figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea wa CHADEMA kwa kivuli cha UKAWA mwaka 2015 Mheshimiwa sana Edward Lowassa, Amekutana na Balozi wa Japan Nchini Bwana Masaharu Yoshida Wilayani Monduli.
Ujio wa Balozi huyu Monduli, umemfurahisha Kiongozi Msafi(asiye na kashfa yoyote) na mnyenyekevu Mheshimiwa Edward Lowassa. Amefarijika sana kuona watu wanamuunga mkono na ametumia nafasi hiyo kumshukuru.
"Nimekutana na Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida pamoja na viongozi wote wa wilaya yetu ya Monduli. Napenda kumshukuru Balozi Yoshida kwa misaada mbalimbali wanayoitoa na wanavyoendelea kudumisha udugu mwema" amesema Mheshimwa Lowassa ambaye alikua Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nafasi inayoheshimika nchini na kwa muda mdogo alokaa kwenye nafasi hiyo, alileta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo nchini na kuamsha hali ya Uwajibikaji. Mungu azidi kumlinda na kumbariki Mheshimiwa Lowassa.