Mo (copy cat) ashindwa kesi ya kuiga sabuni ya Wachina

Mo (copy cat) ashindwa kesi ya kuiga sabuni ya Wachina

Mjanja huyu anakopigi alafu kile kineno "Mo" anakificha juu kama vat..ukiona maandishi makubwa hukumbuki kamo pale juu
Kampuni ya Keds Tanzania Co. Ltd imeshinda shauri lake dhidi ya kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL) ambayo inadaiwa kuiga nembo ya bidhaa ya sabuni ya unga ya Kleesoft.

MeTL inadaiwa kuipa sabuni yake jina la Mo Cleansoft ili kuwepo mfanano na jina la Kleesoft.

Kutokana na ushindi huo, bidhaa za sabuni ya Mo Cleansoft ambazo zilizuiwa ghalani wakati shauri hilo likisikilizwa, sasa zinachukuliwa kama bidhaa `bandia’.

Alipotafutwa kuhusu uamuzi huo, mwanasheria wa MeTL, Catherine Kisasa hakutaka kuzungumza lolote.

Shauri hilo lilifunguliwa Tume ya Ushindani (FCC) na kampuni ya Keds Tanzania na kusikilizwa na kamati ya usikilizaji wa shauri hilo. Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe watatu

Madai ya msingi ya Keds Tanzania yalikuwa ni kuwa kampuni ya MeTL iliiga vitu mbalimbali vilivyomo kwenye bidhaa yao, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Bidhaa (Merchandise Act).

Mambo mengine yaliyolalamikiwa ni kufanana kwa rangi na mwonekano wa vifungashio vya sabuni hizo mbili-- Kleesoft na Cleansoft-- huku Keds Tanzania wakiwatuhumu washindani wao kuwa wameiga rangi na muundo wa vifungashio vyao pamoja na kaulimbiu yao ya “Sabuni Kidogo, Nguvu Zaidi.”

Jambo jingine walilolalamikia ni mfanano wa matamshi ya majina ambao wanadai umekuwa ukiwachanganya walaji.

Matamshi ya majina ya Kleesoft na Cleansoft yanafanana, jambo ambalo wanadai linawachanganya wateja.

Baada ya Keds Tanzania kufungua shauri lao Novemba 7, FCC ilitoa notisi ya kuzuia kuuzwa kwa sababu za Mo Cleansoft ambazo zilizuiwa kwenye maghala mbalimbali ya Buguruni na Mbagala wakati shauri hilo likisikilizwa.

Kwa mujibu wa nyaraka za uamuzi wa FCC ambazo Mwananchi imeziona, FCC imebainisha kwamba muonekano wa sabuni hizo mbili unafanana, jambo ambalo linaweza kuwachanganya watumiaji wa bidhaa hizo.

“Tuna uhakika hata msikilizaji aliye makini hawezi kutofautisha majina hayo mawili yanapotamkwa,” inasema sehemu ya uamuzi wa FCC kama ulivyosainiwa na mwenyekiti wa kamati ya usikilizaji, Josephat Mkizungo.

Akizungumzia suala hilo, mwanasheria wa Keds, Lusajo Mwakalundwa alisema FCC imeamua kwamba sabuni ya Mo Cleansoft ni bandia na shehena iliyozuiwa Novemba 7 inatakiwa kuteketezwa.

“Tutaingia sokoni kukagua kama sabuni za Mo Cleansoft zinapatika. Zile tutakazozikuta zitatakiwa kuteketezwa kwa sababu ni bidhaa bandia,” alisema Mwakalundwa.

Mwanasheria huyo alisema wataenda mahakamani kuzuia uzalishaji wa Mo Cleansoft.

Aliwataka watumiaji wa bidhaa yao ya Kleesoft kuwa makini wanapotaka kununua sabuni hiyo kwa sababu inafanana kwa kiasi kikubwa na sabuni ya Mo Cleansoft.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utajiri wake unatokana na kudandia innovations za watu...hatar sana
 
Aisee. Copy nyingine hovyo kabisa. Na alijua ni bomba maana Kleensoft ndiyo sabuni ya unga iliyotamba sokoni na bora kabisa. Ngoja na sisi tuangalia bag la subuhi pengine tulishaligwa na bandia ya Mo.
 
"Jambo jingine walilolalamikia ni mfanano wa matamshi ya majina ambao wanadai umekuwa ukiwachanganya walaji".
Walaji wa sabuni[emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
ukisikia mlaji unachowaza ni kupeleka mdomoni?? Mtumiaji yoyote WA mwisho WA bidhaa yoyote anaitwa mlaji Kwa Kiswahili,hata mtengenezq betri anawaita wateja wake WA mwisho kama walaji Kwa kiingereza unaweza waita "consumers"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom