Mo Ibrahim: CCM awamu ya nne yavunja record utawala bora

MKALIMOTTO

Senior Member
Apr 7, 2012
136
9
Taarifa ya utawala bora iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Ibrahim Mo imemtaja Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuvunja record ya utawala bora kwa kuiingiza Tanzania kwa mara ya kwanza katika nafasi ya 10 bora kati ya nchi zaidi ya 50 za Africa.

Kati ya nchi hizo, ni Tanzania pekee kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati.

My take:
Watanzania tuzitambue na kuthamini juhudi anazozifanya rais wetu kama vile mafanikio ya kujenga barabara zenye urefu wa km 18,000 ndani ya miaka nane tu ikilinganishwa na km 11,000 alizozikuta, daraja la kusini, la kigamboni, mradi wa mabasi yaendayo kasi, reli ya tanga to musoma+bandari ya musoma itakayoanza hivi karibuni, ufumbuzi wa tatizo la umeme, uvumilivu alionao, uhuru wa kutoa maoni bila mipaka, uhodari wa kutatua matatizo kama uchochezi wa wanasiasa n.k. Hata hivyo tusipozitambua juhudi hizo, watu wa mataifa mengine watazitambua na kumpongeza kwa uwazi kabisa.

Tutabaki tunalalamika kuwa Kikwete hivi Kikwete vile lakini ukweli utabaki kuwa J.K is a super president ever happened in TZ.!
 
Lakini hao hao MO IBRAHIM wamesema mwaka huu hakuna nchi ama kiongozi atakae pata tuzo kwasababu hakuna aliefikia vigezo vyao..kwahiyo bwana zumbukuku kutuingiza top 10 ni blah blah tu hamna kitu hapo
 
JK anauza nchi yetu ndio maana hawaachi kumsifia! Hebu niambie kosa la marehemu Gaddafi ni lipi hata kustahili kuuawa? Ukiona hawa jamaa wa nje wanakusifia ujitazame na kujipanga upya!
 
Taarifa ya utawala bora iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Ibrahim Mo imemtaja Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuvunja record ya utawala bora kwa kuiingiza Tanzania kwa mara ya kwanza katika nafasi ya 10 bora kati ya nchi zaidi ya 50 za Africa.

Kati ya nchi hizo, ni Tanzania pekee kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati.

My take:
Watanzania tuzitambue na kuthamini juhudi anazozifanya rais wetu kama vile mafanikio ya kujenga barabara zenye urefu wa km 18,000 ndani ya miaka nane tu ikilinganishwa na km 11,000 alizozikuta, daraja la kusini, la kigamboni, mradi wa mabasi yaendayo kasi, reli ya tanga to musoma+bandari ya musoma itakayoanza hivi karibuni, ufumbuzi wa tatizo la umeme, uvumilivu alionao, uhuru wa kutoa maoni bila mipaka, uhodari wa kutatua matatizo kama uchochezi wa wanasiasa n.k. Hata hivyo tusipozitambua juhudi hizo, watu wa mataifa mengine watazitambua na kumpongeza kwa uwazi kabisa.

Tutabaki tunalalamika kuwa Kikwete hivi Kikwete vile lakini ukweli utabaki kuwa J.K is a super president ever happened in TZ.!

Kaka hizo danganya toto ili waendelee kuchota maliasili zetu hakuna kitu hapo
 
A wapi danganya wana ccm wenzako wenye akili kama zako hatima yenu iko ukingoni hakuna cha raisi bora analea mafisadi wenzake na kuingia kwenye kumi bora ni danganya toto ili waendelee kuchota rasilimali zetu nakushangaa sana ndugu yangu wewe unaishi Tanzania ipi huoni,husikii yanayoendelea? Na mwisho wa yote umekaribia
 
Twiga wazima wazima wamesafirishwa,madini wanachota kama ya kwao,mpaka sasa kuna pesa ziko uswis ,kesi ya richmond,iptl,epa,deepgreen,mikataba tata ya madini,tumegawa aridhi kwa agrisol kwa kodi ya tsh 200 kwa mwaka,tumeuza viwanja vya wazi,watoto wa vigogo wanaandaliwa kurihi uongozi......
Nauliza hivi TUNASITAHILI KUWA TOP 10 UTAWALA BORA???
 
Matatizo yote ya nchi anayabeba Pinda,ndio maana yeye JK anaonekana kama kiongozi bora.
Kama sasa yuko zake huko Oman anazindua ujenzi wa ofisi ya ubalozi!Kaaazi kweli kweli.
 
A wapi danganya wana ccm wenzako wenye akili kama zako hatima yenu iko ukingoni hakuna cha raisi bora analea mafisadi wenzake na kuingia kwenye kumi bora ni danganya toto ili waendelee kuchota rasilimali zetu nakushangaa sana ndugu yangu wewe unaishi Tanzania ipi huoni,husikii yanayoendelea? Na mwisho wa yote umekaribia
huyu ni diaspora kaka anatupotezea tu muda hapa!
 
SAS kashalainika...Mshiko(pension) unamsubiri Kikwete halafu tutajaambiwa HIZO NI ZILE ZA MONTH IBRAHIM!!
 
Ha ha ha haaaaaaa, mapovu ya nini jamani! Busara na hekima tu hapa wala si matusi. Ukweli ndo huo kuwa J.K yuko juu. Hata hizo miundombinu alizojenga nazo mmeamua msizione, daa kweli mmemchukia ******!
 
Twiga wazima wazima wamesafirishwa,madini wanachota kama ya kwao,mpaka sasa kuna pesa ziko uswis ,kesi ya richmond,iptl,epa,deepgreen,mikataba tata ya madini,tumegawa aridhi kwa agrisol kwa kodi ya tsh 200 kwa mwaka,tumeuza viwanja vya wazi,watoto wa vigogo wanaandaliwa kurihi uongozi......

Nauliza hivi TUNASITAHILI KUWA TOP 10 UTAWALA BORA???

Hivi ni chama gani ambacho vingozi wao hawajaandaa watoto wao? Hebu kitaje nikuorodheshee ndugu na jamaa na vimada walivyopangana.
 
Wakoloni wanapokusifia lazima ujiulize maswali!
Ina maana Mkwerre kamzidi Mwalimu Nyerere kwa utawala bora?
Upumbavu mtupu!
 
Tatizo sio utawala wa JK kuwa mzuri ni kwamba Africa wazuri wote hawapo so huyu ana afadhali eti? Sasa hizi nchi nyingine si ni balaa.. But look at sudan, ethiopia, drc, bhagbo, beghazi, tunisia, fall of egypt and qadfi etc.. Hawa ndio watu #- anaoshindana nao
 
Siyo swala la mkwerre wala mwalimu, jiulize mkwerre kakaa muda gani na mwalimu alikaa muda gani. Siyo unatokwa povu tu utadhani umebwia omo.
 
Taarifa ya utawala bora iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Ibrahim Mo imemtaja Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuvunja record ya utawala bora kwa kuiingiza Tanzania kwa mara ya kwanza katika nafasi ya 10 bora kati ya nchi zaidi ya 50 za Africa.

Kati ya nchi hizo, ni Tanzania pekee kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati.

My take:
Watanzania tuzitambue na kuthamini juhudi anazozifanya rais wetu kama vile mafanikio ya kujenga barabara zenye urefu wa km 18,000 ndani ya miaka nane tu ikilinganishwa na km 11,000 alizozikuta, daraja la kusini, la kigamboni, mradi wa mabasi yaendayo kasi, reli ya tanga to musoma+bandari ya musoma itakayoanza hivi karibuni, ufumbuzi wa tatizo la umeme, uvumilivu alionao, uhuru wa kutoa maoni bila mipaka, uhodari wa kutatua matatizo kama uchochezi wa wanasiasa n.k. Hata hivyo tusipozitambua juhudi hizo, watu wa mataifa mengine watazitambua na kumpongeza kwa uwazi kabisa.

Tutabaki tunalalamika kuwa Kikwete hivi Kikwete vile lakini ukweli utabaki kuwa J.K is a super president ever happened in TZ.!
MKALIMOTTO how all these projects are financed? It is possible the next president will inherent huge debts than those taken over by Mwinyi from Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo sio utawala wa JK kuwa mzuri ni kwamba Africa wazuri wote hawapo so huyu ana afadhali eti? Sasa hizi nchi nyingine si ni balaa.. But look at sudan, ethiopia, drc, bhagbo, beghazi, tunisia, fall of egypt and qadfi etc.. Hawa ndio watu #- anaoshindana nao

Sishangai its because you are a black bat- not known whether a bird or what!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom