kwa mbaaaaali! naiona Tanganyika tuitakayo inakuja!
kweli risasi siyo dawa, na Watanzania hawaogopi risasi tena.
nilidhani baada ya polisi kuuwa mtu maandamano yaliyopita, leo watu wasingejitokeza.
Magamba sasa hawana ujanja, polisi wao wameua wee, wakawa wanasingizia kuwa mauaji hayo yanasababishwa na viongozi wa Chadema, lakini penye ukweli, uongo hujitenga, shughuli yoyote ya CDM, isiyoingiliwa na vyombo vya dola, kama vule, UWT na Polisi, shughuli huisha kwa amani kubwa, kama unavyoona hapo Moro, sasa ni dhahiri siku za magamba kuwa madarakani, zinaanza kuheshibika! ni kweli, tunapaswa kumshukuru Mungu, na kama inavyojieleza slogan ya CDM,wao wana vyombo vya dola, CDM tunaye Mungu wetu, anayetuongoza kwenye haya mapambano!dahaa kweli wakati ni hakimu mzuri sana, muda wa mabadiliko ukifika umefika tu.. hata uzuie vipi! ASANTE MUNGU.
Nani kakuambia? mabadiliko ni kama nature uwezi kuyazuia! CCM watake wasitake oneday lazima wang'oke madarakanikweli risasi siyo dawa, na Watanzania hawaogopi risasi tena.
nilidhani baada ya polisi kuuwa mtu maandamano yaliyopita, leo watu wasingejitokeza.
kwa mbaaaaali! naiona Tanganyika tuitakayo inakuja!
picha mbalimbali zikionesha mapokezi ya viongozi wa bavicha wakiongozwa na mwenyekiti wa taifa, john heche, siku walipowasili mjini morogoro kwa ajili ya mafunzo ya uongozi kwa kamati ya utendaji ya baraza hilo, ambayo yatafuatiwa na kikao cha kikatiba, kitakachofanyika jumatatu, septemba 17, 2012. Polisi walikuwepo tangu mwanzo wa mapokezi hayo yaliyoanzia nje ya mji kidogo, eneo la nanenane, hadi ofisi za chadema mkoa wa morogoro. Ingawa baadhi ya waendesha pikipiki waliojumuika katika mapokezi hayo walilalamika kwa vyombo vya habari kuwa askari waliokuwa kwenye gari la chama walikuwa wanachukua namba za pikipiki zao. Haikujulikana kwa sababu gani (kubambikiwa kesi?).
Maandamano hayo ya kimya kimya ya pikipiki na magari, yakipita katikati kabisa ya mji, yawasisimua wananchi wa morogoro ambao walitokezea barabarani kuona chama chao kina shughuli gani mjini kwa siku hiyo, wengi wakiulizia 'mkutano wapi leo'.
View attachment 65218
View attachment 65219
View attachment 65220
View attachment 65221
View attachment 65222
View attachment 65223
View attachment 65224