Mung Chris
JF-Expert Member
- Sep 12, 2017
- 3,474
- 4,007
Unapo omba kazi lazima tuwe makini na CV zetu zinavyojieleza na grammar spelling, public sector au ajira za serikali huwa hawajali na grammar au spelling wanaangalia tu kama ulisoma basi ila private sector wengi wao wako makini sana mfano NGOs zinazoongozwa na watu wa nje au watanzania wenye elimu makini sana huwa wanasoma kiingereza ulicho kiandika kwenye CV na kujua kama unaweza kujieleza au la, huwa inatokea wengine wanaweza kujieleza ila kuandika hawawezi wakati mwingine huwa najiuliza, kwanini unachokizungumza huwezi kuandika kama unavyo zungumza hapo ndipo huwa nagundua kuwa anayeweza kuzungumza vizuri lakini hawezi kuandika basi ni mvivu wa kusoma ndio maana hawezi kuandika.
Huko unapotuma CV yako endapo CV ina makosa mengi ya grammar wanajua hukuiwasilisha kwa bahati mbaya ila uliandika ukaipitia ukaelewa ndio ukawasilisha, basi hapo ndio huwa wanasema **** aliwasilisha hivi basi kujieleza itakuwa taabu. Hapo chacha.
Nawashauri tuliangalie hili, tuwe makini sana, kama hatujiamini tuwape watu wengine wapitie CV zetu waangalie grammar baada ya hapo watushauri ili isitokee tukakwama kwa sababu hilo.