Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Bob Mkandara, ni mtu ambaye amejikwamua kiubunifu na kujijenga kiuchumi. Ni juhudi zake mwenyewe na kutokukata tamaa au kutafuta njia nyepesi na rahisi kujipatia pesa kukimu maisha yake ndiko kulikonifanya nimtumie kama mfano kuhusu mada yangu mpya.
Sisi kama Taifa, tunatatizo moja kubwa ambalo linabidi tulifanyie kazi kwa mwendokasi wa mwanga na tusiendekeze kusubiri kesho kama tulivyoafanya kwa miaka 46!
Tatizo hili ni fedha.
Fedha, Nyerere na Azimio walisema, si msingi wa maendeleo, bali ni kitendea kazi cha kuleta maendeleo na msukumo wa kuimarisha maisha ya binadamu.
Sisi kama Taifa, hatujajua ni thamani ya pesa kwa kuwa tumelelewa kwa kusaidiwa pesa za misaada au kupokea mishahara lakini si kwa ajili ya uchapaji kazi au ubunifu.
Katika moja ya vitu tunavyojitahidi kukwepa kuvizungumzia ni matunda bora ya Ujamaa na Azimio la Arusha. Tumekimbilia kulaani kuangamia kwa viwanda na uzalishaji mali, huku tumesahau kuwa viwanda na mashirika haya, yalitumia mapato (fedha), kujenga middle class ya Tanzania ambayo ilihemea kuajiriwa na kupewa mshahara na marupurupu mengi, bila kuwa wabunifu wa kuongeza Tija au Ufanisi katika uzalishaji mali.
Pesa tunazo na utajiri tunao, lakini hatuna maadili ya kutuadabisha katika utumiaji wa fedha, hatuna mipango mizuri ya kuongeza fedha kwa kutumia uzalishaji mali na ubunifu, Hatuna uwezo wa kutumia vyanzo vyetu wenyewe kujizalishia mali na kuongeza fedha katika mifuko yetu na kuishia kuwa ombaomba.
Nimetaja vitu vitatu hapo juu. Maendeleo, Maadili na Kujitegemea. Fedha inaweza kupatikana kama jamii in nia ya kweli kuwa na maendeleo ambayo yanakwenda sambamba na maadili ili kujijengea kuwa Taifa na jamii inayojitegemea. Utashangaa ni jinsi gani maneno haya matatu yameweza kujenga sentenso nzuri sana ya kujjipa tumaini.
Umasikini, Unyonge, Uhujumu na Ufisadi, ni matokeo ya kutokuwa wawajibifu katika kuzalisha mali, kutunza thamani ya mali na fedha, kukosekana kwa dhamira ya uchapa kazi na kukosa ubunifu katika kuzalisha na kujipatia fedha.
Tumezoea kupewa vya dezo na kama ule wimbo wa "Kasimu", tunajua kuzitumbua fedha, lakini hatujui jinsi gani ya kuwa wazaishaji wa pesa hizi.
Ukosefu wa maadili ambao umeanzia katika oungozi, umeteremkia katika jamii. Kila mtu anataka pesa, na za haraka haraka, hatutaki kufanya kazi, hatutaki kuwa wabunifu, lakini twataka tuishi kwa neema ya kutafuna jibini na mkate wa kukaanga.
Nimegusia kuanguka kwa mashirika katika kujenga tabaka la kati (middle class). ni ukweli usiofichika kuwa kukosekana kwa ubunifu wa kuongeza ufanisi kulichangia kuanguka kwa mashirika na viwanda. La zaidi, kutolewa holela kwa ajira bila kuangalia na kujihoji kama kuongezeka huku kwa ajira kunawiana na uzalishaji mali na mapato.
Sisi kama Taifa, tulibahatika kujijenga kwa juhudi za kufadhiliwa na si kufanya kazi kwa kujituma au kuwa wabunifu wa vianzo vipya vya kazi au kuendeleza na kupanua vile tulivyorithi kutoka kwa mkoloni.
Hivyo basi, wakati tunapigana vita vya ufisadi ambavyo msingi wake mkuu ni tamaa na uvivu wa kuchapa kazi na kukimbilia kushiba haraka haraka, inabidi tujihoji nafsi kama jamii na Taifa.
Je tukishawafunga Mafisadi wote na kuing'oa CCM, ndi mwanzo wa neema na kutajirika? ndio mwanzo wa kuondoa umasikini na kuleta ubunifu, uwajibikaji, uchapakazi hodari, umakini na udhibiti ili tuiongeze mapesa na kuweza kuwa na huduma bora za jamii na kuwa Taifa linalojitegemea?
Jiulze kibinafsi, je mimi ni mbunifu, mchapa kazi, mwajibikaji, mwadilifu na najua thamani ya pesa na naweza kuizalisha marudufu na kudhibiti isipotee thamani?
Ndio maana namtolea wasifu Bob Mkandara. Yeye ni mmoja katika laki katika Taifa letu.
Ni mpaka pale ambapo tutaanza kujielimisha jinsi ya kutumia pesa na kuwa na malengo muhimu na kutumia pesa hizi kwa malengo ya muhimu na si kutumia tuu kwa kuwa zipo au tutapewa hundi la MDC kutoka kwa Marekani, WB, EU na IMF ndipo tunaweza kuleta maendeleo na kuweza kujitegemea. Kinyume cha hilo, tutaendelea kuwa "Kasimu bin Matanuzi" na hata wakija CUF na CHADEMA, tutaendelea kuzitumbua na kutokujali kuwa pesa, yahitaji kuitumikia.
"Kwa jasho la uso wako utakula chakula" Mwanzo 3:19, sisi tunahemea jasho la wenzetu ndio maana hatuna uchungu na pesa!