Mood swings...wadada mbona mnakuwa hivyo?

Mara nataka ice cream saa saba usiku...mara nakuchukia kama nini...mara hamtaki tv ili mradi vurugu tu..
je kuna namna gani ya kupunguza hormones hizo za hasira na kulialia pia
kuwachukia waliowadungua ?
mna visa nyie!
hebu wenye experience ya vituko hivyo tujuzane..
hata nyinyi akina Ashadii mtuambie mlikuwa mna vituko gani?wengine nasikia mwapenda harufu ya ferry na hamlali na wenzi wenu....
karibuni

Shenzi type
 
Huwa ni vichekesho sana aisee,mke wa friend wangu alikuwa anavaa nguo za mumewe hasa fulana akiombwa azivue zikafuliwe timbwili lake hapo asha ngedere haoni ndani!
 
hayajamkuta..mtu kusikia hamu ya ugali saa 12 asubuhi

yaani, usiombe ukachukiwa sasa. Unaweza ukafukuzwa chumbani ukalale sebuleni. Ila hiyo ya soda ni kweli ilikuwa inamtokea mke wa rafiki yangu. Ngumu kuamini.
 
yaani, usiombe ukachukiwa sasa. Unaweza ukafukuzwa chumbani ukalale sebuleni. Ila hiyo ya soda ni kweli ilikuwa inamtokea mke wa rafiki yangu. Ngumu kuamini.
Hahahaha...mtoto aliyezaliwa angeitwa KEMPSIKI
 
Mimi nilipata bahati, alipobeba mimba akanipenda sana yaani akawa anatamani awe na mimi wakati wote, nikitoka kwenda kazini simu karibu siku nzima, nikirudi nyumbani yuko kifuani wakati wote naguswaguswa na kutekenywa, mpaka akawa anavaa mashati yangu ili ajihisi niko karibu naye. Niliipenda hiyo! Kizazaa sasa alipojifungua, lol (hiyo sitasimulia).
Kwa kuwa tunawapenda, basi tutavumilia yote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom