Modern-Day Slavery on D.C.'s Embassy Row? [Afisa Balozi wetu Mzengi na Utumwa mpya?]

Ni katika kufunika aibu ya Serikali yao ya kuweka madarakani viranja vilaza.wanajuana!
 
huyo mama ni moja wa mabalozi wanaotumia pesa yetu bila huruma, sijui huo ujasiri anautoa wapi?
hivi viti maalumu vitatumaliza.
sijui kikwete anawatoa wapi hawa watu wake, hapa london kaondoka wakati kuna kashifa matumizi mabovu ya pesa, huyu mama anaweza kuwa ka-fisadi!!!!
 
Hivi ni nani alikuwa anamtetea MZENGI kwenye hii kesi?
Usije ukakuta Ni zile Firm za kisheria za kina Majar au ni MKONO kwa KODI ZETU!
 
kweli hata Mungu akiona tunamsubiri atusaidie katika hili atatutia viboko. Mwe, tuchukue hatua
 
Wakimaliza kuvuana magamba wataanza kuchuna ngozi wabakie na vidonda tu maana mwendo huu si salama kwa serikali hata kidogo.
 
Wakimaliza kuvuana magamba wataanza kuchuna ngozi wabakie na vidonda tu maana mwendo huu si salama kwa serikali hata kidogo.
Duh! Hii nchi haitaki viraka tena ni kuibomoa yote na kuijenga upya maana kila tunapoziba pengine panafumuka! Hata mzee wetu Dr slaa atachoka kutusaidia kuwataja ili sisi wananchi tuchukue hatua maana punguani wanaweza kudhani kawa Mtikila!
 
hivi tumeanza kuzoea huu uozo jamani? Hata magazeti makini hayatoi tena habari hizi ukitoa mwanahalisi!
 
Huwa nawaambia kabla ya kutukana angalieni historia huyu Balozi ndie mdhamini Wa kwanza wakati CHADEMA inaanzishwa see the records....
 
Inisikitisha sijui kwanini vijana tusifanye maamuzi magumu naona ka twaongea sana toka hii forum hii ianze 2006 ni miaka 5, inabidi tutende na kuyafanyia kazi haraka tunayoyateta hapa kila siku, ebu tuamke au ndoo bado tupo utozi wa kujisifu kujua kutumia mafacebook, matwitter na jamii forum, tufanye maamuzi haraka
 
huwa nawaambia kabla ya kutukana angalieni historia huyu balozi ndie mdhamini wa kwanza wakati chadema inaanzishwa see the records....

acha upuuzi we kilaza...so huo udhamini unamuondolea vipi utanzania wake?????......mbona stephen wassira alikuwa mbunge wa upinzani na mjumbe wa kamati kuu nccr-mageuzi...leo hii ni mjumbe wa kamati kuu ccm,mbunge na waziri wa ofisi ya rais........fikiria kwa mapana ..mhukumu mtu kwa alichoandika na sio kuangalia vitu ambavyo havimuondolei utanzania wake........
mimi naona kuwa ushauri wa balozi ni wa kutafakari kwa makini...serikali ina uamuzi mmoja wa kumuacha huyo allan abaki marekani alipe mwenyewe au wamfunge...au kumlipia na kumkata mafao yake au kukamata mali zake ....lakini deni lazima lilipwe kwa manufaa ya taifa zima...ujinga wa allan hauwezi kuli cost taifa!
 
Kiranja.

Kwanza kabisa pongezi kwa hiyo habari nyeti. Ombi langu ni hili, itowe kwenye attachiment na uiweke hapo juu ili watu wote waione wasio na akaunti Jamii Forum. Nguvu ya UMMA lazima waione hii habari.
 
Sioni tatizo la Barua ya Ushauri kutoka kwa Balozi Maajar........ni barua nzuri tu..........it is very clear and simple........Jaribuni kujiweka katika position ya Balozi........ndio pengine mtaelewa............

Huyu mama anaweza kuwa na mabaya yake lakini sio kwa barua hii............
 
Huyu bwana baada ya haya yote ameitwa na kupewa cheo kikubwa sana ndani ya idara ya usalama wa taifa letu Tanzania .

Hebu soma hapa ni balozi analalamika kwa rais lakini rais huyo huyo anamwita na kumpa wadhifa mkubwa tena kwenye idara ya usalama wa Taifa.

Mkuu hapo kwenye bold hebu tusaidie wengine ambao hatujui ni nini kinaendelea kumhusu Dr Mzengi???
 
Ungekuwa huu ni uwanja wa matusi huyu Mwanaidi Sinare Maajar leo angekufa kwa matusi ambayo ningempa! Huu ni upumbavu wa hali ya juu uliopitiliza kipimo!! Yaani mtu afanye uhalifu halafu serikali imlipie? Hana adabu kabisa na fikira zake zinawaza usawa wa pua yake. Jamani hii misukule inawezaje kufika mpaka ngazi kuwa mabalozi wakati bongo zao zimegandishwa kwenye ufisadi?? Nadhani hii barua ni vizuri ipelekwe kwa hao hao congress ili waona jinsi Afrika kulivyo na watu majuha!
unajua nchi hasa ktk utawala wa huyu Mkwerez, kua kiongozi si swala la sifa za kutukuka bali inategemea mahusiano yako na Mteuaji/rais. . . Full stop.
 
Sioni tatizo la Barua ya Ushauri kutoka kwa Balozi Maajar........ni barua nzuri tu..........it is very clear and simple........Jaribuni kujiweka katika position ya Balozi........ndio pengine mtaelewa............

Huyu mama anaweza kuwa na mabaya yake lakini sio kwa barua hii............

Ebu fafanua kidogo Mkuu, Kuhusu usahihi wa hiyo barua ya Majaar.
 
Back
Top Bottom