Chuma Chakavu
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 1,523
- 655
Taifa hili tunakoelekea ni kubaya. Tabia ya baadhi ya watanzania kufanya siasa za udini, kumchafua rais yeyote anayekuwa muislam si sawa. Ni kweli kuwa watanzania tumekuwa mashabiki wa kumponda rais Kikwete, si kwasbbu yoyote bali ni kutokana na uislam wake. Mbona Nyerere aliua watu wengi na hammsemi. Aliwapiga exile watz kibao hamsemi eti mmeamua pia kumpa utakatifu, haya bwana. Lakini wajanja tunajua ubaya wa J.K mnaousemea ni upi. J.K si mbaya hivyo isipokuwa ni jitihada za baadhi yetu za kumhakikishia nchi haitawaliki.
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa kikwete alichaguliwa kwa kura za waislam tu!!
unajua ni rais gani wa Tanzania ambaye mpaka sasa ndio anaongoza kwa kusaini hati za kifo na hatimaye kunyongwa watu wengi.
Ni kiashiria kipi kinachotofautisha pale kiongozi anapopingwa kisiasa na pale anapopingwa kwa sababu ya dini yake!?
Mbona hatujasikia rais akilalamika kuwa utendaji wake unakosolewa kwa sababu ya dini yake? au nyie ni mashabiki wake ambao hamna uwezo wa kisiasa wa kujenga hoja kutetea utendaji wake ila mnakimbilia majibu mepesi yasiyo na mashiko ambayo yanaweka wazi ujinga wenu kuwa njia bora ya kumtetea rais kikwete ni kwa kuweka dhana ya udini!
Ina maana ulikuwa unaishi ulimwengu gani wakati mkapa anaongoza Tanzania na pia baada ya kutoka madarakani jinsi alivyokosolewa, kubezwa na kutukanwa lakini si wapambe wake wala yeye aliyejitetea kwa dhana ya udini!
UJINGA WA MJINGA NI ZAO LA ITIKADI ZA KIJINGA ZILIZOTENGENEZWA NA MJINGA KWA AJILI YA WAJINGA ZAIDI YAKE ILI WAJINGA HAO WAZIDI KUWA WAJINGA KULIKO MUASISI WA UJINGA HUO.