Nilifikiri ni kwetu tu ndiyo wamekata, kumbe ni maeneo mengi (Dar, Tanga, Mara, Arusha, Dodoma, Iringa, Mbeya, Singida na Tabora). Basi labda grid ya taifa imetema, au kilio cha akina Yona, Muhongo, Ngeleja na Msabaha vinaisumbua Tanesco!! Tanesco isingefika hapa ilipo kama Prof Kapuya (Waziri wa Kazi enzi zile) asingewaingiza Net Solution pale Tanesco kwa nguvu ya polisi na ndipo hao Net Solution wakachangia kuporomoka kwa Tanesco; just like Mramba kuwaleta South African Airweays ili wasaidie kuua ATC, na sasa wembe umegeuzwa Fast Jet inaiua Preceision Air na inamuathiri hata Mramba mwenyewe (hii inaitwa boomrang effect).