Modern-Day Slavery on D.C.'s Embassy Row? [Afisa Balozi wetu Mzengi na Utumwa mpya?]

Atalipaje hizo dola kudadeki..kwa kipato gani? kweli nchi yajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye choyo.
 
Lakini kama tunamkopesha kuna ubaya gani? Atupe hati za nyumba kama mbili tatu hivi na tumkopeshe hiyo $170,000 ataturudishia na interest yetu ya 30% p.a. kwa 4 or 5 years akishindwa nyumba tunachukua, imekaaje wadau?
 
mbu sugu, asante kwa hii observation yako.

Wanabodi, naombeni tusikurupuke kumshutumu Balozi Maajar.
Maofisa wote wa ubalozi wa nchi zote, wanalindwa na kitu kinachoitwa Diplomatic Immunity under Vienna convention ambapo ofisa ubalozi haruhusiwi kishitakiwa kwa kosa lolote la jinai, ila akifanya jinai huku ana kinga ya kibalozi, then atashitakiwa yeye binafsi, ila nchi husika hutakiwa kufanya haya yafuatayo kwa haraka kadri iwezekanavyo.

1. Kumvua kinga ya kibalozi, hivyo kumruhusu kusimama mahakamani na akikutwa na hatia, huwajibika binafsi hata kama ni jela hufungwa.
2. Nchi husika humrejeshas nyumbani kwa haraka, hivyo kumpatia shield aganst local prosecution, hiki ndicho Tanzania ilichokifanya na ndicho kinachofanywa na nchi nyingi.
-Wale Wataliano waliowalazimisha dada zetu kulala na mbwa ndio waliokolewa kihivi
-Wanabalozi fulani wa nchi ya kiarabu alimbaka msichana wake wa kazi na kuokolewa kihivi
-Mwanabalozi wa Canada aliyemtemea mate Jerry Muro, pia iliokolewa kihivi.
3. Lengo la kuwarejesha nyumbani maofisa hao ni kukwepa legal liability kwa sababu ili kuendesha kesi ya kihivyo, unatakiwa kutumia Private Internation Law ambayo legal fees zake ni very expensive.
4. Huyu binti ametetewa na wanasheria wa msaada wa kisheria, na kushinda kesi. Kwa vile mhusika alitenda kosa akiwa na kinga ya kibalozi, na Tanzania haikumuondolea kinga bali kumrejesha tuu nyumbani na kumpa kazi nyingine, serikali ya Tanzania haiwajibiki kwa deni lake, wala haiwajibiki kulipa, kumlipia, wala kumkopesha bali kitendo cha ofisa mhusika kushindwa kulipa, kutaichafua Tanzania mbele ya jumuiya ya kimataifa.
5. Anachosema balozi Maajar, ni just saving the face of Tanzania, tusikubali kuacha jina la Tanzania likichafuliwa eti kwa sababu ya mpuuzi mmoja aliyefanya mambo ya kishenzi kwa kasichana ka kazi.
6. Kama ilivyo kwa mtoto chini ya miaka 18, akifanya jinai ya madai, mzazio wake atawajibika kumlipia to save his face, ndivyo hivyo Tanzania inavyowajibika kumlipia mpuuzi huyu to save our face!. Balozi Maajar is right.
7. Hii sio mara ya kwanza kwa ofisi za ubalozi kulipa madeni ya watu binafsi na huku serikali ikiwadai wahusika. Kwa wenye kumbukumbu mtakumbuka kisa cha mtoto wa Msekwa ughaibuni, alichuma janga, Baba wakati huo akiwa spika, akakopeshwa, soo likamalizwa, huku nyumbani Msekwa akadaiwa na kulipa mwaka juzi!.

Nadhani mjumbe uko sahihi hata nakumbuka miaka ile kaka zetu walikuwa wakidandia meli kwenda 'mtoni' wakikamatwa wanarejeshwa kwa fedha za serikali ila ilikuwa kazi pale minazi mirefu jamaa wanakupeleka ukonga mpakandugu zako walipe deni! Du
 
Mhhh,makubwa haya , sasa balozi anataka kodi zetu zitumike kumlipia?

Huyu Zipora ni kutoka taifa gani? ni mtanzania ama kutoka nchi gani?

Hii imenikumbusha kisa cha mbunge wa kule Uingereza na house girl wake .........
 
Niliwaahidi kuweka kumbukumbu za kikao cha balozi na mawakili wa Zipora , ntaziweka sasa maana zimefika kwa ukamilifu wake.
 
KUMBUKUMBU ZA MKUTANO KATI YA MHE. BALOZI MWANAIDI SINARE MAAJAR NA WANASHERIA WA ZIPORA MAZENGO KUZUNGUMZIA HUKUM YA MAHAKAMA YA UNITED STATES DISTRICT COURT FOR THE DISTRICT OF COLUMBIA KWA MADAI YA USAFIRISHAJI HARAMU WATU DHIDI YA DR. ALLAN MZENGI

Jumla
Tarehe 1 Novemba, 2010 kulifanyika mkutano kati ya Balozi Mwanaidi Maajar na wanasheria watatu wanaomwakilisha Zipora Mazengo kutoka kampuni ya Mawakili ya hapa Washington ijulikanayo kama Jenner & Block. Madhumuni ya mkutano ilikuwa kuzungumzia hukumu inayomkabili Dr Allan Mzengi kwa madai ya usafirishaji haramu mfanyakazi wake wa ndani Bi Zipora Mazengo na kumtumikisha bila malipo kinyume na sharia za hapa Marekani. Wanasheria waliohudhuria katika mkutano huo ni Martina E. Vandenberg na Lorelie S. Masters ambao ni mapatna katika kampuni hiyo ya mawakili na Daniel I. Weiner ambaye ni wakili wa ngazi ya kawaida. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Hukumu hiyo ilitokana na madai ya Bi Zipora kuwa aliletwa Marekani na Dr. Mzengi na mkewe kwa ahadi ya kufanya kazi kwa malipo halali lakini kinyume chake hawakumlipa mshahara wowote wakati wakimfanisha kazi kama mtumwa kwa massa 15 kila siku na bila kumruhusu kurejea Tanzania kwa miaka mine hata pale alipofiwa na ndugu yake. Alidai pia walizuia pasi yake na pia walimfanyisha kazi ya kupika chakula cha baishara ya kupika aliyokuwa akiifanya mke wake Dr. Mzengi. Alidai pia hata alipoumwa hawakumpeleka hospitali hadi alipozidiwa sana na wakati mwingine alikuwa anapigwa.
Dr. Mzengi hakutetea kesi hiyo kwa kuwa alidai haki ya kinga yake ya kibalozi. Hata hivyo kwa msingi wa Vienna Convention, kufuatana na madai kuwa alikuwa akifanya biashara nyumbani kwake madai ya kinga huenda yasingesimama mahakamani hapa Marekani. Hata hivyo ingekuwa kazi ngumu sana kwa Dr. Mzengi kukanusha madai ya kufanya biasahara kwa kuwa aliyemsaidia Zipora kutoroka alikuwa ni mteja wa mkewe Dr. Mzengi katika biashara hiyo ya chakula. Kwa maana hiyo kinga ya kibalozi ya Dr. Mzengi ilikuwa mashakani.
Katika hukumu ya mahakama Dr. Mzengi na mkewe wameamriwa kumlipa Zipora kiasi cha Dola za Kimarekani milioni moja na laki elfu hamsini na tisa, mia tatu arobaini na nane na point sabini na tisa ($1,050,348.79).
Majadiliano
Wanasheria wa Zipora walikuja kutaka kujua msimamo wa serikali ya Tanzania kuhusu fidia kwa Zipora Mazengo kutokana na hukumu ya kesi ya usafirishaji haramu watu dhidi ya Dr Allan Mzengi.
Balozi maajar aliwaeleza kuwa serikali ya Tanzania inaheshimu sheria za Marekani na pia inaheshimi hukumu itokanayo na mahakama za Marekani ingawa kwa mujibu wa sheria za Tanzania ni lazima hukumu hiyo ipelekwe Tanzania ikubaliwe na mahakama za Tanzania ili iweze kuwa ni hukumu inayotambulika kisheria. Alisema pia kuwa Tanzania ina dhamira ya dhati ya kupambana na biahara ya usafirishaji haramu wa watu duniani ndiyo maana Bunge la Tanzania limepitisha sheria The Anti-Trafficking in persons Act, (Act No-15 of 2008) ambayo imeanza kutumika mwaka jana 2009. Balozi Maajar alieleza nchini Tanzania kuna mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na vita dhidi ya biashara hii haramu na kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya biashara hii na kwamba serikali inaunga mkono shughuli zinazofanywa na mashirika hayo na pia imeanza kuimarisha vyombo vya dola vya utekelzaji wa sheria dhidi ya biashara haramu ya watu.
Akizungumzia kuhusu hukumu ya kesi dhidi ya Dr. Mzengi, Balozi Maajar aliwaeleza wanasheria hao kuwa hukumu hiyo si dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni dhidi ya Dr. Mzengi ambaye ni mwajiriwa wa Serikali. Aliwaeleza kuwa hukumu hii inatakiwa kuthibitishwa na mahakama za Tanzania kwa kufuata taratibu za kisheria zilizopo. Bila kufanya hivyo ni vigumu kwa serikali ya Tanzania kusimamia utekelezaji wa hukumu hiyo. Kwamba kama hukumu hiyo itakaziwa na mahakama za Tanzania, serikali inaweza kuitekeleza ikiwemo kukata mshahara wa Dr Mzengi pamoja na stahili zake nyingine ili kumlipa Zipora.
Kuhusu serikali kulipa kwa niaba ya Dr Mzengi, Balozi Maajar aliwaeleza wanasheria hao kuwa serikali haiwezi kulipa kiasi cha fedha kinachodaiwa kulingana na hukumu hiyo kwa vile ni kinyume cha taratibu za fedha za nchi. Kufanya hivyo kutapelekea kuwepo hoja za wakaguzi wa hesabu za serikali kutoka kwa mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali na pia hoja za kamati ya bunge inayosimamia hesabu za serikali ambayo mwenyekiti wake huwa ni mbunge toka chama cha upinzani.
Sheria za Tanzania
Wanasheria hao waliomba serikali ya Tanzania ibadilishe sheria zake ili kuwezesha hukumu zinazotolewa na mahakama za nchini Marekani kutekelezwa nchini Tanzania. Kwamba wamefanya utafiti na kugundua kuwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania, hukumu zinazotolewa na mahakama za Marekani haziwezi kutekelezwa nchini Tanzania.
Waliendelea kueleza kuwa hawako tayari kwenda Tanzania au kuajiri wanasheria ili kuwezesha hukumu iliyopo kutekelezwa nchini Tanzania kupitia utaratibu wa sheria za Tanzania. Walisema kuwa gharama za kufanya hivyo ni kubwa sana na hawako tayari kuingia katika gharama nyingine kwani hadi hivi sasa wametumia zaidi ya dola za Marekani Laki tatu ($330,000) kwa ajili ya kugharamia kesi hii. Walisema pia kuwa hawana imani na mahakama za Tanzania kwa vile zimejaa rushwa.
Wanasheria hao waliomba Serikali ya Tanzania kumuadhibu Dr. Mzengi kwa kumfukuza kazi na wanataka serikali itunge sheria ili kuweza kumshitaki Dr. Mzengi. Walidai kuwa Dr. Mzengi badala ya kuadhibiwa alipandishwa cheo na kupangiwa kazi katika ofisi ya Rais (Ikulu).
Akijibu hoja hizo, Balozi Maajar aliwaeleza kuwa serikali ya Tanzania na Ubalozi kwa ujumla wanaheshimu hukumu ya mahakama iliyopo dhidi ya Dr Mzengi. Hata hivyo ili hukumu hiyo iweze kutekelezwa Tanzania na ili Serikali iweze kusaidia utekelezaji wake, ni lazima utaratibu wa kisheria uliopo kuhusu hukumu za nje ufuatwe kikamilifu. Aliwaeleza kuwa hata kama sheria ingetungwa isingehusu makosa yaliyofanyika kabla ya sheria hiyo kutungwa.
Balozi Maajar aliwaambia wanasheria hao kuwa njia wanayotumia ya kutoa mashinikizo na propaganda za kuichafua Tanzania kupitia Bunge la Marekani, Serikali ya Marekani (Wizara ya Mambo ya Nje), Vyombo vya habari na taasisi nyingine zinazojihusisha na masuala ya haki za binadamu haiwasaidii katika kupata malipo ya fedha wanayodai. Balozi aliendelea kusisitiza kuwa serkali ya Tanzania haiwezi kulipa chochote kutokana na hukumu ambayo si dhidi yake licha ya mashinikizo yanayotolewa na wanasheria hao.
Balozi alisisitiza kuwa njia nzuri ya kuwawezesha kupata haki yao ni kufuata utaratibu wa kisheria wa kuikaza hukumu hiyo nchini Tanzania. Balozi aliwaambia wanasheria hao kuwa yuko tayari kuwasaidia katika kuwapatia majina ya makampuni na wanasheria nchini Tanzania ambao wanaweza kuwasaidia katika suala hili.
Kuhusu kumuadhibu Mzengi, Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa Mzengi aliadhibiwa kulingana na taratibu za utumishi wa umma nchini. Kwamba serikali haiwezi kufungua kesi dhidi ya Dr. Mzengi kutokana na hukumu iliyotolewa nchini Marekani na ambayo haijapata uhalali wa kutekelezwa nchini. Aliwaeleza kuwa hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kufanya jambo hilo ikiwamo serikali ya Marekani.
Akijibu ombi lao la kutaka Dr Mzengi afukuzwe kazi, Balozi aliwaeleza kuwa serikali haiwezi kumfukuza kazi bila sababu za msingi na bila kufuata taratibu na sheria za nchi, kwani kwa kufanya hivyo serikali itashitakiwa mahakamani na itashindwa. Aliwaeleza pia kuwa iwapo Dr. Mzengi atafukuzwa kazi hatakuwa na uwezo tena wa kulipa pesa hizo wanazotaka alipe hivyo Zipora hatapata chochote kutokana na hatua hiyo.
Kuhusu kupandishwa cheo, Balozi alikanusha kuwa Dr. Mzengi hajapandishwa cheo na kwamba kwa anavyojua yeye Mzengi hafanyi kazi katika ofisi binafsi ya Rais kama wanasheria hao wanavyodai.
Malipo
Kufuatia kauli ya msisitizo kutoka kwa Balozi kuwa serikali ya Tanzania haiwezi kulipa fedha inayodaiwa kama zilivyofanya serikli za Oman na Saudi Arabia kutokana na taratibu za fedha kutoruhusu, na shaka kama fedha hizo zote ni za Zipora na siyo kwamba kiasi kikubwa ni cha mawakili hao walisema kuwa wao wanafanya kazi hii kama msaada tu (pro bono) na si kwa masilahi yao binafsi na kwamba hawategemei fedha yoyote kutokana na hukumu hiyo. Walieleza kuwa hata wao wanajua wazi kuwa Dr. Mzengi hawezi kulipa kiasi cha fedha cha zaidi ya Dola za Kimarekani Million moja zinazodaiwa. Aidha walisema kuwa hata Zipora hatarajii kupata kiasi hicho cha fedha na kwamba kiwango cha chini kabisa wanachotegemewa walipwe ni Dola za Kimarekani laki mbili elfu kumi na sita ($ 216,000), ikiwa ni laki moja sabini na saba elfu ($ 177,083.00) zikiwa mishahara inayodaiwa na Zipora ambayo anadai hakulipwa kwa miaka minne aliyofanya kazi na kiasi kilichobaki ni faini mbali mbali (compensatory damages).
Mengineyo
Wanasheria hao walihitimisha hoja zao kwa kueleza yafuatayo:
· Wanaomba Dr. Mzengi aendelee kuwekewa shinikizo ili atoe utaratibu wa jinsi atakavyolipa pesa hizo anazodaiwa hususan mishahara ambayo haikulipwa (back wages).
· Waliahidi kuacha kampeni chafu dhidi ya Tanzania kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo ili kutoa nafasi kwa serikali kulishughulikia suala hili. Walitaka kupata ahadi kutoka kwa Balozi ni lini suala hili litamalizika.
· Wanataka kupata majibu ya "Demarche" iliyopelekwa serikali ya Tanzania.
· Walisisitiza kuwa hawataacha kufuatilia suala hili hadi ufumbuzi wake upatikane. Kwamba wataendelea kuwasiliana na Bunge la Marekani na Wizara ya Mambo ya Nje hadi hapo suluhu itakapopatikana.
· Walitaka kujua hatua za kuchukuliwa iwapo Dr. Mzengi atakubali kuanza kulipa na baadaye kuacha kulipa.
· Walitaka kujua mchakato wa maombi ya pasi ya kusafiria ya Zipora Mazengo yaliyowasilishwa ubalozini umefikia wapi.
· Walisema kuwa wizara ya usalama wa Ndani ya Marekani imemtambua na kumthibitisha Zipora Mazengo kama muathirika wa biashara haramu ya usafirishaji watu na imempa visa ambayo inamuwezesha kuishi na kufanya kazi Marekani katika uhai wake wote.
Akijibu hoja hizo, Balozi Maajar alisisitiza yafuatayo:
· Kampeni chafu dhidi ya serikali ya Tanzania hazitasaidia kulipatia ufumbuzi suala hili. Njia nzuri ni kwa njia ya majadiliano na Balozi Maajar aliwahakikishia ushirikiano wa dhati katika hili. Hata hivyo Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa hayuko tayari na hatavumilia kuona kampeni chafu dhidi ya Tanzania zinaendelea kutokana na suala hili. Aliwaeleza kuwa iwapo wataendelea na kampeni hizo chafu hatatoa ushirikiano wowote kwao na atalishughulikia suala hili kiserikali tu kwa kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Aliwaeleza kuwa hawana haki yoyote kuendelea na kampeni chafu dhidi ya Tanzania.

Balozi aliwaeleza kuwa iwapo wataendelea na kampeni hizi chafu dhidi ya serikali basi na yeye ataanza kampeni za kuisafisha Tanzania dhidi ya propaganda hizo ambazo si za haki.

· Kuhusu shinikizo kwa Dr. Mzengi, Balozi aliwahakikishia kuwa tayari kuna shinikizo kubwa na la kutosha la kumtaka Dr. Mzengi atoe kwa maandishi namna bora atakavyolipa fedha hizo.

· Kwa upande wa majibu ya "Demarche" toka serikali ya Tanzania, Balozi aliwashauri wanasheria hao kufuatilia majibu hayo katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwani kwa mujibu wa taratibu za kiserikali Balozi hawezi kuwasiliana na wanasheria hao katika mambo rasmi kati ya serikali na serikali.

· Kuhusu uwezekano wa Dr. Mzengi kuacha kulipa baada ya kuwa ameanza kulipa, Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa serikali italifanyia kazi kwa umakini suala hilo ili kuhakikisha kuwa suala kama hilo halijitokezi katika siku za usoni endapo Dr. Mzengi atakuwa amekubali kuanza kumlipa Zipora.

· Kuhusu ni lini suala hili litamalizika, Balozi hakutoa ahadi yoyote ila aliwaeleza wanasheria hao kuwa serikali inahitaji muda wa kutosha wa kulifanyia kazi suala hilo hivyo haiwezi kuliwekewa muda maalumu.

· Kwa upande wa suala la pasi ya kusafiria ya Zipora Mazengo, Balozi aliwaahidi wanasheria hao kuwa atalifanyia kazi na kuagiza afisa uhamiaji wa hapa ubalozini kufuatilia huko uhamiaji makao makuu kuona mchakato huu umefikia wapi na kama itakuwa tayari Mkuu wa Utawala Lily Munanka aliyepo Tanzania hivi sasa aje nayo.

· Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa Serikali ya Tanzania na yeye binafsi wana nia ya dhati ya kuona Zipora anapata haki yake anayosthili. Aliwahakikishia kuwa ubalozi uko wazi kwa Zipora kuja wakati wowote anapotaka kufanya hivyo na hakuna mtu atakayemdhuru na pia ajisikie huru kwenda nchini Tanzania wakati wowote atakapotaka kufanya hivyo.

· Balozi alihitimisha maelezo yake kwa kusisitiza tena kuwa utekelezaji wa suala hili ungekuwa rahisi sana kama wanasheria hao wangefuata utaratibu wa kisheria wa kutekeleza hukumu yao nchini Tanzania badala ya kuendelea na kampeni zao kuichafua Tanzania.

Nawasilisha
C/PUB
03Novemba, 2010
 
sijui nijilime risasi au nimlime mtu risasi!!!!!!..........

Huna sababu ya kujilima risasi ila kuna haja ya kutazama upya watu ambao tunawapa majukumu sensitive ya Nchi wako kwa ajili ya nchi ama ni kwa ajili ya masilahi yao binafsi?
 
Sasa hizi minutes mbona hazipo kwenye PDF file ama ndivyop balozi zetu wanafanya? si ni rahisi kwa mtu kubadilisha na hata kuweka ya kwake ?
 
· Wanataka kupata majibu ya “Demarche” iliyopelekwa serikali ya Tanzania.
· Walisisitiza kuwa hawataacha kufuatilia suala hili hadi ufumbuzi wake upatikane. Kwamba wataendelea kuwasiliana na Bunge la Marekani na Wizara ya Mambo ya Nje hadi hapo suluhu itakapopatikana.
· Walitaka kujua hatua za kuchukuliwa iwapo Dr. Mzengi atakubali kuanza kulipa na baadaye kuacha kulipa.
· Walitaka kujua mchakato wa maombi ya pasi ya kusafiria ya Zipora Mazengo yaliyowasilishwa ubalozini umefikia wapi.
· Walisema kuwa wizara ya usalama wa Ndani ya Marekani imemtambua na kumthibitisha Zipora Mazengo kama muathirika wa biashara haramu ya usafirishaji watu na imempa visa ambayo inamuwezesha kuishi na kufanya kazi Marekani katika uhai wake wote.
Akijibu hoja hizo, Balozi Maajar alisisitiza yafuatayo:
· Kampeni chafu dhidi ya serikali ya Tanzania hazitasaidia kulipatia ufumbuzi suala hili. Njia nzuri ni kwa njia ya majadiliano na Balozi Maajar aliwahakikishia ushirikiano wa dhati katika hili. Hata hivyo Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa hayuko tayari na hatavumilia kuona kampeni chafu dhidi ya Tanzania zinaendelea kutokana na suala hili. Aliwaeleza kuwa iwapo wataendelea na kampeni hizo chafu hatatoa ushirikiano wowote kwao na atalishughulikia suala hili kiserikali tu kwa kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Aliwaeleza kuwa hawana haki yoyote kuendelea na kampeni chafu dhidi ya Tanzania.

Balozi aliwaeleza kuwa iwapo wataendelea na kampeni hizi chafu dhidi ya serikali basi na yeye ataanza kampeni za kuisafisha Tanzania dhidi ya propaganda hizo ambazo si za haki.

· Kuhusu shinikizo kwa Dr. Mzengi, Balozi aliwahakikishia kuwa tayari kuna shinikizo kubwa na la kutosha la kumtaka Dr. Mzengi atoe kwa maandishi namna bora atakavyolipa fedha hizo.

· Kwa upande wa majibu ya “Demarche” toka serikali ya Tanzania, Balozi aliwashauri wanasheria hao kufuatilia majibu hayo katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwani kwa mujibu wa taratibu za kiserikali Balozi hawezi kuwasiliana na wanasheria hao katika mambo rasmi kati ya serikali na serikali.

· Kuhusu uwezekano wa Dr. Mzengi kuacha kulipa baada ya kuwa ameanza kulipa, Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa serikali italifanyia kazi kwa umakini suala hilo ili kuhakikisha kuwa suala kama hilo halijitokezi katika siku za usoni endapo Dr. Mzengi atakuwa amekubali kuanza kumlipa Zipora.

· Kuhusu ni lini suala hili litamalizika, Balozi hakutoa ahadi yoyote ila aliwaeleza wanasheria hao kuwa serikali inahitaji muda wa kutosha wa kulifanyia kazi suala hilo hivyo haiwezi kuliwekewa muda maalumu.

· Kwa upande wa suala la pasi ya kusafiria ya Zipora Mazengo, Balozi aliwaahidi wanasheria hao kuwa atalifanyia kazi na kuagiza afisa uhamiaji wa hapa ubalozini kufuatilia huko uhamiaji makao makuu kuona mchakato huu umefikia wapi na kama itakuwa tayari Mkuu wa Utawala Lily Munanka aliyepo Tanzania hivi sasa aje nayo.

· Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa Serikali ya Tanzania na yeye binafsi wana nia ya dhati ya kuona Zipora anapata haki yake anayosthili. Aliwahakikishia kuwa ubalozi uko wazi kwa Zipora kuja wakati wowote anapotaka kufanya hivyo na hakuna mtu atakayemdhuru na pia ajisikie huru kwenda nchini Tanzania wakati wowote atakapotaka kufanya hivyo.

· Balozi alihitimisha maelezo yake kwa kusisitiza tena kuwa utekelezaji wa suala hili ungekuwa rahisi sana kama wanasheria hao wangefuata utaratibu wa kisheria wa kutekeleza hukumu yao nchini Tanzania badala ya kuendelea na kampeni zao kuichafua Tanzania.

Nawasilisha
C/PUB
03Novemba, 2010

Kwa minutes hizi, kwanza inabidi wanajamii forum tumpongeze Mh Balozi. Kwani maelezo yake kwa hau mawakili hao wezi wa bi Zapora, ni safi na yako very straight. Sioni ni kwa vipi huyu Balozi alaumiwe. Hebu wote someni vyema huo mhutasari. Mtakubaliana na mimi kuwa Balozi kaonesha msimamo.
Kwa ufupi hawa jamaa mawakili wanataka tu kuichafua nchi kwa upuuzi tu. Kwanini wanakataa kuja Tz kukazia hukumu ya kesi? Eti hawaziamini mahakama zetu. Sisi tutaziamini vipi mahakama za Marekani? Kama kweli wanaushahidi na kesi yao na wanaiamini hukumu hiyo ni ya haki wanaogopa nini kuileta mahakama yaa Tz ikaziwe na hapo Allan atabanwa alipe. Na gharama zote za kesi si kawaida analipa mshitakiwa? sasa taabu yao nini kama si ujambazi wao tu.

Nina wasiwasi huyu bint katumiwa na wajanja wakimwemo hao mawakili, moja kujipatia fedha na pili kujipatia visa ya kuishi Marekani. Sasa tunaambia visa ya Marekani kashaipata. Mission is completed.
 
KUMBUKUMBU ZA MKUTANO KATI YA MHE. BALOZI MWANAIDI SINARE MAAJAR NA WANASHERIA WA ZIPORA MAZENGO KUZUNGUMZIA HUKUM YA MAHAKAMA YA UNITED STATES DISTRICT COURT FOR THE DISTRICT OF COLUMBIA KWA MADAI YA USAFIRISHAJI HARAMU WATU DHIDI YA DR. ALLAN MZENGI

Jumla
Tarehe 1 Novemba, 2010 kulifanyika mkutano kati ya Balozi Mwanaidi Maajar na wanasheria watatu wanaomwakilisha Zipora Mazengo kutoka kampuni ya Mawakili ya hapa Washington ijulikanayo kama Jenner & Block. Madhumuni ya mkutano ilikuwa kuzungumzia hukumu inayomkabili Dr Allan Mzengi kwa madai ya usafirishaji haramu mfanyakazi wake wa ndani Bi Zipora Mazengo na kumtumikisha bila malipo kinyume na sharia za hapa Marekani. Wanasheria waliohudhuria katika mkutano huo ni Martina E. Vandenberg na Lorelie S. Masters ambao ni mapatna katika kampuni hiyo ya mawakili na Daniel I. Weiner ambaye ni wakili wa ngazi ya kawaida. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Hukumu hiyo ilitokana na madai ya Bi Zipora kuwa aliletwa Marekani na Dr. Mzengi na mkewe kwa ahadi ya kufanya kazi kwa malipo halali lakini kinyume chake hawakumlipa mshahara wowote wakati wakimfanisha kazi kama mtumwa kwa massa 15 kila siku na bila kumruhusu kurejea Tanzania kwa miaka mine hata pale alipofiwa na ndugu yake. Alidai pia walizuia pasi yake na pia walimfanyisha kazi ya kupika chakula cha baishara ya kupika aliyokuwa akiifanya mke wake Dr. Mzengi. Alidai pia hata alipoumwa hawakumpeleka hospitali hadi alipozidiwa sana na wakati mwingine alikuwa anapigwa.
Dr. Mzengi hakutetea kesi hiyo kwa kuwa alidai haki ya kinga yake ya kibalozi. Hata hivyo kwa msingi wa Vienna Convention, kufuatana na madai kuwa alikuwa akifanya biashara nyumbani kwake madai ya kinga huenda yasingesimama mahakamani hapa Marekani. Hata hivyo ingekuwa kazi ngumu sana kwa Dr. Mzengi kukanusha madai ya kufanya biasahara kwa kuwa aliyemsaidia Zipora kutoroka alikuwa ni mteja wa mkewe Dr. Mzengi katika biashara hiyo ya chakula. Kwa maana hiyo kinga ya kibalozi ya Dr. Mzengi ilikuwa mashakani.
Katika hukumu ya mahakama Dr. Mzengi na mkewe wameamriwa kumlipa Zipora kiasi cha Dola za Kimarekani milioni moja na laki elfu hamsini na tisa, mia tatu arobaini na nane na point sabini na tisa ($1,050,348.79).
Majadiliano
Wanasheria wa Zipora walikuja kutaka kujua msimamo wa serikali ya Tanzania kuhusu fidia kwa Zipora Mazengo kutokana na hukumu ya kesi ya usafirishaji haramu watu dhidi ya Dr Allan Mzengi.
Balozi maajar aliwaeleza kuwa serikali ya Tanzania inaheshimu sheria za Marekani na pia inaheshimi hukumu itokanayo na mahakama za Marekani ingawa kwa mujibu wa sheria za Tanzania ni lazima hukumu hiyo ipelekwe Tanzania ikubaliwe na mahakama za Tanzania ili iweze kuwa ni hukumu inayotambulika kisheria. Alisema pia kuwa Tanzania ina dhamira ya dhati ya kupambana na biahara ya usafirishaji haramu wa watu duniani ndiyo maana Bunge la Tanzania limepitisha sheria The Anti-Trafficking in persons Act, (Act No-15 of 2008) ambayo imeanza kutumika mwaka jana 2009. Balozi Maajar alieleza nchini Tanzania kuna mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na vita dhidi ya biashara hii haramu na kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya biashara hii na kwamba serikali inaunga mkono shughuli zinazofanywa na mashirika hayo na pia imeanza kuimarisha vyombo vya dola vya utekelzaji wa sheria dhidi ya biashara haramu ya watu.
Akizungumzia kuhusu hukumu ya kesi dhidi ya Dr. Mzengi, Balozi Maajar aliwaeleza wanasheria hao kuwa hukumu hiyo si dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni dhidi ya Dr. Mzengi ambaye ni mwajiriwa wa Serikali. Aliwaeleza kuwa hukumu hii inatakiwa kuthibitishwa na mahakama za Tanzania kwa kufuata taratibu za kisheria zilizopo. Bila kufanya hivyo ni vigumu kwa serikali ya Tanzania kusimamia utekelezaji wa hukumu hiyo. Kwamba kama hukumu hiyo itakaziwa na mahakama za Tanzania, serikali inaweza kuitekeleza ikiwemo kukata mshahara wa Dr Mzengi pamoja na stahili zake nyingine ili kumlipa Zipora.
Kuhusu serikali kulipa kwa niaba ya Dr Mzengi, Balozi Maajar aliwaeleza wanasheria hao kuwa serikali haiwezi kulipa kiasi cha fedha kinachodaiwa kulingana na hukumu hiyo kwa vile ni kinyume cha taratibu za fedha za nchi. Kufanya hivyo kutapelekea kuwepo hoja za wakaguzi wa hesabu za serikali kutoka kwa mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali na pia hoja za kamati ya bunge inayosimamia hesabu za serikali ambayo mwenyekiti wake huwa ni mbunge toka chama cha upinzani.
Sheria za Tanzania
Wanasheria hao waliomba serikali ya Tanzania ibadilishe sheria zake ili kuwezesha hukumu zinazotolewa na mahakama za nchini Marekani kutekelezwa nchini Tanzania. Kwamba wamefanya utafiti na kugundua kuwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania, hukumu zinazotolewa na mahakama za Marekani haziwezi kutekelezwa nchini Tanzania.
Waliendelea kueleza kuwa hawako tayari kwenda Tanzania au kuajiri wanasheria ili kuwezesha hukumu iliyopo kutekelezwa nchini Tanzania kupitia utaratibu wa sheria za Tanzania. Walisema kuwa gharama za kufanya hivyo ni kubwa sana na hawako tayari kuingia katika gharama nyingine kwani hadi hivi sasa wametumia zaidi ya dola za Marekani Laki tatu ($330,000) kwa ajili ya kugharamia kesi hii. Walisema pia kuwa hawana imani na mahakama za Tanzania kwa vile zimejaa rushwa.
Wanasheria hao waliomba Serikali ya Tanzania kumuadhibu Dr. Mzengi kwa kumfukuza kazi na wanataka serikali itunge sheria ili kuweza kumshitaki Dr. Mzengi. Walidai kuwa Dr. Mzengi badala ya kuadhibiwa alipandishwa cheo na kupangiwa kazi katika ofisi ya Rais (Ikulu).
Akijibu hoja hizo, Balozi Maajar aliwaeleza kuwa serikali ya Tanzania na Ubalozi kwa ujumla wanaheshimu hukumu ya mahakama iliyopo dhidi ya Dr Mzengi. Hata hivyo ili hukumu hiyo iweze kutekelezwa Tanzania na ili Serikali iweze kusaidia utekelezaji wake, ni lazima utaratibu wa kisheria uliopo kuhusu hukumu za nje ufuatwe kikamilifu. Aliwaeleza kuwa hata kama sheria ingetungwa isingehusu makosa yaliyofanyika kabla ya sheria hiyo kutungwa.
Balozi Maajar aliwaambia wanasheria hao kuwa njia wanayotumia ya kutoa mashinikizo na propaganda za kuichafua Tanzania kupitia Bunge la Marekani, Serikali ya Marekani (Wizara ya Mambo ya Nje), Vyombo vya habari na taasisi nyingine zinazojihusisha na masuala ya haki za binadamu haiwasaidii katika kupata malipo ya fedha wanayodai. Balozi aliendelea kusisitiza kuwa serkali ya Tanzania haiwezi kulipa chochote kutokana na hukumu ambayo si dhidi yake licha ya mashinikizo yanayotolewa na wanasheria hao.
Balozi alisisitiza kuwa njia nzuri ya kuwawezesha kupata haki yao ni kufuata utaratibu wa kisheria wa kuikaza hukumu hiyo nchini Tanzania. Balozi aliwaambia wanasheria hao kuwa yuko tayari kuwasaidia katika kuwapatia majina ya makampuni na wanasheria nchini Tanzania ambao wanaweza kuwasaidia katika suala hili.
Kuhusu kumuadhibu Mzengi, Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa Mzengi aliadhibiwa kulingana na taratibu za utumishi wa umma nchini. Kwamba serikali haiwezi kufungua kesi dhidi ya Dr. Mzengi kutokana na hukumu iliyotolewa nchini Marekani na ambayo haijapata uhalali wa kutekelezwa nchini. Aliwaeleza kuwa hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kufanya jambo hilo ikiwamo serikali ya Marekani.
Akijibu ombi lao la kutaka Dr Mzengi afukuzwe kazi, Balozi aliwaeleza kuwa serikali haiwezi kumfukuza kazi bila sababu za msingi na bila kufuata taratibu na sheria za nchi, kwani kwa kufanya hivyo serikali itashitakiwa mahakamani na itashindwa. Aliwaeleza pia kuwa iwapo Dr. Mzengi atafukuzwa kazi hatakuwa na uwezo tena wa kulipa pesa hizo wanazotaka alipe hivyo Zipora hatapata chochote kutokana na hatua hiyo.
Kuhusu kupandishwa cheo, Balozi alikanusha kuwa Dr. Mzengi hajapandishwa cheo na kwamba kwa anavyojua yeye Mzengi hafanyi kazi katika ofisi binafsi ya Rais kama wanasheria hao wanavyodai.
Malipo
Kufuatia kauli ya msisitizo kutoka kwa Balozi kuwa serikali ya Tanzania haiwezi kulipa fedha inayodaiwa kama zilivyofanya serikli za Oman na Saudi Arabia kutokana na taratibu za fedha kutoruhusu, na shaka kama fedha hizo zote ni za Zipora na siyo kwamba kiasi kikubwa ni cha mawakili hao walisema kuwa wao wanafanya kazi hii kama msaada tu (pro bono) na si kwa masilahi yao binafsi na kwamba hawategemei fedha yoyote kutokana na hukumu hiyo. Walieleza kuwa hata wao wanajua wazi kuwa Dr. Mzengi hawezi kulipa kiasi cha fedha cha zaidi ya Dola za Kimarekani Million moja zinazodaiwa. Aidha walisema kuwa hata Zipora hatarajii kupata kiasi hicho cha fedha na kwamba kiwango cha chini kabisa wanachotegemewa walipwe ni Dola za Kimarekani laki mbili elfu kumi na sita ($ 216,000), ikiwa ni laki moja sabini na saba elfu ($ 177,083.00) zikiwa mishahara inayodaiwa na Zipora ambayo anadai hakulipwa kwa miaka minne aliyofanya kazi na kiasi kilichobaki ni faini mbali mbali (compensatory damages).
Mengineyo
Wanasheria hao walihitimisha hoja zao kwa kueleza yafuatayo:
· Wanaomba Dr. Mzengi aendelee kuwekewa shinikizo ili atoe utaratibu wa jinsi atakavyolipa pesa hizo anazodaiwa hususan mishahara ambayo haikulipwa (back wages).
· Waliahidi kuacha kampeni chafu dhidi ya Tanzania kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo ili kutoa nafasi kwa serikali kulishughulikia suala hili. Walitaka kupata ahadi kutoka kwa Balozi ni lini suala hili litamalizika.
· Wanataka kupata majibu ya "Demarche" iliyopelekwa serikali ya Tanzania.
· Walisisitiza kuwa hawataacha kufuatilia suala hili hadi ufumbuzi wake upatikane. Kwamba wataendelea kuwasiliana na Bunge la Marekani na Wizara ya Mambo ya Nje hadi hapo suluhu itakapopatikana.
· Walitaka kujua hatua za kuchukuliwa iwapo Dr. Mzengi atakubali kuanza kulipa na baadaye kuacha kulipa.
· Walitaka kujua mchakato wa maombi ya pasi ya kusafiria ya Zipora Mazengo yaliyowasilishwa ubalozini umefikia wapi.
· Walisema kuwa wizara ya usalama wa Ndani ya Marekani imemtambua na kumthibitisha Zipora Mazengo kama muathirika wa biashara haramu ya usafirishaji watu na imempa visa ambayo inamuwezesha kuishi na kufanya kazi Marekani katika uhai wake wote.
Akijibu hoja hizo, Balozi Maajar alisisitiza yafuatayo:
· Kampeni chafu dhidi ya serikali ya Tanzania hazitasaidia kulipatia ufumbuzi suala hili. Njia nzuri ni kwa njia ya majadiliano na Balozi Maajar aliwahakikishia ushirikiano wa dhati katika hili. Hata hivyo Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa hayuko tayari na hatavumilia kuona kampeni chafu dhidi ya Tanzania zinaendelea kutokana na suala hili. Aliwaeleza kuwa iwapo wataendelea na kampeni hizo chafu hatatoa ushirikiano wowote kwao na atalishughulikia suala hili kiserikali tu kwa kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Aliwaeleza kuwa hawana haki yoyote kuendelea na kampeni chafu dhidi ya Tanzania.

Balozi aliwaeleza kuwa iwapo wataendelea na kampeni hizi chafu dhidi ya serikali basi na yeye ataanza kampeni za kuisafisha Tanzania dhidi ya propaganda hizo ambazo si za haki.

· Kuhusu shinikizo kwa Dr. Mzengi, Balozi aliwahakikishia kuwa tayari kuna shinikizo kubwa na la kutosha la kumtaka Dr. Mzengi atoe kwa maandishi namna bora atakavyolipa fedha hizo.

· Kwa upande wa majibu ya "Demarche" toka serikali ya Tanzania, Balozi aliwashauri wanasheria hao kufuatilia majibu hayo katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwani kwa mujibu wa taratibu za kiserikali Balozi hawezi kuwasiliana na wanasheria hao katika mambo rasmi kati ya serikali na serikali.

· Kuhusu uwezekano wa Dr. Mzengi kuacha kulipa baada ya kuwa ameanza kulipa, Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa serikali italifanyia kazi kwa umakini suala hilo ili kuhakikisha kuwa suala kama hilo halijitokezi katika siku za usoni endapo Dr. Mzengi atakuwa amekubali kuanza kumlipa Zipora.

· Kuhusu ni lini suala hili litamalizika, Balozi hakutoa ahadi yoyote ila aliwaeleza wanasheria hao kuwa serikali inahitaji muda wa kutosha wa kulifanyia kazi suala hilo hivyo haiwezi kuliwekewa muda maalumu.

· Kwa upande wa suala la pasi ya kusafiria ya Zipora Mazengo, Balozi aliwaahidi wanasheria hao kuwa atalifanyia kazi na kuagiza afisa uhamiaji wa hapa ubalozini kufuatilia huko uhamiaji makao makuu kuona mchakato huu umefikia wapi na kama itakuwa tayari Mkuu wa Utawala Lily Munanka aliyepo Tanzania hivi sasa aje nayo.

· Balozi aliwaeleza wanasheria hao kuwa Serikali ya Tanzania na yeye binafsi wana nia ya dhati ya kuona Zipora anapata haki yake anayosthili. Aliwahakikishia kuwa ubalozi uko wazi kwa Zipora kuja wakati wowote anapotaka kufanya hivyo na hakuna mtu atakayemdhuru na pia ajisikie huru kwenda nchini Tanzania wakati wowote atakapotaka kufanya hivyo.

· Balozi alihitimisha maelezo yake kwa kusisitiza tena kuwa utekelezaji wa suala hili ungekuwa rahisi sana kama wanasheria hao wangefuata utaratibu wa kisheria wa kutekeleza hukumu yao nchini Tanzania badala ya kuendelea na kampeni zao kuichafua Tanzania.

Nawasilisha
C/PUB
03Novemba, 2010

Now naelewa kwa nini Maajar alikuwa hataki tena hii kazi

inataka mtu uwe na moyo sana kuifanya
 
Back
Top Bottom