Acha wewe. wewe umetafiti nini? Amesema nini kuhusu Ubungo? Jimboni Mnyika ni mtupu mimi nalijua hilo kwa kuwa Mnyika ni Mbunge wangu. Mimi nimewahi kusema hapa Mnyika aitumie Ilani ya CCM kuwakandamiza sijui hataki kuisoma? Sijasikia akiwakumbusha watekeleze ahadi lukuki za barabara za jimboni Ubungo. Akisimamia hilo na barabara zile zikatengenezwa mbona atapeta tu mwaka 2015 lakini kinyume na hapo huenda akausikia Ubunge kwenye Bomba. Nyie mdanganyeni mkidhani mnamsaidia kumbe mnampoteza ati kinara; kinara wakati jimbo lake hali inatisha? wewe umewahi kupita barabara ya Kimara Mwisho kuelekea Kisukuru/segerea? Hali inatisha. Unaijua Bonyokwa wewe, Golani je, unaifahamu Kibangu ama King'ong'o au Kilungule. Utadhani hawakupiga kura hawa.
Najua hana pesa za kuleta maji wala barabara lakini hata kelele na kuwahamasisha watu wake. Mnyika ahamasishe tu barabara zile hazihitaji pesa nyingi na watu wa kule hawana makuu wewe pata grader la manispaa watajaza mafuta lichonge barabara. Awahakikishie watu kwamba atawaletea grader la manispaa waao wajitolee mafuta watu watatoa hela za mafuta na barabara zitachongwa; watu wa huko hawalalilii lami wao wanataka passability tu.