasa kama mwaka jana Ulanga walifanya? Na wakafanikiwa? Nao Elimu yao sio ya kutosha kweli?
Katika mnada uliofanyika mkoa wa Songwe 1st June, kilo moja iliuzwa kwa bei ya shilingi 2877.
Lakini madalali wa wahindi hununua ufuta kati ya shilingi 800 hadi 1600.
Mkuu wa Mkoa kusitisha zoezi hili kwa kisingizio Wakulima hawako tayari sio za kweli bali tuamini amefika bei kwa wahindi na kaamua kumuuza mkulima.
Mkuu huyo huyo wa Mkoa ndio alituma barua kwa wakuu wa Wilaya waandae mfumo ambako katima hizo wilaya tatu tayari Bodi ya Maghala ilishatafuta watunza maghala na kuyaandaa kwa muda mrefu ili kazi ianze.
Kweli hii awamu ya 6 ndio imeamua kurudisha nyuma juhudi zote za wakulima na kuruhusu wanyonyaji wachache waendelee kufaidika kupitia jasho la watanzania wanyonge?
Tunakuomba Rais Samia haya mambo uyaangalie. Itavunja moyo watu kulima. Bei za pembejeo ziko juu sana na bado wakuu wa mikoa wanatumika wakulima wasipate bei nzuri za mazao?
Ni lini huyo Mkuu wa Mkoa amekaa na Wakulima na akagundua hawana elimu ya kutosha? Inahitaji elimu gani kujua wauzie wapi?
Kama wamekuwa wanalima na kuja kuwauzia wahindi Dar, je watashindwa kupeleka mzigo kwenye ghala hapo hapo na uuzwe? Hizi ni hujuma za kipumbavu kabisa.
Huyu Mkuu wa Mkoa awajibishwe. Bodi ya Maghala imezunguka huko pamoja na TMX kutoa elimu kwa magari na gharama ya Serikali. Leo mtu mmoja sababu ya kupewa hongo anakuja kusitisha mfumo na wakati katika ghala la Ulanga, Mlimba na Malinyi tayari wameshaanza kukusanya Ufuta?
Mama Samia tunakuomba uwasaidie hawa Watanzania masikini wanaoonewa. Tutatoa namba kwa vyombo husika vya madalali wa wahindi ili kupitia TCRA mawasiliano yao yachunguzwe maana wao ndio wamekuwa wakimpigia simu ili aue huo mfumo. Aibu kubwa sana kwa Taifa letu.
Chini ni attachment ya tangazo lililotolewa na ofisi ya Mkurugenzi juzi. Ambalo leo Ndugu Shigella kasisitsha. Sasa serikali moja kila mtu anafanya yake. Wengine kwa maslahi ya wananchi. Wengine kwa maslahi ya wanyonyaji.
UPDATES:
MKUU WA MKOA WA MOROGORO KAFIKA LEO KATIKA GETI AMBALO MKUU WA WILAYA ALITOA MAAGIZO KUWA UFUTA USIOPITIA KATIKA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI USIVUKE KWA MUJIBU WA MAAGIZO YA SERIKALI.
LAKINI MKUU WA MKOA KAFIKA LEO NA KURUHUSU UENDELEE KUPITA HAPO. HIVYO KATENGUA MAAGIZO YA SERIKALI YALIYOTOLEWA KWA MAANDISHI KWA MDOMO WALA SIO OFFICIAL DOCUMENT TOKA OFISI YA MKUU WA MKOA.
SHIGELLA ACHUNGUZWE KATIKA HILI. KWANZA ALIKUWA NA DHARURA GANI HADI KUWAHI KUFANYA HAYO SIKU YA WEEKEND?