RIP dear soldiers, ila ndg zangu Watz. Hawa polisi ni sehemu ya jamii yetu. Hakuna sababu ya kuwachukia, mimi naamini kuwa nao hawapendi kufanya yale ambayo yanakera watu ila wanalazimishwa na mfumo wa utawala. Sitaki kutoa mfano maana mahali hapa sio pake. tusifurahie kufa kwao, hebu jaribu kufikiri ni familia ngapi zimeathirika kutoka na hili? fikiria wawe sehemu ya familia yako ungeyasema hayo unayoyasema sasa.
MUNGU ZIFARIJI FAMILIA ZOTE Zilizopatwa na misiba hii mizito,
Ee Bwana Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, uturehemu, msiba huu utukumbushe kuwa sisi tu wapitaji tu katika ulimengu huu, maana hatudumu daima, Tumekutenda dhambi kwa kuwaza, kwa kunena na kutenda. Tumepungukiwa na utukufu wako,tunakuomba uturehemu. Tunakuomba usiukumbuke uovu wetu, utakapofika wakati wetu wa kuondoka katika uso wa nchi basi tufe vema tukiwa katika mikono yako ambayo ni salama, AMINA.