Mo Ibrahim: CCM awamu ya nne yavunja record utawala bora

Kwenye kuendeleza Barbara na miundo mbinu I agree. Tatizo Hilo la utawala bora halipo. Ni udini na makundi mwanzo mwisho.
sasa unawezaje kumsifia mtu ambae anashindwa kuudhibiti udini,huoni udini ukikolea hata hizo barabara zitapasuka kwa mabomu,jk ni dhaifu hata mkimpa udaktari wa kuhonga.
 
Tatizo sio utawala wa JK kuwa mzuri ni kwamba Africa wazuri wote hawapo so huyu ana afadhali eti? Sasa hizi nchi nyingine si ni balaa.. But look at sudan, ethiopia, drc, bhagbo, beghazi, tunisia, fall of egypt and qadfi etc.. Hawa ndio watu #- anaoshindana nao
Hapo sasa nimeelewa
 
Who is Mo Ibrahim? Sasa yeye na Foundation yake wakisema hivyo kwani ndio kweli? Ni kweli Tanzania inastahiri hizo sifa? Mo Ibrahim ni mchumia tumbo yupo kimaslahi zaidi taasisi yake haina tofauti na REDET.....
 
sorry mkalimotto

1. hivi daraja lakusini aka daraja la Mkapa limeanza kutumika lini vile tukumbushe ?
2.hivi daraja la kigamboni nalo limeanza kutumika tangu lini vile ?
3.hivi mgao wa umeme umekuwa historia tangu lini vile ?
4.hivi tangu kj ameingia madarakani umaskini umeongezeka au umepungua.? kwa % ngapi ?
5.hivi alivyoingia madarakani deni la Taifa lilikua sh ngapi ? je na sasa limeongezeka au limepungua ?

Sorry bro hebu jaribu kujibu hayo nione Iq yako ili nifikirie kama kunaulazima wa kukuuliza maswali ya Advance coz haya ni ya std II
 
Ni kweli kikwete ni kiongozi ambaye tz haijawahi kupata kama yeye.Alitakiwa aongoze zaidi ya miaka 10,angeiacha nchi mbali sana.Kuna watu wanamchukia kwa sababu zao za kiimani na si kingine kwa sababu hatuoni hoja zaidi ya matusi,hasira na chuki.

Wamejaribu kumchokoza lakini hachokozeki,wamechochea vurugu lakini wameshindwa na nia yao ili kutia dosari uongozi wake.Sasa ripoti mbalimbali zinazotolewa na taasisi za kimataifa juu ya mafanikio ya uongozi wake zimekuwa zikiwakera na kuwaumbua,wanachotaka ionekane nchi imemshinda jambo ambalo si kweli.

Kwa haya yanayotokea kwa mafanikio ya uongozi wake,na hila mbalimbali zinazofanywa kutia dosari mafanikio yake,naungana na wale waliosema Jakaya Kikwete ni CHAGUO LA MUNGU.
Hivi kwa nini kikwete akikutana na upinzani watu wanakimbilia kwenye dini? Hivi mbona wamarekani wanampa wakati mgumu obama na hali amefanya mengi mazuri likiwemo la matishio ya ugaidi ambayo yaliwasumbua sana lakini hawazungumzii dini wala rangi yake? Hivi hapa tanzania wanaoipinga ccm ni wakristo na wapagani peke yao? Hivi ni dini gani inayoisumbua serikali kwa maandamano na vurugu kila kukicha? Hivi haya ya akina ponda
Yangekuwa yanafanywa na watu wa makanisani ingekuwaje? Hivi akina lipumba na cuf wote wamekuwa wakristo? Au baada ya kikwete kulipaswa kusiwe na upinzani, kama nyerere, mwinyi na mkapa walikumbana na upinzani kwanini yeye na hasa sasa ambapo uelewa umeongezeka asipingwe? Mwaka 2015 kikwete alikuwa dini gani? UBONGO WAKO UNAHITAJI MATIBABU
 
Hii ni kwa sababu anawafuata huko nje kuwaongopea pasipo na wa kukanusha. Hii ni kwa sababu asilimia kubwa ya muda wake ni utalii wa nje.
 
Kwa uwelewa wangu mdogo ni kuwa daraja la kusini liwe la Umoja ama daraja la Mkapa limejengwa enzi za Mkapa . Barabara unazosema zilianzwa kujengwa enzi za Mkapa na fedha zilishatengwa .Cha kustaajabisha kasi ilianza kupungu alipoingia baba Riz kwa kuzipeleka ndiko siko -kuzurura dunia nzima .

Hizo tuzo za Mo Ibrahim ni usanii mtupu ,zinawafaa kina Diamond na Wema

Mwakalunga acha u miopic. Mkapa ameacha km 11,000 na J.K amejenga zake 18,000. Soma ripoti ya Magufuli inayotaja barabara na km zake.
 
Taarifa ya utawala bora iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Ibrahim Mo imemtaja Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuvunja record ya utawala bora kwa kuiingiza Tanzania kwa mara ya kwanza katika nafasi ya 10 bora kati ya nchi zaidi ya 50 za Africa.

Kati ya nchi hizo, ni Tanzania pekee kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati.

My take:
Watanzania tuzitambue na kuthamini juhudi anazozifanya rais wetu kama vile mafanikio ya kujenga barabara zenye urefu wa km 18,000 ndani ya miaka nane tu ikilinganishwa na km 11,000 alizozikuta, daraja la kusini, la kigamboni, mradi wa mabasi yaendayo kasi, reli ya tanga to musoma+bandari ya musoma itakayoanza hivi karibuni, ufumbuzi wa tatizo la umeme, uvumilivu alionao, uhuru wa kutoa maoni bila mipaka, uhodari wa kutatua matatizo kama uchochezi wa wanasiasa n.k. Hata hivyo tusipozitambua juhudi hizo, watu wa mataifa mengine watazitambua na kumpongeza kwa uwazi kabisa.

Tutabaki tunalalamika kuwa Kikwete hivi Kikwete vile lakini ukweli utabaki kuwa J.K is a super president ever happened in TZ.!

Kimsingi mhe.Makalimoto uko sahihi,hizi propaganda za kusifiwa mara kwa mara ni aibu tupu kwa sisi kama watz.Kuwa ndani ya kumi bora si tija.Ila kwa mtazamo wako si dhambi.Ukiwa makini nchi nyingi za kiafrika zinafanya mambo ovyo ovyo sana ikiwemo Tanzania.Tanzania ingekuwa makini hada kwa 10% tungekuwa na uchumi bora kuliko nchi nyingi duniani.Leo kweli ndugu yangu nchi yetu inapitwa na vinchi vidogo kama Qatar,kenya,Rwanda,Rumenia na hata Mali.Tuwe wakweli nchi yetu kama tunataka kwenda lazima kwanza tubadili mitazamo.Shida yetu yawezekana hatusomi vitabu wala kutafuta ukweli wa mambo katika dunia hii.Kwa jinsi raslimali zilivvyonyingi tz na kwa kuwa chama tawala kimeshindwa kuzisimamia kwa manufaa ya watanzania ni bora tuwe wakweli chama cha mapinduzi kimeshindwa kazi.Wanaosifia ni wahuni na janga kwa taifa letu.Soma kwa undani kitabu cha BILDERBERG ujionee jinsi nchi kama tz inavyolazimishwa kubaki masikini.R.I.P CCM:watu wa diaspora tunarudi kusaidia ukombozi mpya wa nchi.
 
Ndugu yangu mtu kuwa Super president kuna vigezo.Tupe vigezo vinavyokufanya wewe useme huyo dugu yako ni super president. Naona wewe unaweza kuwa kilaza na huwezi kuwa na hoja za great thinkers. Usimsifu mtu kwasababu anatoka kwenu.Nchi imejiongoza kwa miaka saba tunasubiri kupoteza miaka mingine mitatu. kwaiyo Miaka kumi mingine imepotea tunasubiri kupata raisi wa kweli mwaka 2015,na si raisi Jina. Rafiki yangu soma vitabu vya graet leaders and great president usiwe kasuku wa kulishwa maneno.
 
Taifa hili tunakoelekea ni kubaya. Tabia ya baadhi ya watanzania kufanya siasa za udini, kumchafua rais yeyote anayekuwa muislam si sawa. Ni kweli kuwa watanzania tumekuwa mashabiki wa kumponda rais Kikwete, si kwasbbu yoyote bali ni kutokana na uislam wake. Mbona Nyerere aliua watu wengi na hammsemi. Aliwapiga exile watz kibao hamsemi eti mmeamua pia kumpa utakatifu, haya bwana. Lakini wajanja tunajua ubaya wa J.K mnaousemea ni upi. J.K si mbaya hivyo isipokuwa ni jitihada za baadhi yetu za kumhakikishia nchi haitawaliki.
 
Hiyo tuzo ya Mo Ibrahim atachukuwa rais Kikwete, akimaliza kipindi chake.
 
Ha ha ha haaaaaaa, mapovu ya nini jamani! Busara na hekima tu hapa wala si matusi. Ukweli ndo huo kuwa J.K yuko juu. Hata hizo miundombinu alizojenga nazo mmeamua msizione, daa kweli mmemchukia ******!
miundominu labda ungefuatilia ni utekelezaji tu wa mikataba iliyokuwepo toka nyuma si kitu aliekianzisha, alichokianzisha ambacho ktk utawala wake ningependa akitolee maelezo ni kilimo kwanza, mfumuko wa bei ya 20% kulinganisha na 0% aliyoikuta, kutopanda mishahara pamoja na ugumu wa maisha kupanda, ufisadi uliokithiri na kuwaogopa hao mafisadi, kuongeza deni la taifa, kunyimwa misaada na jumuia ya kimataifa kwa jinsi anavyoendesha uchumi vibaya hadi kufikia hatua ya kukopa benki za ndani na kuchukua pesa zetu za mifuko ya jamii na kupitisha sheria kandamizi ya kuzuia fao la kujitoa, kuchapisha noti zaidi kuliko mzunguko huku akijua fika ilo linamuumiza maskini wa chini, uuzaj wa ardhi holela kwa wageni, kuzidiwa na majirani zetu ktk east afrika kiuchumi hadi tunashindwa shindana nao!
 
Hivi takwimu za imf na world bank zinasemaje kuhusu uchumi wetu vile! Uchumi unapaa kwa kasi ya ajabu.Njoo kwenye halisi,afya zetu ziko vp,elimu je,? Ukipewa sifa za kijinga na wewe ukazikubali utakuwa na matatizo kwenye ubongo wako
 
Kaka hizo danganya toto ili waendelee kuchota maliasili zetu hakuna kitu hapo

Mgema akisifiwa...! hizi ripoti huwa na za kisanii ulaghai ambapo viongozi mbumbumbu huingia mkenge kwa kuendeleza sera mbovu na nia mbaya za kuifilisi nchi! tuliyaona haya hata wakati wa mkapa, ripoti lukuki zisizo kichwa wa miguu kutoka kila kona ya ulimwengu kumbe danganya toto watu mliwe vyenu!LOL
 
Inaonesha mleta mada karidhika na "ripoti" ya Mo Ibrahim Foundation na wala hataki kujiuliza wala kuchambua.

Je Mkalimotto, kwa kutumia akili zako kweli anaona kuna utawala bora, maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kupunguka kwa maradhi, umaskini, rushwa au njaa nchini?

Hizi peremende za wahujumu uchumi na mabosi zinatafutiwa "uhalali" na ripoti nyepesi kama hizo. Kwa sasa haziwezi fanikiwa, inabidi warudi studio!

Kuhusu mafanikio ya Kikwete je ni rasilimali kiasi gani imetumika (uwiano na tija) ktk kutengeneza hizo 18,000 kms za barabara? Je unajua kuwa kwa sababu ya rushwa na ubadhirifu uliokithiri kwenye serikali yake 1 km ya Kikwete ni sawa na 1.8km za wakati wa Mwinyi na 3.2km enzi za Mwalimu? Hilo daraja nalo sasa lishakuwa nongwa; lakini je unajua hiyo ilikuwa ni mikakati na mipango ya awamu ya kwanza na ya pili? Mwambie Kikwete ageuze Kigoma iwe Dubai kama alivyo ahidi hapo ndipo atakuwa na cha kujivunia......vinginevyo aendelee tu na misele yake duniani.
 
Back
Top Bottom