Mnyika: Ni miezi 5 sasa NEC hawajajibu barua yangu kuhusu walikopata majina ya Wabunge 19 na nani amesaini fomu zao

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,725
141,586
Katibu mkuu wa Chadema J J Mnyika amesema ni miezi 5 imepita tangu amwandikie mkurugenzi wa uchaguzi NEC akitaka kujua ni nani alipeleka orodha ya majina ya akina Halima Mdee na wenzake na form zao zilisainiwa na nani pahala alipotakiwa kusaini Katibu mkuu.

J J Mnyika anashangazwa sana na ukimya wa NEC ambao walipokea barua yake tangu 27/11/2020

Ikumbukwe hapa tarehe 10/05/2021 Bawacha wanatimba bungeni kwenda kuwafurusha akina Halima Mdee na wenzake.

mnyika.JPG

1.jpg
2.jpg
Kazi Iendelee!
 
Attachments

  • Barua ya Mnyika.pdf
    476.2 KB · Views: 12
Covid 19 ni shida wanatafuna kodi zetu na kutusababishia hasara huku wakina spika wakiwa wanawalinda nadhani kuna kitu nyuma ya pazia wale wanaowalinda wanafaidika.
 
Na mwingine akatolewa gerezani usiku wa manane alfajiri akapewa ubunge! Hii nchi ilichezewa sana kwa kiwango kisichomithilika; kwa kiwango cha kutia aibu! Na bado wahusika pamoja na uvunjaji wa hatari wa Katiba na sheria za nchi wapo; wamekalia ofisi za umma bila wasiwasi
 
Chadema wakianza kulalamika tu haileti maana hichi ni chama walitakiwa kuwa na misimamo mikali katika mambo ya msingi kama haya ya kichama manaachia watu kuwafanyia maamuzi ya ndani na miezi mitano mko kimyaa tu. Kuweni strong katika maamuzi ya kimsingi
 
Bawacha watakinukisha wiki ijayo!
 
Chadema wakianza kulalamika tu haileti maana hichi ni chama walitakiwa kuwa na misimamo mikali katika mambo ya msingi kama haya ya kichama manaachia watu kuwafanyia maamuzi ya ndani na miezi mitano mko kimyaa tu. Kuweni strong katika maamuzi ya kimsingi
Wafanyaje wavamie jengo la NEC?
 
Back
Top Bottom