MNYIKA: Katiba mpya 2025 tumechelewa

MNYIKA: Katiba mpya 2025 tumechelewa

..Mnamlaumu Mbowe na Chadema bila sababu na hamko kiuhalisia.

..Majority ya Kamati Kuu ya Chadema walifungwa jela na Magufuli.

..Kwenye nchi zenye wananchi wanaojitambua serikali haiwezi kufanya uhuni wa kufunga wapinzani na wananchi wakakubali kama ilivyotokea kwa Mbowe na wenzake.

..Mbowe alikwenda kwenye maridhiano kwasababu huku kitaa hakuna watu wa kukinukisha. Tusubiri kizazi kingine lakini sio hiki cha Watanzania wa sasa hivi.

..Sikubaliani na wewe kwamba tatizo ni uongozi ktk vyama vya upinzani. Mimi nadhani Watanzania bado hatujapigika kisawasawa kiasi cha kuamua kutaka mabadiliko.

..Vilevile sikubaliani na wewe kwamba Cdm ndio watetezi wa kukosekana kwa muda wa kuleta Katiba mpya btn now and 2025.

..Nadhani wanaoilaumu Cdm kuhusu kuchelewa kwa Katiba Mpya ni watu waoga wasiotaka kukabiliana na Ccm.

..Jambo lingine ni Watanzania kupenda kutengeneza our own fake reality na kujifanya hatuoni tatizo, au kusukumia lawama kwa wasiohusika na tatizo.

..Katiba imekwamishwa na Ccm. Kuwalaumu Chadema ni kujifanya vichwa maji.
Mkuu nakuunga mkono asilimia 100%. Umefanya uchambuzi usio pindisha ukweli.
 
Zitto alishawaambia mpiganie kwanza tume huru ya uchaguzi mkaishia kumtukana leo hii bila aibu mnakiri katiba kwa sasa haiwezekani!!... nani aliwaloga CHADEMA? Au mlidhani wabunge wenu 19 wa viti maalum na mmoja wa kuchaguliwa ndo wangeweza kuwasaidia kwenye kupata katiba mpya?
Unapokuwa fundi kulaumu wapinzani Wakati mchezo wote mchafu unafanywa na ccm nakuona. Umepungua ama kwa makusudi au kwa kukosa weledi.Nyinyi ndio mnatufanya tukose umeme mpaka Karne hii
 
Kwa kweli hili neno hata Mimi limenishangaza sana. Huku kuchelewa ni Kwa kipimo Cha nani? Kuchelewa Kwa wao kwenda kwenye uchaguzi Kwa Katiba hii wanayoilalamikia kuwa ni ya kuibakiza CCM madarakani?
 
Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo ametoa kauli Jana kuwa mchakato wa kupata katiba mpya tayari jambo Hilo haliwezekani ! Ameomba kufanyike marekebisho yenye tija kwenye tume ya uchaguzi.

Mimi nachojiuliza MNYIKA anaposema tumechelewa anamaanisha yeye ndiye aliyechelewesha mchakato huo mbona anatamka maneno ya jumlajumla.


Ndugu zangu hivi vyama vya upinzani tunavyoamini tuviangalie kwa undani Zaidi kuna watu wanaamini kwamba hivi vyama vinaweza kuiondoa ccm kwenye box la Kura la hasha Hilo halitokuja kuwezekana Kwani vyama hivi ni vivuli kuwa Tanzania kuna upinzani , upinzani wa Tanzania ni kiini macho kuna watu wananeemeka kwa kuhadaa wananchi kuwa wanakosoa serikali.huku mlango wa nyuma wakila donge Nono la keki ya taifa.
Anachosema ni ukweli mchakato wa katiba ni process ndefu hivyo kwa muda uliobaki si rahisi kupata katiba lkn nashangaa humu ndani kuna watu bado vichwa vyao ni vigumu
 
Sikilizeni, alichokifanya Zitto si sawa.

Kwanza, alishiriki tume ya Mkandara akijua kabisa ulikuwa ni ulaghai wa kutafuta namna ya kufuta maoni ya Tume ya Warioba. Zitto alijua hilo lakini akaingia katika mchakato haramu kwasababu binafasi. Yes ni binafasi kwakuwa;
1. Rasimu ya Warioba ndio ilibeba maoni halali ya Watanzania. Hii ya Mkandara ilikuwa ya nini?
2. Zitto anajua ACT ambayo ni CUF ilikuwa katika GNU na kuwa na Tume huru. Matokeo yake tunayajua na Marehemu Jecha ameondoka na kuwaachia majonzi. Sababu za Tume huru ya CUF a.k.a ACT ya wakati huo kufeli ni Katiba
3. Huwezi kubadilisha vifungu vya Tume ya Uchaguzi bila kufumua vifungu vya Katiba. Nilipomuona ameenda Bungeni kushangilia mswada nilimshangaa sana, yaani ni kama 'amateur' Huwezi kuwa na Tume huru wakati Rais akiwa na nguvu juu ya tume hiyo

Hata hivyo Zitto anasukumwa na ACT Wazalendo waliofeli mara nyingi Zanzibar na kukubali nusu mkate.
Lakini madhara yake ni makubwa, ushiriki wa Zitto tume ya Mkandara ulitoa uhalali wa haramu hiyo.
Laiti asingeshiriki tusingekuwa na haya ya leo, akaunga mkono kwasababu tusizozijua. Ni felia tu kama hawa akina Mnyika
CHADEMA muelewe kuwa rasimu sio katiba. Wengi wenu mnalazimisha kuwa rasimu ya Warioba ipite kama ilivyo kitu ambacho ni kinyume na sheria ya mabadiliko ya katiba. Rasimu ya Warioba lazima ijadiliwe na bunge la mabadiliko ya katiba ili ipatikane katiba pendekezwa ambayo wananchi tutaipigia kura. Hii kulazimisha kuwa Rasimu ya Warioba ndo katiba ni jambo la kushangaza kwa taasisi kubwa kama CHADEMA
 
Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo ametoa kauli Jana kuwa mchakato wa kupata katiba mpya tayari jambo Hilo haliwezekani ! Ameomba kufanyike marekebisho yenye tija kwenye tume ya uchaguzi.

Mimi nachojiuliza MNYIKA anaposema tumechelewa anamaanisha yeye ndiye aliyechelewesha mchakato huo mbona anatamka maneno ya jumlajumla.


Ndugu zangu hivi vyama vya upinzani tunavyoamini tuviangalie kwa undani Zaidi kuna watu wanaamini kwamba hivi vyama vinaweza kuiondoa ccm kwenye box la Kura la hasha Hilo halitokuja kuwezekana Kwani vyama hivi ni vivuli kuwa Tanzania kuna upinzani , upinzani wa Tanzania ni kiini macho kuna watu wananeemeka kwa kuhadaa wananchi kuwa wanakosoa serikali.huku mlango wa nyuma wakila donge Nono la keki ya taifa.
Takwa la katiba mpya kutoka vyama vya upinzani limeanza lini?Mbona mnalaumu kama msio na kumbukumbu na kama mnazo mbona hamlaumu mamlaka kukalia kimya matakwa ya wananchi ya kuandikwa katiba mpya?
 
Back
Top Bottom