Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,722
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Nipashe la Jumapili ya leo kwa humu jf, nimeweka hoja na swali "Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Kwa Aliyoyafanya, Anastahili Pongezi na Shukrani Stahiki!. Watanzania Wenye Shukrani Tumshukuru au Bado?".
Juzi Ijumaa nimemsikiliza kwa makini sana hotuba ya Rais Samia, kulivunja Bunge kuhitimisha utawala awamu yake ya kwanza ya utawala wa Awamu ya sita, nimemsikiliza kupitia jicho la tatu na sikio la tatu, kiukweli kabisa, Rais Samia amefanya mengi, makubwa, mazuri, anastahili apewe asante yake stahiki, na kama stahiki yake ni kupewa maua, apewe tuu maua yake!.
Japo siungi mkono kiongozi kutoa hotuba ndeefu kwa zaidi ya saa mbili, kwasababu wataalamu wa saikolojia ya umakini wa ubongo wa binadamu wanasema ubongo wa binadamu unaweza kumakinika kwa lisaa moja tuu, mtu ukihutubia zaidi ya saa 1, ubongo unashika baadhi tuu, na mengine yanapitia huku na kutokea kule, lakini kwa vile mafanikio ni mengi, wasaidizi wake hutuba, walikuwa na kibarua kigumu cha kuamua yapi wayaweke na yapi wayaache maana mazuri ni mengi, enzi za JPM, niliwashauri Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . na kwa vile Watanzania wameukubali ushauri wangu huu, Pre GE2025 - Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! hivyo 2025 tunakwenda na Mama kwa kumpa mitano 5, provided kama HII sauti niliyoisikia sio sauti ya kweli ya kwake YEYE, then nawashauri na Wasaidizi wa Samia, wawe wanamuandalie hotuba concise, akihutubia asizidishe lisaa limoja!.
Hapa nimezungumzia kumsikiliza kwa makini kwa kumsikiliza huku unamtazama kwa jicho la tatu na kumsikiliza kwa kuisikiliza sauti kwa sikio la tatu. Hakuna ubishi kwenye hotuba za viongozi, kuna vitu kiongozi huwa anaandikiwa, yeye anavipitia na kuvisoma, kuvipunguza au kuviongeza na kuna vitu ni vyake mwenyewe anatoa moyoni mwake, anaviongeza kwenye kuhutubia, kwenye muziki hii inaitwa adlib, kwenye hotuba ni impromptu.
Sisi wenye jicho la tatu, jicho tunduizi, tukimsikiliza mtu anapohutubia hotuba rasmi, huku tunamtazama, japo kila anachohutubia ni anasema yeye, lakini tunauwezo wa kubaini hiki anakisema kwasababu ameandikiwa na hiki anakisema ni kimetoka moyoni, mhutubiaji akisema vitu vya kusema tuu, tunasema ni paying lip services, niliishawahi kuliulizia hili humu Je, kuna uwezekano baadhi ya Viongozi wetu wanatoa baadhi ya Ahadi kwa "Paying lip Services"? miongoni mwa vitu ambavyo Rais Samia amevisema kwa kuvitoa moyoni mwake kwenye hotuma ya Rais Samia kulivunja Bunge ile sehemu ya shukrani!.
Mimi nitaweka vichache nilivyovisikia vya kutoka moyoni mwake, na kikubwa nilichoguswa nacho sana ni jinsi Rais Samia alivyo mtu rahimu, mtu wa shukrani kwa kutoa shukrani za dhati toka moyoni mwake kwa makundi mbalimbali, kuanzia kwa wasaidizi wake hadi wale wa ofisi binafsi zikiwemo shukrani kwa liwazo lake la moyo wake, na kukiri hii kazi ya urais ni kazi ngumu, bila liwazo la moyo, mtu unakuwa huwezi!, pia zile shukrani kwa wapinzani, shukrani kwa kukosolewa na shukrani hadi kwetu sisi waandishi wa habari ni vitu vya moyoni kwake, this is good, inaonyesha the human side of Samia, hii niliwahi kuisema humu, Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila... hii inamaana kuna yale mambo fulani ya ajabu ajabu yanayotokea na serikali yake kunyooshewa kidole, ni uthibitisho sio yeye, ila kwavile mkubwa ni jalala, kila ubaya, atatupiwa yeye, na hapa simaani yeye ni mtakatifu au ni malaika na hawezi kukosea Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda muda wenyewe sasa ndio umefika, muda muafaka ukifika, Watanzania wote katika umoja wetu, twendeni tukafanya lile jambo letu!.
Kwa maoni yangu, viongozi wetu wanapohutubia, wasaidizi wao hotuba, wajifunze kuanda hotuba za kisasa ambazo ni hotuba smati, ambazo ni ahadi kwenye hotuba hizo ni ahadi za kisasa zenye kitu kinachoitwa SMART Objectives, zenye ahadi zenye malengo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu wa utekelezaji. Sio kiongozi anahutubia na kusema tuu, tutafanya hiki na kile, bila kuonyesha kitafanywa lini.
Tanzania kuliwahi kutokea watu, wakati wa kuomba wa kuomba kura, wakainadi ilani ya chama chao, tuliahidiwa kukamilisha mchakato wa katiba mpya, Watanzania wapenda demokrasia tukajitoa kwa moyo kwelikweli, tukajituma, tukapiga kura kwa wingi kwa matumaini ya kupata katiba mpya. Baada ya kuchaguliwa, kibao kikageuka kiongozi mkuu akasema “katiba sio kipaumbele changu”. Hilo la katiba likaishia hapo!. Awamu ya pili ya kiongozi huyo, hilo la katiba mpya halikuwepo tena kwenye ila na likaishia hapo!.
Sisi watu wa media kama mhimili wanne, hatukupaswa kunyamazia hilo, tulipaswa kumbananisha, ukiahidi, lazima utekeleze!, mimi angalau angalau nililiulizia Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?
Sisi media ya Tanzania tunapaswa kubadilika twende na usasa, tufike kiwango cha kuweka kumbukumbu kwa kutumia uandishi wa kisasa wa data journalism, uandishi wa takwimu, siku kiongozi anaingia, madarakani, anaahidi nitafanya hiki na kile, ile hotuba yake ya kwanza zile ahadi tunaziweka kwenye bullet points (silijui neno hili kwa Kiswahili), ila yale uliyoyasema, na kuyaahidi, tunayaorodhesha na kuyaweka kumbukumbu kwa pointi fomati.
Utawala wake ukifika katikati kati ya muhula, baada ya miaka 2 na nusu, tunamfanyia kitu kinaitwa MTR (mid term review), kwenye yale aliyoahidi, ametekeleza yapi na yapi bado?. Mimi nilimfanyia Rais Samia MTR Ili kuisaidia nchi na kumsaidia Rais Samia, je tumfanyie an honest MTR based on SMART Objectives za tulipotoka, tulipo to determine tunapokwenda? Halafu mwisho wa awamu yake tunakuja na tathmini kuu ya yote aliyoahidi, aliyotekeleza na ambayo hakutekeleza, ndipo tunamtathmini atatufaa aendelee au ajipumzikie tuu, tutafute mwingine.
Rais Samia, kwa vile alipoingia, aliingia kwa kukuta mambo yameishapangwa na kuanzwa na mtangulizi wake, tunapaswa kumshukuru kwa kuyapokea kwa kukubali kuyaendeleza mazuri yote ya mtangulizi wake kisha na yeye akaongezea mapya ya kwake, na ametekeleza kikamilifu kwa kukamilisha aliyoyakuta na kuongeza mapya. Kiukweli anastahili.
Kutokana na urefu wa hotuba yake mimi nimeguswa zaidi na kile kipande cha shukrani. Nilikuwa nikisikiliza hatuba za Mwalimu Nyerere, Rais Mwinyi na Mkapa, hakuna hata mara moja wanafamilia wameshukuriwa hata kutajwa tuu. JK angalau angalau, JPM, tumwache apumzike, lakini Rais Samia, ameishukuru familia yake likiwemo liwazo la moyo wake.
Hatuba hii ya Rais Samia, ndio kwa mara yangu ya kwanza nimemsikia rais wa JMT, akiwashukuru wapinzani na kusema wote ni Watanzania, tunajenga nyumba moja, hatuna sababu kugombea fito. Maneno hayo ni faraja sana kwa upinzani na naamini tutashuhudia hata kale ka simba ka Kizimkazi, kakiachiliwa kutoka kwenye ile cage!. Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
Kwa mara ya kwanza, rais wa JMT, ameushukuru ukosoaji!, akasema unamsaidia kurekebisha na kujenga. Maneno haya ni makubwa sana, yanayothibitisha hawa wakosoaji wanaopotezwa kubugudhiwa na kushughulikiwa, wanashughulikiwa na watu wasiojulikana na sii yeye na serikali yake!. "Kati ya Wasifiaji wa Rais Wakiwemo Machawa na Wakosoaji wa Rais, Watu Critical, Nani Wanamsaidia zaidi Rais, Serikali Yake?
Katika hotuba hii, pia ni kwa mara ya kwanza sisi watu wa mhimili wanne, media, tumeshukuriwa kwa kazi nzuri. Hakuna kitu kinaleta faraja kama appreciation, kushukuriwa kwa unachokifanya. Asante sana Rais Samia kwa hili, akirejea, asiishie kutupongeza media, atuwezeshe tuweze Media ni Mhimili Muhimu kama ile mitatu ila ni dhaifu kiuchumi. Je, imefika wakati wapewe Ruzuku au iachwe ipambane na hali yake?
Nimalizie kwa kutoa wito kwa Watanzania, tuwe watu wa shukrani, unapotendewa wema, na kushukuriwa, nawe lipa wema, tusiwe watovu wa fadhila na watovu wa shukrani, tumrudishie shukrani zetu stahiki. Rais Samia anastahili ….. shukrani zetu, tumpe tuu maua yake Kwa kukamilisha yale ya mtangulizi wake, kisha kujumlisha na ya kwake anayotenda, kutomshukuru ni kujichumia tu dhambi za bure!
Namalizia na lile swali la msingi la uzi huu
"Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Kwa Aliyoyafanya, Anastahili Pongezi na Shukrani Stahiki!. Watanzania Wenye Shukrani Tumshukuru au Bado?.
Mungu Mbariki Rais Samia,
Mungu Tubariki Watanzania Tuwe Watu wa Shukrani na Kukumbuka Fadhila
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.