Mombasa: Mwanaume ajichoma moto kupinga hali ngumu ya maisha

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Mwanaume mmoja amelazwa Hospitali nchini Kenya baada ya kujichoma moto katika eneo la Mwembe Tayari Kaunti ya Mombasa huku chanzo cha kufanya hivyo kikiwa bado hakijafahamika ingawa taarifa za awali zinasema sababu ni kutuma ujumbe kwa serikali kuhusu ugumu wa maisha.

Video inayosambazwa mtandoni inamuonesha Mtu huyo ambaye inadaiwa kuwa ni Mwanafunzi wa Engineering, akiwa anajimwagia mafuta kisha kujichoma moto akiwa amesimama kwa juu na kufanya Mashuhuda wapige kelele na kupata taharuki.

The Citizen Kenya wanaripoti kuwa Mwanaume huyo ambaye jina lake halijafahamika anaendelea kutibiwa kufuatiwa majeraha aliyoyapata kabla ya kusaidiwa na Wasamari wema ambao waliuzima moto, Polisi Kenya bado hawajatoa taarifa kuhusu tukio hilo.
 
Mwanaume mmoja amelazwa Hospitali nchini Kenya baada ya kujichoma moto katika eneo la Mwembe Tayari Kaunti ya Mombasa huku chanzo cha kufanya hivyo kikiwa bado hakijafahamika.

Video inayosambazwa mtandoni inamuonesha Mtu huyo ambaye inadaiwa kuwa ni Mwanafunzi wa Engineering, akiwa anajimwagia mafuta kisha kujichoma moto akiwa amesimama kwa juu na kufanya Mashuhuda wapige kelele na kupata taharuki.

The Citizen Kenya wanaripoti kuwa Mwanaume huyo ambaye jina lake halijafahamika anaendelea kutibiwa kufuatiwa majeraha aliyoyapata kabla ya kusaidiwa na Wasamari wema ambao waliuzima moto, Polisi Kenya bado hawajatoa taarifa kuhusu tukio hilo.
Huyo labda atakuwa Coco reborn aka kipcoco kipreborn🤣🤣
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom