Ilipo ishia.
Monica: Niliona watu wenye nguo nyeupe wakitokea pande nne za dunia na mmoja wao akasema "muacheni kwanza huyu ngoja wengine wote tuwachukue" Nilijaribu kuongea kuwa uliza nyie ni nani lakini mdomo wangu ulikuwa mzito sikuweza hata kuongea, akilini ninawaza cha kusema lakini siwezi.
Part II inaendelea....
Monica: Nikasikia sauti mmoja akiita "Gabriel, Gabriel" mmoja wa hao watu akageuka, hakika nilishindwa kuiona vizuri sura yake, maana uso wake ulikuwa unag'aa mithili ya miale ya jua.
Yule aliyeitwa kwajina hilo alijibu akisema "Yuhiel mshike mkono mlete hapa"
Ndipo Monica alipo poteza fahamu na hakuelewa tena kitu gani kinaendelea.
Sauti za ndege akiimba zilisikika kwa mbali, wengine ni kama miluzi ya watu wanaofukuza mbwa mwizi, zingine kama kuku akitafuta sehemu ya kutagia. Kila aina ya sauti zilisikika.
Pale ndipo nilipo pata fahamu na kuona moshi mnene ukitokea upande wa kulia kwangu. Sikuelewa huo moshi ni kwaajili ya nini Monica alisema.
Hakuna mtu hata mmoja aliye baki isipokuwa Monica pekee yake maana basi liliteketea lote kwa moto. Hakuna mabaki yoyote yaliyobaki.
Ndipo Monica akaanza kulia kwa sauti ya huzuni akiita Mage, Mage, Mage uko wapi. Kila akiita mwangi ulisikika ukirundia maneno yake. Hakuna hata chembe ya kitu kilibaki pale.
Ilikuwa ni kama saa 12 alfajiri ndipo alipogundua kumbe amebaki peke yake. Majeraha madogo madogo kwenye mguu wake wa kushoto na mgongoni aliyapata. Kusema kweli Monica hakuumia.
Hakuelewa ni kitu gani kilichomfanya achomoke ndani ya gari pasipo yeye kuumia.
Ilikuwa kama umbali wa mita 20 kutoka barabarani, akiendelea kulia hakuna mtu yeyote aliye pita barabarani. Macho yake yalivimba na kuwa mekundu mithili ya mtu aliyepakwa pilipili kwenye macho. Mdomo wake ulikauka na pua yake kujaa makamasi kama mama aliyepotelewa na mwanae mpenzi.
Mda huo Monica alijipa matumaini huenda Mage yupo sehemu na kuendelea kuita kwa sauti. Mpaka pale sauti yake ilipokauka na kushindwa kabisa kuongea.
Njaa nayo ilianza kunyemelea tumbo lake, kichwa chake kilikuwa kizito kana kwamba kabeba mzinga wa maboksi ya chaki. Alikuwa akisikia sauti ndani ya kicha ikitwanga "kiko! kiko! kiko! kiko!" Mpigo yake ya moyo yakipiga haraka haraka.
Japo kuwa Monica alikuwa kwenye majonzi sura yake zuri ya kiafrika haikupotea. kadri alivyozidi kufumba macho na kufunga mdomo mashimo yalijitokeza kwenye mashavu yake mithili ya visima juu ya mawe ya engaruka.
Monica alichoka, hakuwa na wakumsaidia wala kuongea naye tu. Monica alizoa kusikia sauti za watu leo hii hakuna hata mmoja wa kuongea naye. Monica aliishiwa nguvu, ndipo usingizi mzito ukampitia
Je usingizi huo ulikuwaje endelea kufuatilia