Mo kabla ya kutoa bil 20 kajifunze kidogo Kwa GSM

Pesanyingi

JF-Expert Member
Apr 15, 2023
400
665
Uwongozi wa Club ya Simba ni wakati sahihi sasa kujifunza jinsi ya kuendesha Club kisasa na siyo kisiasa.
Tukianzia Kwa upande wa watani zetu Yanga,tangu GSM apewe timu Club ya Yanga imebadilika sana kiuwendeshaji.

Wamejitahidi sana katika kufanya sajili bora kitaalamu na siyo kuokota okota wachezaji.
Timu inacheza kwa spirit ya hali ya juu sana ndani ya dk 90.

Hakuna mwanya wa makundi ndani ya Yanga, kama ilivyokuwa hapo awali. Tofauti na Club yangu pendwa Simba,Siasa ndiyo zinaongoza club hii.Tukumbuke pia katika kubadilisha mfumo wa kiuwendeshaji Simba ndiyo tulianza ila hadi Sasa tumekwama.

Tangu msimu huu uanze timu imekuwa ikishida ki miujiza ujiza. Wachezaji wamekuwa wazito na hawajitumi huku wakijiona ni super star,kasoro Kibu Denis ndiyo amekuwa na moyo wa upambanaji.

Kwa upande wa kocha msimu huu hatuna kocha,mme dharau uwezo wa mgunda mkiamini ngozi nyeupe.
Wanachama na wapenzi tulichanga pesa za ujenzi wa uwanja ila hakuna lolote linaloendelea haya ni machache tu kuonyesha ndani ya Club mambo si shwari.

Kwako rais wa heshima Mo,kajifunze Kwa GSM kama unania ya kweli na Simba na Sina lengo la kuulizia bil 20 zako kwanza najuwa "unapata hasara" kuihudumia club hapa nimekunukuu kama ulivyowahi kusema siku za nyuma.
 
Hii wiki Mo ajiandae kukumbushiwa zile Bil. 20 kila dakika! Kazi anayo.
Kumbe ndio maana huwa ana pressure sana wakati wa mechi masikini, anayajua yatokanayo.
 
Back
Top Bottom