Mnyika kinara bungeni

Mnyika kinara bungeni

Mnyika kinara bungeni
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), kwa sasa ndiye anashikilia rekodi ya ukinara wa kuchangia mara nyingi bungeni, akifuatiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA) na Godfrey Zambi wa Mbozi Mashariki (CCM).

Kwa mujibu ya rekodi zalizomo kwenye mtandao wa Bunge, Mnyika ambaye ni kipindi chake cha kwanza bungeni, ameonekana kufanya vizuri zaidi sambamba na wabunge wenzake kadhaa wa CHADEMA.

Takwimu hizo hazijawahusisha mawaziri, manaibu wao, Spika, naibu wake, wenyeviti watatu wa Bunge, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa vile nafasi zao zinawapa uwezekano mkubwa wa kuchangia hoja wakati wowote.
Wabunge kumi ambao wameshika nafasi za juu ni Mnyika akiwa amechangia (184), kuuliza maswali ya nyongeza (28) na msingi (7), akifuatiwa na Zitto (79), (25) na (8) wakati Zambi anashika nafasi ya tatu kwa (70), (26) na (9).

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anashika nafasi ya nne akiwa amechangia mara 93, maswali ya nyongeza 19 na yale ya msingi 7, akifuatiwa na Diana Chilolo wa Viti Maalumu (CCM) aliyechangia mara 61, maswali ya nyongeza 41 na msingi 9.

Nafasi ya sita inashikiliwa na Halima Mdee wa Kawe (CHADEMA) akiwa na rekodi ya 59, 15 na 6 akifuatiwa na Moses Machali wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi) mwenye michango 57, nyongeza 30 na maswali ya msingi 7.

Magdalena Sakaya wa Viti Maalumu (CUF) amejinyakulia nafasi ya nane akiwa na michango 52, maswali ya nyongeza 13 na ya msingi 4, huku Mbunge wa Kisarawe, Seleman Jafo (CCM) akifuatia kwa 51, 10 na 6.

Anayefunga dimba kwa kumi bora ni Ester Bulaya wa Viti Maalumu (CCM) mwenye michango 47, nyongeza 17 na maswali ya msingi 3, akiwa amefungana na Martha Mlata wa Viti Maalumu (CCM) mwenye rekodi ya michango 47, nyongeza 11 na maswali ya msingi 5.
Ni takriban miaka miwili tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu, ambapo vyama vya upinzani hususan CHADEMA, wabunge wake wameendelea kuonesha umahiri bungeni, kwani hata Bunge la tisa lililopita kwa mujibu wa utafiti wa shirika moja, Zitto na Dk. Willibrod Slaa akiwa mbunge wa Karatu wakati huo, walishika nafasi za juu.

Katika mtiririko huo wa takwimu hizo kwenye mtandao wa Bunge, wabunge wanaoonekana kuwa na alama ndogo wengi ni wale wa Viti Maalumu CCM na baadhi ya CUF.


Source: Tanzania Daima 20/8/12

Nimekuta hii twitter Mnyika akipewa kubwa JJMnyika: "@Allykhana: JJMnyika tuondolee unafiki wenu yaan leo ndio mnawatakia Waislam heri ya Eid?"►Nashukuru kwa mtizamo wako.Leo pia ni Eid(pili)


Ebu angalieni Mnyika alivyo kilaza yaan kaacha watumia Waislam Heri ya sikuku jana leo analeta majibu mepesi namna hii

Huyu Kilaza kazoea miongozo upstairs pamejaa makamasi
 
Last edited by a moderator:
Mbona unapanic! Usijali bado muda hupo wa kutatua hizo kero bila shaka Mnyika atafanyia kazi kero zako!

Anaonewa vipi wakati yeye kinara? Hivi vijisababu eti Keenja kakaa miaka mingapi ni vya kisengelema. Siku tukiwapa nchi CDM watakuja na majibu hayo hayo CCM imekaa miaka 50. Wakati anaomba kura Mnyika alisema ataondoa hizi kero na akirudi atapimwa kwa hilo sio idadi ya miongozo ya spika.
 
Huyo si bado mwanjomwanjo, ndio mwaka mara yake ya kwanza bungeni ana moto, sijui kama atakuwa na nyingine ya kuchaguliwa.
 
Na top ten ya wanaolala ni
1. Wassira
2. Komba
3. Kabaka
4. Mrema
.
.
.
etc
 
anastahili pongezi ikizingatiwa kuwa hoja zake nyingi zilikuwa na mashiko angalau kodi zetu zimeenda kihalali tofauti na baadhi ya wale walalavi na waleta ushindani usio na maana
 
Na top ten ya wanaolala ni
1. Wassira
2. Komba
3. Kabaka
4. Mrema
.
.
.
etc

Mkuu ongeza Annah Makinda na Job Ndugai kwani hata wakikalia kile kiti maamuzi wanatoa wakitoka usingizini
 
Nimekuta hii twitter Mnyika akipewa kubwa JJMnyika: "@Allykhana: JJMnyika tuondolee unafiki wenu yaan leo ndio mnawatakia Waislam heri ya Eid?"►Nashukuru kwa mtizamo wako.Leo pia ni Eid(pili)


Ebu angalieni Mnyika alivyo kilaza yaan kaacha watumia Waislam Heri ya sikuku jana leo analeta majibu mepesi namna hii

Huyu Kilaza kazoea miongozo upstairs pamejaa makamasi

Mkuu naona elimu akhera imekukaa kweli. Hapa tumia elimu DUNIA
 
Nenda John nenda na udhidi kusonga mbele,kama mtu anaona hufanyi la maana jimboni kwako huyo analake jambo.Umakini wako hata lukuvi anauelewa,uonae John hatendi vyema jimboni umejaribu kuwasiliana nae kujua tatizo?Ikiwa una lengo nzuri na wanaUbungo, mshauri mbunge harafu uone utelezaji wake kwani wote lengo ni kuondoa kero za wananchi hasa kwa kutumia vitu vitatu yaani AKILI, UTASHI na UHURU.
 
leteni na kumi bora za wavivu na watoro bungeni tujue, ili 2015 tuchukue maamuzi sahiii.!
 
cha muhimu ni kutoa points, kuna wabunge ni vinara wa kusimama lakini michango yao ni pumba tupu.. na wengine wanafanya kazi ya kuijibia serikali (mbunge haelewi anafanya nini bungeni) kisingizio ni kuitetea serikali ya chama changu.

next time tunahitaji vinara wa kutoa points kama huyo Chilolomo, jafu, mkalata ni pigo kwa watz lkn wapo top 10 na huwezi kuwalinganisha na mtu kama filikunjombe
 
Mkuu ningekushauri badala ya kuhangaika na Mnyika kwa kupiga propaganda ungefanya jitihada za kuleta mrejesho wa mbunge wa Ukonga ambaye tangu achaguliwe hajawahi kukutana na watu wake na ndiye mbunge ambaye nauli ya daladala kwenye jimbo lake ni Sh 1000 kutokana na ubovu wa barabara.Lakini huyu humsemei kwa vile ni kada mwenzio siyo?
Molemo mbona hunielewi. Mimi nasema juu ya Mbunge wangu Mnyika ambaye nilimpa kura. Sina haja na wabunge wa majimbo mengine; hayo hayanihusu. Kama hawawatendei haki wapiga kura wao basi na wao watapata haki yao; sitaki Mnyika afike huko.
 
Last edited by a moderator:
Ipo kwenye bajeti tayari

Si kweli! Naambiwa na wakazi wa kule kwamba alishafanyiwa design lakini hata malipo kwa watakaobomolewa bado. Hapo ndipo Mnyika akaze buti aipate hiyo barabara na ya maramba mawili na pia zile za Goba; hapo atapeta lakini akijielekeza na kujikita tu kwenye bandari na uwekezaji next uchaguzi labda akagombee kwingine. Ni ushauri tu
 
Nimeipenda sana hiyo,CCM wajue sasa mambo yamebadilika na sasa wajiandae kwa Movement 4 Exchange.
 
Molemo mbona hunielewi. Mimi nasema juu ya Mbunge wangu Mnyika ambaye nilimpa kura. Sina haja na wabunge wa majimbo mengine; hayo hayanihusu. Kama hawawatendei haki wapiga kura wao basi na wao watapata haki yao; sitaki Mnyika afike huko.

Nina uhakika ulimpa kura yule mama wa CCM.Hata kama ni kiapo nitakula kuthibitisha hukumpa Mnyika kura.Hata Mnyika afanye mema mangapi kamwe huwezi kumuunga mkono.

Mnyika kijana wetu songa mbele,idadi kubwa ya wapiga kura wako tunakuunga mkono.....
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na kuwa kinara wa kuchangia pia alikuwa mnywaji mzuri pale chako ni chako hadi anakopa nadhani kuna uhusiano wa nguvu alikokuwa anazipata za kuchangia ***** bungenii maana lunch lazima apite ashtue na asubuhi pia anashtua!!:A S-baby:
 
Back
Top Bottom