Moderators wawe wabunifu wa kuyatengeneza majukwaa yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moderators wawe wabunifu wa kuyatengeneza majukwaa yao

Discussion in 'Sports' started by Candid Scope, Oct 7, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Moderators ningewashauri kuwa na ubunifu wa kuyatengeneza majukwaa kuwa na mvuto zaidi badala ya kusubiria tu mada za kutoka kwa wadau.

  Mfano, michezo ya super league ningetegemea moderator anatuandalia thread inayoonyesha matokeo ya kila timu na pengine hata kupanga msimamo wa ligi ya nyumbani, hili linaweza kutoa tashwira nzuri ya jukwaa la michezo na pia kuleta mvuto zaidi wa jukwaa hili badala ya kutegemea fulani mwenye bahati abandike kivyake hapa.

  Sijajua bado vigezo wanavyopata hawa moderators, maana moja wapo ingekuwa mwenye uwezo wa kubuni na kuendesha jukwaa fulani kwa ufanisi ndiye anayeweza kuratibu jukwaa fulani.

  Cha kushangaza utamwona moderator amejaa tele kule pembezoni kwa jukwaa la wakubwa kule ukingoni mwa meza sijajua ni lini anapokuwa na wasaa wakupitia mada hapa kwenye majukwaa ya kawaida.

  Naomba nisipopolewe kwa mawe, ni ushauri wangu tu.
   
Loading...