Mongol Empire: Jeshi katili zaidi katika historia ya vita

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,463
2,000
Habari za jioni wana JF.....Tunapoongelea ukatili wa majeshi wengi watakimbilia kuwaza hitler alivyoua wayahudi au Jinsi Mehmet Ali alivyochinja chinja mataifa mbalimbali kwa kuitanua dola yake ya Ottoman... Ila wengi sidhani kama wanakumbuka ukatili mkubwa uliofanywa na Dola ya Mongolia na kuiacha dunia mdomo wazi na hata kuacha alama kubwa kwenye historia ya dunia.

images (64).jpg
Mongol Empire ilipatikana Asia ya kati na lilikuwa taifa dogo sana ila kufikia karne ya 13 AD chini ya kiongozi shupavu,jemedari Genghis Khan taifa hili liliamka kutoka kuwa kanchi maskini mpaka kuwa ufalme uliotawala ''dunia''. Genghis Khan alifanya mengi sana yanayostahili uzi wake ila kwa leo tujikite kwenye ukatili wa jeshi lake chini ya walioitwa "mbwa watano" ambao ni Kublai,Subotai,muqhali,Jelbe na Jelme. Hawa walikuwa magenerali muhimu sana kwa Genghis khan kiasi wakaweza kuitawala dunia kwa wakati wao. Walitumia sana majasusi,mbinu za kuzubaisha maadui na pia kutumia muda mrefu zaidi kumsoma adui ili wajue wanamtandikia wapi lakini kubwa zaidi na kiini cha uzi huu ni hii mbinu ya kisaikolojia waliyoitumia kutawala dunia, twende pamoja.

MBINU YA UKATILI
Mwaka 1219 Genghis khan alituma "mabalozi" kama 500 kwenda ufalme wa Kwaremzia (Iran-Afghanistan ya sasa) ili kutengeneza uhusiano wa kibiashara sasa mtawala wao akahisi watakuwa ni majasusi maana Genghis alifahamika sana kwa uwezo wake wa kutengeneza mfumo bora wa intelijensia.Hivyo akaamua kuwaua wote.... Genghis alipoona kimya akatuma tena wawakilishi watatu kufuatilia ila mmoja akachinjwa na wawili wakarudishwa na hiko kichwa. Huyu Sultan hakujua anacheza na Moto....!! Kilichofuata ni kipigo cha "mbwa mwizi" baada ya jeshi la Mongol kuzunguka utawala huu wakibaka,kuchinja na kuteketeza chochote kilicho mbele yao na mpaka vita inaisha walikuwa wameua robo ya wakazi wa ufalme huu yaani watu 1.25 Million.Kwa staili hii ya kuteketeza kabisa miji yaani kuua kila mtu,kubaka,kuchoma mji mzima n.k walijijengea sifa ya ukatili mbele ya falme zingine.

Mbinu waliotumia ni kuwatesa maadui kisaikolojia kwa kuwajaza hofu ili washindwe kupambana nao mfano wakati wanajitanua huko Asia walikuwa wakivuka vijiji na miji hata wakiwa na wanajeshi 10 tu hawakuti upinzani sababu walijua kitakachofuata ni kijiji kizima kufutwa kwenye ramani. Na Mongols walikuwa na tabia ya kuteketeza chochote kitakachomzuia kusonga mbele. Yaani wakifika wanakuambia chagua moja yaani ama surrender ama mchinjwe wote.
images (66).jpg

Mfano mwaka 1221, Western Xia huko china (Tibet ya sasa) walileta upinzani kwa Genghis Khan ambaye naye alijibu kwa kuwapa option 2 wajisalimishe au wateketezwe..... Xia ikaamua wapigane!!! Mbwa 5 wa Mongol wakaazimia kuteketeza Jamii nzima ambapo walichinja kuanzia wazee mpaka watoto,walibaka wanawake na kuteketeza makazi yao kwa moto hadi kupelekea kuufuta utawala huo kwenye ramani ya dunia.

Kwa ufupi mbinu hii iliwasaidia kumaliza vita haraka sana maana mataifa yalijisalimisha yenyewe hivyo kuwezesha kusonga mbele kwa haraka sana,bila kutumia rasilimali zozote au kupoteza muda hadi kufikia kuwa utawala mkubwa zaidi katika historia ya dunia.

UVAMIZI WA ULAYA
Mongols waliamua kutanua utawala wao kwa kuvamia ulaya kati ya mwaka 1237-40 na walifanikiwa kuiteketeza Urusi pia kuwachinja almost wanajeshi wote wa poland,Georgia,Bulgaria na Hungary. Katika tukio moja walipovamia Kiev (ukraine ya sasa) walitoa wito wajisalimishe lakini Wafalme wa Urusi walipogoma kusurrender mongols waliwavamia na kuwabananisha kati mto Kalka kiasi kwamba hawakuwa na pakukikimbilia na hapo ndipo walichinja kila mwanajeshi inaelezwa kuwa katika kila wanajeshi 10 wa Urusi ni 1 tu ndio aliyekuwa anasalia hivyo 90% ya Jeshi la wafalme wa Urusi hapo ukraine liliteketezwa kwenye uvamizi huu. Baada ya kuteketeza nchi za ulaya mashariki kma Georgia,croatia,poland na Hungary, walipanga sasa kuvamia mataifa yaliyobaki ya Ulaya na huku yakijawa hofu kubwa kwamba race ya wazungu ingeweza kufutwa kwenye uso wa dunia ghafla majeshi ya mongol yanapokea taarifa mbaya kwamba Khan(mfalme) wao Ogedei (mrithi wa ganghes) amefariki hivyo inabidi majeshi yarudi Mongolia yahakikishe anapatikana khan mpya na kuzima uasi wowote unaoweza jitokeza na hapo ndio ikawa pona ya ulaya kutoka mikono ya wakatili hawa.

Inaelezwa kwamba Mongol Empire iliteketeza zaidi ya watu million 40 kwenye vamizi zao inayowakilisha 10% ya watu duniani wakati huo ..... Kiufupi ndio uvamizi ulioua watu wengi zaidi katika historia maana ilikuwa ni chinjachinja mwanzo mwisho.
images (65).jpg
Sanamu ya Ganghes khan

SILAHA ZA KIBAIOLOJIA
Ikumbukwe kwamba licha tu ya ukatili wa kuchinja chinja ila Mongol empire walikuwa wavumbuzi wa kutumia silaha za kibaiolojia vitani inaelezwa na wanahistoria kupitia maandiko ya Gabrielle De Mursi kuwa Mongol walipouzingira mji wa caffa,1346 waliamua kutumia maiti zenye bacteria wa Yersinia pestis ambao walisababisha ugonjwa wa TAUNI hivyo mongols wakausambaza ugonjwa huu ambao uliteketeza mji huo na hata waliotoroka walienda kuambukiza miji ya jirani na kuwa mojawapo wa chanzo cha mlipuko wa ugonjwa wa tauni kusambaa ulaya ambapo mpaka unaisha uliua watu million 75..... Hivyo tunaweza kuona aina ya ukatili waliokuwa nao Mongols na kuwafanya kuwa moja ya jeshi tishio duniani.
images (67).jpg
HITIMISHO
kwa kuhitimisha nanukuu kitabu cha 48 laws of power sheria #5 SO MUCH DEPENDS ON REPUTATION-GUARD IT WITH YOUR LIFE... Yaani ''Kila kitu kinategemea sifa uliyojijengea - ilinde kwa maisha yako yote''. Sheria hii tunaona ndio iliwasaidia hawa Mongols kwamba walijulikana sifa yao ni ukatili na kwamba ukipingana nao basi umekwisha. Hii iliwasaidia maadui wao wawaogope hata kama wamekuja na jeshi dhaifu ila kwa ''sifa'' waliokuwa nayo walijikuta wakivuka falme nyingi bila kuzuiwa au upinzani wowote!!

Naomba kuwasilisha

Karibuni Wana JF intelligence wote
cc Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
 

Mr Miller

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
11,189
2,000
Iko series moja ya marcopolo ukiichek unapta kuona jeshi hili lilivyo hatari
Kweli walikuwa wanatisha sijui kwa nini walikuwa awajaja African au walimuogopa mansa musa
Kuna mtu aliwahi nambia kuwa hawa jamaa ndio asili/chimbuko halisi la wale jamaa wa vimacho vidogo wote yaani mjapani, mkorea, mchina, nk.
Mwenye ufahamu anifafanulie hapa kwa faida ya wote.
Hawa wapumbavu walikuwa wanawapika mateka wao nje ya mageti ya maadui wao kabla ya uvamizi. Pia walikuwa wanatanguliza mateka mbele wakienda vitani.
 

WILE

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
4,001
2,000
Kuna mtu aliwahi nambia kuwa hawa jamaa ndio asili/chimbuko halisi la wale jamaa wa vimacho vidogo wote yaani mjapani, mkorea, mchina, nk.
Mwenye ufahamu anifafanulie hapa kwa faida ya wote.
Siyo kweli wote walikuwepo kabla ya Mongols hawajavamia tawala zao na Japan ni sehemu pekee Khan alishindwa kuvamia baada ya kujaribu mara mbili akafariki lakini kilichowaokoa wa Japan ni bahari.
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,463
2,000
Kuna mtu aliwahi nambia kuwa hawa jamaa ndio asili/chimbuko halisi la wale jamaa wa vimacho vidogo wote yaani mjapani, mkorea, mchina, nk.
Mwenye ufahamu anifafanulie hapa kwa faida ya wote.
Nachofahamu kabla wataalam hawajaja ni kwamba Mongol Empire iliikuta china ikiwepo tayari ndio maana kwenye uzi nimeongelea Mongols walivamia western Xia mpaka hapo inaifanya china kuwepo kabla ya Mongol Empire..... Pia kuna wakati Mongols walitaka kuvamia visiwa vya Japan ila walishindwa hivyo kufanya wajapan kuwepo kabla ya Mongols

Ambacho huyo jamaa alikwambia na ni sahihi kwamba chinese na japanese ni race ya MONGOLOIDS lakini haina connection yoyote na Mongol empire ila ni kwamba jamii yote ya chinese,japan,korea,mongolia n.k zipo classified kama Mongoloids sababu kiachiolojia eneo la mongolia la leo ndio ilipo asili ya watu hao wa Asia

Wataalam zaidi watanisahihisha
 

G.Jacob

JF-Expert Member
Aug 12, 2013
3,495
2,000
Nachofahamu kabla wataalam hawajaja ni kwamba Mongol Empire iliikuta china ikiwepo tayari ndio maana kwenye uzi nimeongelea Mongols walivamia western Xia mpaka hapo inaifanya china kuwepo kabla ya Mongol Empire..... Pia kuna wakati Mongols walitaka kuvamia visiwa vya Japan ila walishindwa hivyo kufanya wajapan kuwepo kabla ya Mongols

Ambacho huyo jamaa alikwambia na ni sahihi kwamba chinese na japanese ni race ya MONGOLOIDS lakini haina connection yoyote na Mongol empire ila ni kwamba jamii yote ya chinese,japan,korea,mongolia n.k zipo classified kama Mongoloids sababu kiachiolojia eneo la mongolia la leo ndio ilipo asili ya watu hao wa Asia

Wataalam zaidi watanisahihisha
Nadhani nilikosea kuuliza Swali lakini hapo kwenye phrase ya mwisho umejibu exactly nilichokimaanisha kwamba chimbuko la kiasili la hiyo Jamii ya watu wenye vimacho vidogo kwa maana ya mongoloids ni Mongolia.

Ahsante mkuu.
 
Top Bottom