..Mnamlaumu Mbowe na Chadema bila sababu na hamko kiuhalisia.
Simlaumu Mbowe na CDM kwa suala la Katiba kama jukumu lao, hapana! Sikubaliani nao kwa 'approach' yao
Wanachama wengi wa CDM ni ''political capital'.
Wakati wa kesi yao, Tsh Milioni 300+ zilichangwa katika masaa 24 ikiwa ni testimony kwamba wana Umma.
..Majority ya Kamati Kuu ya Chadema walifungwa jela na Magufuli.
Michango ilikuwa ni clear message kwa Watawala kwamba kuna 'resentment' katika sehemu ya Jami
..Mbowe alikwenda kwenye maridhiano kwasababu huku kitaa hakuna watu wa kukinukisha. Tusubiri kizazi kingine lakini sio hiki cha Watanzania wa sasa hivi.
Hapa ndipo ninapomuona Mbowe ana makosa. Akiwa mahabusu harakati ziliendelea tena Mahakamani.
Watu waliimba Katiba mpya mbele ya Mahakama na Polisi. Ilikuwa 'courage' isiyo ya kawaida.
Mbowe kutoka tu hata kabla ya kukutana na watu wake akaenda Ikulu, kuanzia hapo kila jambo likapooza
Mkutano wa BAWACHA Iringa Wanawake walikula mihogo chini ya miti na kuhudhira kwa gharama zao..
Siku ile Mbowe hakuwa na la kusema! kwanini alikikmbilia Ikulu kwanza. 'political blunder !
Mbowe akiwa Marekani akasema kuna 'wahafidhina' katika chama chake, hatoki katika mariadhiano
M/kiti alijua maridhiano na CCM ni ndoto. CUF na ACT wakajaribu, yeye akajaribu na Magufuli. Mara zote matokeo yalikuwa ya hovyo.
Hazikuwepo dalili za kufanikiwa, mwisho wa siku walimmwaga mzima bila chembe ya ridhiano,
Mbowe kapoteza muda kuaminisha CDM kuna jambo! hajifunzi kutokana na makosa?
2025 msimamo ni kususia chaguzi. Ghafla Mbowe anawaambia Wanachama wajiandae kwa chaguzi.
Ni kana kwamba hana kumbu kumbu za nini kilitokea 2020 au ana matumaini feki bila kujua ni feki.
Nililtegemea CDM waongoze jitihada za kususia katiba kama walivyosusia Tume ya Mkandara.
Moja ya sababu za Mbowe kutolewa ni kutaka CDM warejee katika majadiliano ya TCD.
Mara zote CDM wanaposusia Mwenyekiti wa CCM ana fura , maana yake CDM ni 'force to reckon with'
Muda uliopotea katika maridhiano ungetumika kushinikiza katiba na kueleza agenda ya kususia uchaguzi.
Inawezekana Mbowe hana mbinu mpya angejiuzulu waje wenye new ideas, ndani ya CDM wapo
Tuna mifano ya ACT na CUF walivyofeli Zanzibar, leo Mnyika anapita pale pale walipojikwaa wengine ili akaangukie pale pale. Na CCM wanajua hilo wanawasubiri waangukie pua tena. Wameleta mswada feki kama chambo
..Sikubaliani na wewe kwamba tatizo ni uongozi ktk vyama vya upinzani. Mimi nadhani Watanzania bado hatujapigika kisawasawa kiasi cha kuamua kutaka mabadiliko.
Yes ndio maana nasema CDM waache kuingia katika michakato ili Wananchi wajifunze.
Kinyume chake ni kuwapa CCM uhalali. Ni kama Zitto na ACT walivyotoa uhalali wa Tume feki ya Mkandara. iLaiti ACT, wenye nguvu visiwani wasingeshiriki Tume ya Mkandara, tungelikuwa pengine leo hii.
Hivyo, badala ya kwenda uchaguzi wa serikali za mitaa au uchaguzi mkuu na mabadiliko feki ni afadhali CDM wakatae ili wananchi wapigike na kupitia hilo watafunguka.
In fact haya tunayoyaona ya Bandari ni kutokana na ukweli kwamba 2020 ilikuwa dhahma , Wananchi wanajua hilo ndio maana wanaunga mkono makundi tofauti yenye misimamo mikali na si maridhiano feki
..Vilevile sikubaliani na wewe kwamba Cdm ndio watetezi wa kukosekana kwa muda wa kuleta Katiba mpya btn now and 2025.
Mnyika kasema muda hautoshi akiakisi kauli ya Mbowe ya siku za nyuma akiwa kanda ya Ziwa.
Waliopaswa kutumia 'muda' ni Wahuni wa CCM , siyo Chadema !
..Nadhani wanaoilaumu Cdm kuhusu kuchelewa kwa Katiba Mpya ni watu waoga wasiotaka kukabiliana na Ccm.
..Katiba imekwamishwa na Ccm. Kuwalaumu Chadema ni kujifanya vichwa maji.
Ni kweli CCM ilivuruga mchakato na haina nia njema, tulishangaa Mbowe kukaa nao meza moja.
Sijui Mbowe alitegemea maua ya aina gani. Hawa CCM ni Wahuni wazoefu haifai kukaa nao mezani.
Mkao na CCM ni haramu na kujI najisi, kama Mbowe alivyo '' jinajisi'' kwa maridhiano
CDM wana option, kwamba, wajifiche nyuma, mambo yatokee yenyewe kimiujiza au Watangulie ili kujenga imani kwamba ni mbadala. Kuchukua ruzuku za kazi za siasa halafu kukwepa majukumu ya siasa ni kujitweza.
Wananchi wanapokubaliana na sauti ya Watanzania badala ya Chama kikuu cha upinzani , ni wake up call.