Mochwari ya Muhimbili wanamjaribu Rais Magufuli?

Njaro

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
356
787
Mochwari ya Muhimbili inazidi kunishangaza. Wakati kuna vituko vya kuchanganya maiti likijitokeza kwa zaidi ya mara mbili na Baadhi yao walichukuliwa hatua na wengine kubakizwa kuna hili lingine la kumjaribu Rais Magufuli linazidi kukua.

Miezi miwili iliyopita nilipata msiba wa kufiwa na shangazi yangu katika wodi ya Mwaisela ambapo Nesi aliyekuwa zamu alinifuata na kuniuliza hii ni maiti yako nikamwambia ndio akaniambia nakuunganisha na mtu wa Mochwari aitwaye Abdallah, akanipa na mawasiliano yake ya Simu ili niwasiliane nae aweze kunihifadhia marehemu wangu kwa bei chee na nilipowasiliana nae akanitajia gharama nikalipia lakini cha kushangaza sikupewa risiti licha ya kumwambia anipatie. Kama mimi nimefanyiwa hivi, Inavyoonyesha kuna pesa nyingi zinazoishia mikononi mwa wajanja janja wachache huku Serikali ikipoteza mapato yake.

Hilo lilipita, majuzi nikafiwa tena na mwanangu ambapo nilimpeleka mochwari ya Muhimbili nikakutana na mhudumu aliyekuwa mapokezi aitwaye Seleman (nilisikia akiitwa na staff mwenzie) ambapo alinitajia gharama za kuhifadhi mwili ambapo niliambiwa jumla ni Tsh. 165,000/- gharama za kulaza marehemu wangu kwa siku tatu, kumweka dawa asiharibike, kumwogesha na kumvalisha marehemu wangu. Lakini akaniambia nitoe Tsh. 150,000/- lakini hakuna risiti kwani alidai ananisaidia tu, nami kwa sababu msiba wa Mwanangu ulinichanganya sikutia neno

Ikumbukwe hili ni tukio limejitokeza mara mbili kwangu la kutoa pesa pasipo kupewa risiti. Inavyoelekea pale kuna mtandao hatari wa akina Abdallah, Seleman na wengineo wa kuficha malipo ya taasisi na pesa hiyo kuingia mifukoni mwao.

Muhimbili kupitia idara ya mochwari inapoteza mapato mengi yanayoishia mikononi mwa wajanja wachache. Hawa watu wanamjaribu Rais Magufuli kwa kutokukusanya mapato vizuri na kuna haja ya suala hili limulikwe na wahusika hawa wachukuliwe hatua stahiki.
 
Dah pole na misiba.

Ina maana kutunza maiti ni biashara pia aisee; napiga picha kwa wale wasio na uwezo inakuwaje sijapata kuona sector wafanyakazi waliokosa morals na compassion kama hii.

Worst katika maisha yetu asilimia kubwa tutatumia hizi huduma sijui kwanini wengine awaoni madhara ya unqualified ppl kupewa hizi sector; viongozi wa leo wanadhani awatakuja kumbana na hayo mambo katika maisha yao na awaoni sababu ya kuona mambo yanabadilika.
 
Mochwari ya Muhimbili inazidi kunishangaza. Wakati kuna vituko vya kuchanganya maiti likijitokeza kwa zaidi ya mara mbili na Baadhi yao walichukuliwa hatua na wengine kubakizwa kuna hili lingine la kumjaribu Rais Magufuli linazidi kukua.

Miezi miwili iliyopita nilipata msiba wa kufiwa na shangazi yangu katika wodi ya Mwaisela ambapo Nesi aliyekuwa zamu alinifuata na kuniuliza hii ni maiti yako nikamwambia ndio akaniambia nakuunganisha na mtu wa Mochwari aitwaye Abdallah, akanipa na mawasiliano yake ya Simu ili niwasiliane nae aweze kunihifadhia marehemu wangu kwa bei chee na nilipowasiliana nae akanitajia gharama nikalipia lakini cha kushangaza sikupewa risiti licha ya kumwambia anipatie. Kama mimi nimefanyiwa hivi, Inavyoonyesha kuna pesa nyingi zinazoishia mikononi mwa wajanja janja wachache huku Serikali ikipoteza mapato yake.

Hilo lilipita, majuzi nikafiwa tena na mwanangu ambapo nilimpeleka mochwari ya Muhimbili nikakutana na mhudumu aliyekuwa mapokezi aitwaye Seleman (nilisikia akiitwa na staff mwenzie) ambapo alinitajia gharama za kuhifadhi mwili ambapo niliambiwa jumla ni Tsh. 165,000/- gharama za kulaza marehemu wangu kwa siku tatu, kumweka dawa asiharibike, kumwogesha na kumvalisha marehemu wangu. Lakini akaniambia nitoe Tsh. 150,000/- lakini hakuna risiti kwani alidai ananisaidia tu, nami kwa sababu msiba wa Mwanangu ulinichanganya sikutia neno

Ikumbukwe hili ni tukio limejitokeza mara mbili kwangu la kutoa pesa pasipo kupewa risiti. Inavyoelekea pale kuna mtandao hatari wa akina Abdallah, Seleman na wengineo wa kuficha malipo ya taasisi na pesa hiyo kuingia mifukoni mwao.

Muhimbili kupitia idara ya mochwari inapoteza mapato mengi yanayoishia mikononi mwa wajanja wachache. Hawa watu wanamjaribu Rais Magufuli kwa kutokukusanya mapato vizuri na kuna haja ya suala hili limulikwe na wahusika hawa wachukuliwe hatua stahiki.

Pole na kufiwa, umempata marehemu wako, umemzika, unelipa kiasi sahihi, usimlaumu jamaa wa mochwari hao wote kuanzia Mhasibu, wauguzi wanajua, kwa hiyo hii sio breaking news. Dhamira ya kupambana na rushwa unatakiwa iwe strategically.

Kwani tragic wanatoa receipt? Ukidai sana eti iwashe gari urudi nyuma Kama 34km kituoni ndo upate receipt, hii kitu ya trafic kukosa receipt inaniumaga sana sana sana mpaka natamani kulia.
 
Mkuu Pole sana kwa kuondokewa na Wapendwa wako.
Mungu akutie wepesi
 
kwa nn umetoa rushwa? alafu unalalamika sijui selemeni mara abdallah kwa nn usingetoa taarifa kwa mkubwa wao wa department? then tangu huo tunaoukisia kuwa wizi utokee Leo ni siku ya ngapi? kwa nn hukusema tangu siku hizo? ok bado hujachelewa tafuta means yakuondoa huo uovu
 
Kwa
Mochwari ya Muhimbili inazidi kunishangaza. Wakati kuna vituko vya kuchanganya maiti likijitokeza kwa zaidi ya mara mbili na Baadhi yao walichukuliwa hatua na wengine kubakizwa kuna hili lingine la kumjaribu Rais Magufuli linazidi kukua.

Miezi miwili iliyopita nilipata msiba wa kufiwa na shangazi yangu katika wodi ya Mwaisela ambapo Nesi aliyekuwa zamu alinifuata na kuniuliza hii ni maiti yako nikamwambia ndio akaniambia nakuunganisha na mtu wa Mochwari aitwaye Abdallah, akanipa na mawasiliano yake ya Simu ili niwasiliane nae aweze kunihifadhia marehemu wangu kwa bei chee na nilipowasiliana nae akanitajia gharama nikalipia lakini cha kushangaza sikupewa risiti licha ya kumwambia anipatie. Kama mimi nimefanyiwa hivi, Inavyoonyesha kuna pesa nyingi zinazoishia mikononi mwa wajanja janja wachache huku Serikali ikipoteza mapato yake.

Hilo lilipita, majuzi nikafiwa tena na mwanangu ambapo nilimpeleka mochwari ya Muhimbili nikakutana na mhudumu aliyekuwa mapokezi aitwaye Seleman (nilisikia akiitwa na staff mwenzie) ambapo alinitajia gharama za kuhifadhi mwili ambapo niliambiwa jumla ni Tsh. 165,000/- gharama za kulaza marehemu wangu kwa siku tatu, kumweka dawa asiharibike, kumwogesha na kumvalisha marehemu wangu. Lakini akaniambia nitoe Tsh. 150,000/- lakini hakuna risiti kwani alidai ananisaidia tu, nami kwa sababu msiba wa Mwanangu ulinichanganya sikutia neno

Ikumbukwe hili ni tukio limejitokeza mara mbili kwangu la kutoa pesa pasipo kupewa risiti. Inavyoelekea pale kuna mtandao hatari wa akina Abdallah, Seleman na wengineo wa kuficha malipo ya taasisi na pesa hiyo kuingia mifukoni mwao.

Muhimbili kupitia idara ya mochwari inapoteza mapato mengi yanayoishia mikononi mwa wajanja wachache. Hawa watu wanamjaribu Rais Magufuli kwa kutokukusanya mapato vizuri na kuna haja ya suala hili limulikwe na wahusika hawa wachukuliwe hatua stahiki.

Kwa nini hukwenda kwa mkurugenzi wa hospitali ili ulipe na kupewa risiti? Wewe ndiye utaisaidia takukuru kuwakamata hao wahudumu.
 
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe..Amin.
Kwanza pole sana kwa misiba yote na sote tukumbuke ya kuwa sisi sote ni wasafiri.
Kulingana na Thready yako huenda ukawa una makosa au labda pia kutokana na Khali zilizokupata ndizo zilizo changia kukunyima haki ya kutaka kujua uhalali wa malipo ya kufadhi miili ya marehemu hao.

Anyway kwakuwa sekta hii kiukweli bila unafiki mara nyingi tunapopatwa na maswahiba haya kwa ndugu,jamaa na marafiki na kupeleka miili au mwili kwaajili kuhifadhi mara nyingi huwezi kuhoji sana uhalali wala kutokuwa na uhalali kutokana na Majonzi pamoja na uhuzuni ya kupoteza ndugu zetu.

My Take: Ninashauri awamu hii iachane na mfumo wa matamko mengi yasiyo na Tija kwa sisi wananchi, na hatimaye wafanye vitendo na tuvione.

Wizara ya afya yule Dada anayeitwa Ummy na Kigwangala hebu simameni vizuri katika sekta ya afya na wengineo WOTE mliopewa dhamana na kuacha na Ngonjera na Maagizo yasiyo na Tija, kwa mfano hapa majuzi Serikali ilitoa Tamko la Wagonjwa kupatiwa Vyakula Muhimbili na hivyo hakuna haja ya kumpekelekea mgonjwa wako chakula tena hospitalini.

Hakika niliposikia na kusoma Taarifa hizo nilishtushwa sana kwani ninafahamu Taifa langu na aina ya Viongozi tulio nao, nilijua fika kuwa tutapoteza ndugu zetu kwa kukosa chakula na siyo tena magonjwa.Mungu si Athumani baada ya Tamko hilo akaingilia kati na kubadilisha mawazo ya watoa Matamko baada nadhani ya Malaika kuwashukia wengine na kuwajulisha watoa matamko kusitisha mfumo huo haraka.

Nilifurahi sana kusikia hivyo...huu ni mfano mmoja tu kuna mengi sana sana.
Hivyo hebu Serikali mtusaidie na muwe na hruma na sisi wananchi wenu na mjue ya kuwa kila mtu atatoa hesabu yake,tuokoeni na ya yale maswahiba ya Tanzania yaani Ujinga,Umasikini,Maradhi,Ufisadi,Rushwa, n.k. huku mkinyenga mahusiano mazuri na sisi mnao tuongoza ili tushirikiane kwa pamoja na kuachana na Unafiki uliokithiri ktk nchi yetu.
 
Daa polee sana mkuu yan hii shida ikikuta unaweza toa hela hata usijue ya nn??
 
Yan nikikumbuka kifo ama nitakufa naishiwa na ham hata ya kula. Lawama zote ziwaendee wazaz wet wa kwanza Adam na eva. Yan eva angekomaa kutokula lile tunda sasa hiv tungekuwa tunakula bata Edeni bila bugza.walikosea sana
 
Pesa ilipwe kwa mhasibu na hapo mochwari nenda na risiti halali kwa malipo sahihi. Naamini msiba ulichangia kutofanya uamuzi sahihi. Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom