Mohammed Hussein Tshabalala 'asinya' Simba SC mbele ya Kocha Mkuu Profesa Gomez

Sii manager wake alisema au ndio ilikuwa kuwatingisha kidogo simba
Sikutaka kuisema hii Siri ila kwa Faida ya wengi na nikiwa Mdau ( Mtu ambaye nilishakutana nayo sana ) ngoja leo niiweke wazi.

Kinachofanyika huwa tunakiita ( Kujambisha ) au ( Kupigisha Shoti ) ambapo Mchezaji husika au hata Meneja wake wakiona yupo katika Kiwango kizuri na Mkataba unakaribia kumalizika hutafuta Waandishi wa Habari au Wahariri wao.

Kisha Mchezaji au Meneja wake huwaambia hawa Waandishi wa Habari au Watangazaji wa Redio na hata Runinga kuwa wajambishe ( watishie ) Mchezaji ama anahamia kwa Mahasimu Yanga au Simba.

Taarifa za Mchezaji huyo kutaka Kuhamia kwa Timu Pinzani ( Hasimu ) zikienea kawaida Matajiri wa hivi Vilabu ( Mo Dewji na GSM ) huogopa na Presha kutoka kwa Mashabiki nayo hupanda hivyo haraka sana huamua Kumuita Mchezaji au Meneja wake ili Kumalizana haraka kwa kuingia nae Mkataba mpya.

Mchezaji akishasinya ( akiingia Mkataba ) tu kama Mfano akiwa amepewa Tsh Milioni 100 za Mkataba mpya Meneja wake atachukua 10% mpaka 15% kulingana na walivyokubaliana ila kwa Wale Waandishi wa Habari ( mpaka Watangazaji wa Redio na Runinga ) walioshiriki katika Kupigisha Shoti ( Kutishia Nyau ) nao kila Mmoja hupewa Asante ya Tsh 500,000/= ya Kufanikisha zoezi zima.

Baada ya Mjambisho ( Kupigisha Shoti ) kwa Wachezaji wa Simba SC kumalizika ( kuisha ) Leo muda wowote kuanzia sasa tegeeni Sikio kuna Wachezaji Watatu wa Yanga SC ( Mmoja Mzawa na Wawili wa Kigeni ) nao wataingia katika Mchezo huu huu wa Kupigishana Shoti ( Kujambisha ) huku wakihusishwa kutakuwa na Simba SC na najua kwa jinsi Yanga SC na GSM wanavyowahitaji hawa Wachezaji ni lazima tu wataufyata Kwao na watamalizana nao kwa kuwapa Pesa ndefu ya Mkataba mpya.
 
Back
Top Bottom