Mnyika: Ni miezi 5 sasa NEC hawajajibu barua yangu kuhusu walikopata majina ya Wabunge 19 na nani amesaini fomu zao

Kwanini hiyo barua ya Mnyika aliyopeleka Tume haiwekwi hadharani?

Hilo lingeepusha Spika wa Bunge kukejeliwa kama ilivyo sasa na kupoteza heshima ya Bunge.

Tupunguze hadithi za kutunga
Muulize mnyika alimwandika na yule aliekuwa magereza na kutuma watu wakamtoe usiku kinyume na taratibu ili akaapishwe,jamani Hutu kashikiwa akili
 
Kwanini hiyo barua ya Mnyika aliyopeleka Tume haiwekwi hadharani?

Hilo lingeepusha Spika wa Bunge kukejeliwa kama ilivyo sasa na kupoteza heshima ya Bunge.

Tupunguze hadithi za kutunga
Mwambie mnyika aiweke kwa sababu anayo copy yake.
Spika hawezi kuiweka mtandaoni kwa kuwa anajua kulinda heshima ya kiapo chake cha maadili.

Ukiitaka mwambie mnyika aiweke.
 
Kinachofikirisha.... Chadema kwa walivyojimbanua kuwa ni watetezi wa haki na utawala wa sheria kwanini mpaka sasa hawajibu rufaa ya kina Mzee Mdee, kwa nini wanaendelea kupokea ruzuku isiyo halali.. Ndugai aliwahoji ikiwa wanaamini wabunge hao si halali wanashindwa nini kuweka pingamizi mahakamani?🤔
 
Kwa jinsi mchezo unavyoonekana hauhitaji hata akili ndogo kujua ubunge wa akina halima ni magumashi . Akina halima wanatafuta hela.

Ninachojiuliza ni kwanini spika anawang'ang'ania?
Wanawategemea sana kujenga hoja?:- maana ni kweli wanajitahidi sana kwenye kujenga hoja.
Au ni mapenzi,, maana idadi ya wanawake bungeni ni ndogo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…