Cosmasjulius
JF-Expert Member
- May 22, 2018
- 695
- 1,024
Mpuuzi sana hyu muhindi bingwa wa kuigaiga ameshindwa kuajiri wabunifu kaxi ya kuajiri mapopoma ili atajirike zsidi kupitia wenzie hovyo ili jamaa la mikia😀😀😀Mzee wa ku copy!! Hatimaye apatikana!!! Yeye style yake anzisha bidhaa kwa kuumiza kichwa, ikipendwa tu sokoni, anakuja naye ki vyake!! Kwa kupitia humo humo!! Eti KLEENSOFT, anakuja na CLEAN SOFT!! Hahaaaa, hapo kweli kwenye matangazo ya radioni, msikilizaji atatofautisha vipi?
mkuu watu wameupiga chini hauna soko kabisaAmetoa hadi mo ukwaju aisee anauza 300 tu [emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
Wazo zuri!
!
Yes.... Kuliko Kuziteketeza Ni Bora Wakazigawa Kwa Wagonjwa, Wafungwa, Mashuleni Na Kadhalika
Povu la nn akwende anaiga sana atafute watu wenye vipaji vyao hawalipe vzri naona mbumbumbu roho zinawauma😀😀😀😀mnaotumia muda kumnanga Mo, tuelezeni nyie mlivyoanzisha vya kwenu? Umekaa umeajiriwa halafu unaleta dharau kwa watoa ajira, umbwaa kabisa
Graduate ni tatizo . Lakini unakuta ni certificate graduateKuna hii Niceone na Doffi majina tofauti mwonekano unaofanana sana sijui nani kamwai mwenzake,watu wa production na masoko punguzeni copy and paste jitahidi kuwa wabunifu.Au ndio kusema graduate wetu wa vyuo vikuu awana upeo wa ubunifu zaidi ya kudurufu kazi za wenzao.Kwenye kampuni za maziwa watu wanaigana mpaka unajuliza tumeshindwa kuwa wabunifu.
Walaji=Consumers"Jambo jingine walilolalamikia ni mfanano wa matamshi ya majina ambao wanadai umekuwa ukiwachanganya walaji".
Walaji wa sabuni[emoji848][emoji848]
Sent using Jamii Forums mobile app
Mo kazidi sasa, pia sijui kwanini sio wabunifu, kaiga sabuni ya jamaa vilevile tofauti ni jina tuMzee wa ku copy!! Hatimaye apatikana!!! Yeye style yake anzisha bidhaa kwa kuumiza kichwa, ikipendwa tu sokoni, anakuja naye ki vyake!! Kwa kupitia humo humo!! Eti KLEENSOFT, anakuja na CLEAN SOFT!! Hahaaaa, hapo kweli kwenye matangazo ya radioni, msikilizaji atatofautisha vipi?
Mkuu hatuwezi kuwa wote wazalishaji,tunachozungumzia hapa ni kukosa ubunifu wa bidhaa zake.kwa mfano bidhaa ya ukwaju haikuwepo sokoni Azam ndio wameileta hii bidhaa sasa kwa tabia yake alipoona Azam amepiga bao na yy akaleta wa kwake.Matokeo yake amepiga chinimnaotumia muda kumnanga Mo, tuelezeni nyie mlivyoanzisha vya kwenu? Umekaa umeajiriwa halafu unaleta dharau kwa watoa ajira, umbwaa kabisa
Ni Kleesoft na siyo Kleensoft.Mzee wa ku copy!! Hatimaye apatikana!!! Yeye style yake anzisha bidhaa kwa kuumiza kichwa, ikipendwa tu sokoni, anakuja naye ki vyake!! Kwa kupitia humo humo!! Eti KLEENSOFT, anakuja na CLEAN SOFT!! Hahaaaa, hapo kweli kwenye matangazo ya radioni, msikilizaji atatofautisha vipi?
Huwezi kuwa na marketing team mzuri kama hauwalipi vizuriZa mwizi 40 amezidi kuiga sijui Hana marketing team nzuri inayo weza kufanya innovation
Biashara za MO zimejaa ujanja ujanja sana!Kampuni ya Keds Tanzania Co. Ltd imeshinda shauri lake dhidi ya kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL) ambayo inadaiwa kuiga nembo ya bidhaa ya sabuni ya unga ya Kleesoft.
MeTL inadaiwa kuipa sabuni yake jina la Mo Cleansoft ili kuwepo mfanano na jina la Kleesoft.
Kutokana na ushindi huo, bidhaa za sabuni ya Mo Cleansoft ambazo zilizuiwa ghalani wakati shauri hilo likisikilizwa, sasa zinachukuliwa kama bidhaa `bandia’.
Alipotafutwa kuhusu uamuzi huo, mwanasheria wa MeTL, Catherine Kisasa hakutaka kuzungumza lolote.
Shauri hilo lilifunguliwa Tume ya Ushindani (FCC) na kampuni ya Keds Tanzania na kusikilizwa na kamati ya usikilizaji wa shauri hilo. Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe watatu
Madai ya msingi ya Keds Tanzania yalikuwa ni kuwa kampuni ya MeTL iliiga vitu mbalimbali vilivyomo kwenye bidhaa yao, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Bidhaa (Merchandise Act).
Mambo mengine yaliyolalamikiwa ni kufanana kwa rangi na mwonekano wa vifungashio vya sabuni hizo mbili-- Kleesoft na Cleansoft-- huku Keds Tanzania wakiwatuhumu washindani wao kuwa wameiga rangi na muundo wa vifungashio vyao pamoja na kaulimbiu yao ya “Sabuni Kidogo, Nguvu Zaidi.”
Jambo jingine walilolalamikia ni mfanano wa matamshi ya majina ambao wanadai umekuwa ukiwachanganya walaji.
Matamshi ya majina ya Kleesoft na Cleansoft yanafanana, jambo ambalo wanadai linawachanganya wateja.
Baada ya Keds Tanzania kufungua shauri lao Novemba 7, FCC ilitoa notisi ya kuzuia kuuzwa kwa sababu za Mo Cleansoft ambazo zilizuiwa kwenye maghala mbalimbali ya Buguruni na Mbagala wakati shauri hilo likisikilizwa.
Kwa mujibu wa nyaraka za uamuzi wa FCC ambazo Mwananchi imeziona, FCC imebainisha kwamba muonekano wa sabuni hizo mbili unafanana, jambo ambalo linaweza kuwachanganya watumiaji wa bidhaa hizo.
“Tuna uhakika hata msikilizaji aliye makini hawezi kutofautisha majina hayo mawili yanapotamkwa,” inasema sehemu ya uamuzi wa FCC kama ulivyosainiwa na mwenyekiti wa kamati ya usikilizaji, Josephat Mkizungo.
Akizungumzia suala hilo, mwanasheria wa Keds, Lusajo Mwakalundwa alisema FCC imeamua kwamba sabuni ya Mo Cleansoft ni bandia na shehena iliyozuiwa Novemba 7 inatakiwa kuteketezwa.
“Tutaingia sokoni kukagua kama sabuni za Mo Cleansoft zinapatika. Zile tutakazozikuta zitatakiwa kuteketezwa kwa sababu ni bidhaa bandia,” alisema Mwakalundwa.
Mwanasheria huyo alisema wataenda mahakamani kuzuia uzalishaji wa Mo Cleansoft.
Aliwataka watumiaji wa bidhaa yao ya Kleesoft kuwa makini wanapotaka kununua sabuni hiyo kwa sababu inafanana kwa kiasi kikubwa na sabuni ya Mo Cleansoft.
Si ingezoeleka tu kuwaita watumiaji badala ya walaji? Hivi ni sahihi kusema kuna walaji wanaokula sabuni ya Kleesoft? Maana ingeleta maana nzuri tu kusema watumiaji wanaotumia bidhaa au huduma fulani.Kwenye lugha ya biashara mtumiaji wa mwisho ndio mlaji "consumer".
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Anaweza kuikopi yanga huyu....
ni kukaa nae chonjo...
Ndio!"majina ambao wanadai umekuwa ukiwachanganya walaji."
Walaji wa sabuni au ?
Sent using Jamii Forums mobile app
"majina ambao wanadai umekuwa ukiwachanganya walaji."
Walaji wa sabuni au ?
Sent using Jamii Forums mobile app
Vyoyote vile lakini kwenye matamshi, mtu kutofautisha ni vigumu!!Ni Kleesoft na siyo Kleensoft.