VIDEO - Ajichoma Moto Kupinga Hali Ngumu ya Maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Ajichoma Moto Kupinga Hali Ngumu ya Maisha

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Jul 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  <tbody>[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG]
  Mwanaume wa nchini Israel alipojichoma moto kupinga hali ngumu ya maisha[/TD]
  [TD]Tuesday, July 17, 2012 9:16 AM
  Mwanaume mmoja wa nchini Israel, amejichoma moto katika kupinga hali ngumu ya maisha na gharama kubwa sana za mahitaji ya lazima.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 40, alijimwagia mwenyewe mafuta ya taa na kujichoma moto mbele ya maelfu ya watu waliokuwa wakiandamana mjini Tel Aviv kupinga gharama kubwa na hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi wa Israel.

  Tukio hilo lilionyeshwa LIVE na televisheni ya Channel 10 ya nchini Israel na kuwaonyesha jinsi baadhi ya waandamanaji wakijaribu kuokoa maisha ya jamaa huyo kwa kujaribu kuuzima moto huo kwa kutumia maji toka kwenye chupa za maji ya kunywa.

  Mwanaume huyo aliungua vibaya na jitihada za kuuzima moto huo zilifanikiwa kwa msaada wa polisi wa Israel waliowahi kufika eneo la tukio.

  Katika hali ya kushangaza mwanaume huyo huku akiwa ameungua vibaya na nguo zake zote zikiwa zimeungua, alianza kuramba ice cream aliyopewa na mmoja wa wanawake waliokuwa wakiandamana.

  Huku akinyoosha mikono yake juu kuonyesha ishara ya ushindi mwanaume huyo alipakizwa kwenye ambulansi na kuwahishwa hospitali ambako anaendelea kupatiwa matibabu ya majeraha ya moto huo uliounguza sehemu kubwa ya mwili wake.

  Angalia VIDEO ya tukio hilo chini[/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli...........
   
 3. KABAVAKO

  KABAVAKO JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Serikali ya Israel inatumia fedha zote kukandamiza waarabu badala ya kutoa huduma bora kwa watu wake
   
 4. D

  Dopas JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni kama serikali ya CCM kutumia hela zake kwa matanuzi na safari za viongozi badala ya kutoa huduma bora kwa wananchi wake.
   
Loading...