Mo kabla ya kutoa bil 20 kajifunze kidogo Kwa GSM

Pesanyingi

JF-Expert Member
Apr 15, 2023
400
665
Uwongozi wa Club ya Simba ni wakati sahihi sasa kujifunza jinsi ya kuendesha Club kisasa na siyo kisiasa.
Tukianzia Kwa upande wa watani zetu Yanga,tangu GSM apewe timu Club ya Yanga imebadilika sana kiuwendeshaji.
Wamejitahidi sana katika kufanya sajili bora kitaalamu na siyo kuokota okota wachezaji.
Timu inacheza kwa spirit ya hali ya juu sana ndani ya dk 90.
Hakuna mwanya wa makundi ndani ya Yanga,kama ilivyokuwa hapo awali.
Tofauti na Club yangu pendwa Simba,Siasa ndiyo zinaongoza club hii.Tukumbuke pia katika kubadilisha mfumo wa kiuwendeshaji Simba ndiyo tulianza ila hadi Sasa tumekwama.
Tangu msimu huu uanze timu imekuwa ikishida ki miujiza ujiza.
Wachezaji wamekuwa wazito na hawajitumi huku wakijiona ni super star,kasoro Kibu Denis ndiyo amekuwa na moyo wa upambanaji.
Kwa upande wa kocha msimu huu hatuna kocha,mme dharau uwezo wa mgunda mkiamini ngozi nyeupe.
Wanachama na wapenzi tulichanga pesa za ujenzi wa uwanja ila hakuna lolote linaloendelea haya ni machache tu kuonyesha ndani ya Club mambo shwari.
Kwako raise wa heshima Mo,kajifunze Kwa GSM kama unania ya kweli na Simba na Sina lengo la kuulizia bil 20 zako kwanza najuwa "unapata hasara" kuihudumia club hapa nimekunukuu kama ulivyowahi kusema siku za nyuma.
 
Moo Asisahau kujifunza pia namna Bora ya kushangilia ushindi wa derby kama Yanga Pira GAMONDI mtu mbad! Mzee wa nyuklia, anaua mbu (Simba) kwa bunduki!

Leo nilimuona Kibu Denis mkandaji akilia kwa uchungu kwenye benchi lao Leo ufalme wake umefutwa RASMI na Max Nzengeli Iniesta mpya NBC premier league!!
 

Attachments

  • VID-20231105-WA0025.mp4
    3.4 MB
Brother toa neno.
Unahisi tufanye nini kwa sasa????
Binafsi nashauri.
Simba lazima tufanye marekebisho makubwa yafuatayo:
1. Tuuze wachezaji wazembe na wazee km Onana etc
2. Robertinho atoke
3. Yanga watueleze wanatoa wapi makocha.
Wewe toa ushauri please
 
Bila uwongozi kubadilishwa wakapata Viongozi wa mpira kama Eng Heris wa Yanga. Simba bado itakuwa ni timu inayoendeshwa ki uswahili Swahili tu.Chakufanyika Mo anatakiwa aondoke na safu yake
Huyo mwenyekiti wake sijuwi hata kama ana taaluma ya mpira kila nikiangalia anayoyafanya.MFANO (kumleta Manzoki wakati wa uchaguzi alafu wanajuwa hawawezi msajili) hilo TU lilitosha mwenyekiti kuachia ngazi kama Simba wangekuwa smart na serious.
Wapo wawekezaji wenye nia ya dhati ya kuifanya Simba kupiga hatua zaidi ya hapo.
Kuliko kundi la kina tyrgane na wenzake kila siku kuwahadaa mashabaki kwamba oooo Simba tunaenda kucheza nusu fainal wakati wanasajiki wachezaji wa bei ya chini au waliochoka na kutumika na timu zingine. .
 
Back
Top Bottom