Mo (copy cat) ashindwa kesi ya kuiga sabuni ya Wachina

Mo (copy cat) ashindwa kesi ya kuiga sabuni ya Wachina

GREAT VISIONAIRE

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Posts
365
Reaction score
454
Kampuni ya Keds Tanzania Co. Ltd imeshinda shauri lake dhidi ya kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL) ambayo inadaiwa kuiga nembo ya bidhaa ya sabuni ya unga ya Kleesoft.

MeTL inadaiwa kuipa sabuni yake jina la Mo Cleansoft ili kuwepo mfanano na jina la Kleesoft.

Kutokana na ushindi huo, bidhaa za sabuni ya Mo Cleansoft ambazo zilizuiwa ghalani wakati shauri hilo likisikilizwa, sasa zinachukuliwa kama bidhaa `bandia’.

Alipotafutwa kuhusu uamuzi huo, mwanasheria wa MeTL, Catherine Kisasa hakutaka kuzungumza lolote.

Shauri hilo lilifunguliwa Tume ya Ushindani (FCC) na kampuni ya Keds Tanzania na kusikilizwa na kamati ya usikilizaji wa shauri hilo. Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe watatu

Madai ya msingi ya Keds Tanzania yalikuwa ni kuwa kampuni ya MeTL iliiga vitu mbalimbali vilivyomo kwenye bidhaa yao, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Bidhaa (Merchandise Act).

Mambo mengine yaliyolalamikiwa ni kufanana kwa rangi na mwonekano wa vifungashio vya sabuni hizo mbili-- Kleesoft na Cleansoft-- huku Keds Tanzania wakiwatuhumu washindani wao kuwa wameiga rangi na muundo wa vifungashio vyao pamoja na kaulimbiu yao ya “Sabuni Kidogo, Nguvu Zaidi.”

Jambo jingine walilolalamikia ni mfanano wa matamshi ya majina ambao wanadai umekuwa ukiwachanganya walaji.

Matamshi ya majina ya Kleesoft na Cleansoft yanafanana, jambo ambalo wanadai linawachanganya wateja.

Baada ya Keds Tanzania kufungua shauri lao Novemba 7, FCC ilitoa notisi ya kuzuia kuuzwa kwa sababu za Mo Cleansoft ambazo zilizuiwa kwenye maghala mbalimbali ya Buguruni na Mbagala wakati shauri hilo likisikilizwa.

Kwa mujibu wa nyaraka za uamuzi wa FCC ambazo Mwananchi imeziona, FCC imebainisha kwamba muonekano wa sabuni hizo mbili unafanana, jambo ambalo linaweza kuwachanganya watumiaji wa bidhaa hizo.

“Tuna uhakika hata msikilizaji aliye makini hawezi kutofautisha majina hayo mawili yanapotamkwa,” inasema sehemu ya uamuzi wa FCC kama ulivyosainiwa na mwenyekiti wa kamati ya usikilizaji, Josephat Mkizungo.

Akizungumzia suala hilo, mwanasheria wa Keds, Lusajo Mwakalundwa alisema FCC imeamua kwamba sabuni ya Mo Cleansoft ni bandia na shehena iliyozuiwa Novemba 7 inatakiwa kuteketezwa.

“Tutaingia sokoni kukagua kama sabuni za Mo Cleansoft zinapatika. Zile tutakazozikuta zitatakiwa kuteketezwa kwa sababu ni bidhaa bandia,” alisema Mwakalundwa.

Mwanasheria huyo alisema wataenda mahakamani kuzuia uzalishaji wa Mo Cleansoft.

Aliwataka watumiaji wa bidhaa yao ya Kleesoft kuwa makini wanapotaka kununua sabuni hiyo kwa sababu inafanana kwa kiasi kikubwa na sabuni ya Mo Cleansoft.
 
Duuu huyu jamaa kapata ajali ya kawaida


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna hii Niceone na Doffi majina tofauti mwonekano unaofanana sana sijui nani kamwai mwenzake,watu wa production na masoko punguzeni copy and paste jitahidi kuwa wabunifu.Au ndio kusema graduate wetu wa vyuo vikuu awana upeo wa ubunifu zaidi ya kudurufu kazi za wenzao.Kwenye kampuni za maziwa watu wanaigana mpaka unajuliza tumeshindwa kuwa wabunifu.
 
Mzee wa ku copy!! Hatimaye apatikana!!! Yeye style yake anzisha bidhaa kwa kuumiza kichwa, ikipendwa tu sokoni, anakuja naye ki vyake!! Kwa kupitia humo humo!! Eti KLEENSOFT, anakuja na CLEAN SOFT!! Hahaaaa, hapo kweli kwenye matangazo ya radioni, msikilizaji atatofautisha vipi?
 
Sasa BRELA walisajilije business zinazofanana kimatamshi au kuna loopholes kwenye usajili wa majina ya biashara
Rejea mada hapo juu, Brela husajili Kampuni kama zilivyotajwa hapo juu. Kinachozungumziwa hapo ni bidhaa zinazomwendea mlaji ambao ni ubunifu wa kampuni husika ili kuliteka soko.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom