Mnyika kalisahau jimbo lake la Kibamba

Mnyika kalisahau jimbo lake la Kibamba

Wewe unaesema mkazi wa kibamba huyu diwani unamfahamu au hata kumsikia

Mimi ni mkazi wa Jimbo la Kibamba kata ya Msumi, huyo Diwani hanihusu, kazi zake za katani kwake ni kwa ajili ya wakazi wa kata yake, mimi nalia na Mbunge wangu wa Jimbo la Kibamba.
 
Jimbo la Kibamba lina kata sita, kuwa specific kwamba hiyo ilikuwa kata gani, madawati mangapi.

Nini kimefanyika kwenye kata zingine au
hakuna huo uhitaji? BTW, kazi ya mbunge siyo kugawa madawati, ni kuhimiza serikali itimize wajibu wake wa kugawa madawati kwa kila shule.
Nawe usiwe mgumu kuelewa ni Kata ya Kibamba ambako inaongozwa na Mgawe Ernest...hapohapo unakiri kibamba ina kata sita na utekelezaji wa kila kata siyo wa kukurupuka lazima awe na mipango na unavyodai hajawawakilisha wananchi utadhani ulikuwa huelewi yaliyokuwa yakiendelea bungeni hasa kwa wale wa kambi ya upinzani..watu wa Kibamba wamepata mtu makini na changamoto zipo kila sehemu..bunge la mwezi wa 9 ataendelea kuwawakilisha jimbo la Kibamba
 
Mimi ni mkazi wa Jimbo la Kibamba kata ya Msumi, huyo Diwani hanihusu, kazi zake za katani kwake ni kwa ajili ya wakazi wa kata yake, mimi nalia na Mbunge wangu wa Jimbo la Kibamba.
Kumbe upo kata ya Msumi anza kwanza kumlaumu diwani wako halafu uje kwa Mbunge wako,ndomana nikakuuliza wewe ni msemaji wa jimbo la kibamba..atafika kata zote kama unavyotaka wewe
 
Nawe usiwe mgumu kuelewa ni Kata ya Kibamba ambako inaongozwa na Mgawe Ernest...hapohapo unakiri kibamba ina kata sita na utekelezaji wa kila kata siyo wa kukurupuka lazima awe na mipango na unavyodai hajawawakilisha wananchi utadhani ulikuwa huelewi yaliyokuwa yakiendelea bungeni hasa kwa wale wa kambi ya upinzani..watu wa Kibamba wamepata mtu makini na changamoto zipo kila sehemu..bunge la mwezi wa 9 ataendelea kuwawakilisha jimbo la Kibamba

Mkuu labda wewe ni mtu wake wa karibu, ninategemea ukamshauri haya tunayoyaandika humu, siyo uzushi, yanayozungumzwa kwenye vijiwe vya kahawa, kwenye daladala za kwetu huko shamba, kwenye mikusanyiko yoyote ile ni juu ya Mnyika kutoonekana na kutojua nini kinaendelea juu yake.

Mara ngapi tumeawaona kina Prof Jay, Sugu, Zitto wako majimboni kwao, kama hujaingia bungeni njoo jimboni kaa na wananchi, waeleze nini kinaendelea kule, hawa hawa wananchi utakuja baadae kuwaomba kura wakati walikupa ukakimbia?

Mshauri jamaa asipotee sana, tunauhitaji mchango wake na nina uhakika hata yeye anazihitaji kiura zetu.
 
Kumbe upo kata ya Msumi anza kwanza kumlaumu diwani wako halafu uje kwa Mbunge wako,ndomana nikakuuliza wewe ni msemaji wa jimbo la kibamba..atafika kata zote kama unavyotaka wewe

Diwani anafanya part yake, mimi ninamzungumzia Mbunge.

Diwani tunakaa naye vikao mbalimbali, ila huyu mbunge ndiye hatumwoni wala kumsikia.

Na ukumbuke kitu kimoja, Diwani siyo Mwakilishi wa Mbunge kusema kwamba kama akitekeleza majukumu yake basi mbunge naye kafanya.
 
Mimi ni Mkazi wa jimbo la Kibamba, nilimpigia kura yangu Mh Mnyika bila hata ya kuzisikia sera zake, ni moja ya wabunge vijana niliokuwa nina imani nao sana sana hasa kutokana na michango yake bungeni (Bunge lililopita), harakazi zake za kisiasa akishirikiana na wenzake kipindi hicho kabla Chadema haijamkaribisha Lowassa.

Kiukweli toka Bunge hili jipya lilivyoanza kumekuwa na tetesi mbali mbali juu mwenendo wa Mh Mnyika kisiasa, wengine wakisema hashirikiani na wenzake kwa sababu hajamkubali EL, anataka kujitoa kwenye chama etc etc, huku yeye akiwa kimya.

Sasa basi toka tumemchagua Mnyika, hajawahi hata siku moja kuja jimboni either kutoa shukran kwa kura alizopewa, au hata kuhudhuria vikao vya madiwani, kufanya mikutano ya kisiasa jimboni, kufanya mikutano na wananchi wakamweleza kero zao ili angalau hata akazisemee Bungeni.

Mnyika ni wakati sasa wa kubadilika kama kweli anataka maisha yake ya kisiasa yaendelee, au ampishe mtu mwingine anayetaka kuwawakilisha wananchi Bungeni.

Mnyika popote ulipo, fanya shughuli za chama lakini kumbuka wananchi waliokuchagua ukawawakilishe, haututendei haki, sitaki kujuta kwa kutompa Dr Fenella Mkangara (CCM), lakini ninaamini kwa mwenendo huu watu tutaanza kujiuliza mara mbili mbili juu ya kama tulipoteza kura au la!
Tatizo la Mnyika hana washauri,washauri wake ni mdogo wake na vijana wa mtaani wengine redbrigade ambao maisha yameshawashinda na hawana mbele wala nyuma yaani ni wachumia tumbo pamoja na wazee wachumia tumbo wa chadema,hana jopo zuri la washauri asipojiangalia ataondoka ktk ulimwengu wa siasa na akumbuke aliondoka ubungo baada ya kuona upepo c mzuri,hasa na huko alikokwenda ajiangalie lisemwalo lipo kama halipo basi laja
 
Kuna thread zingine yaani miezi 8,lawama kibao.hauoni hali siasa nchini?
 
Kuna thread zingine ni ovyo kabisa..!buku saba inakuhusu.yaani miezi 8,lawama kibao.hauoni hali siasa nchini?

Mkuu hivi kuja Jimboni kutoa shukrani kwa kuchaguliwa inahitaji miezi mingapi?

Sugu, Zitto, Profesa Jay, na wengineo tunaowaona majimboni wao wana miezi tofauti na Mnyika?

Tunazungumzia kuja kuongea na wananchi, kuzisikiliza kero zao, kuwasilisha kero hizo kwa serikali kupitia Bunge.
 
Mkuu labda wewe ni mtu wake wa karibu, ninategemea ukamshauri haya tunayoyaandika humu, siyo uzushi, yanayozungumzwa kwenye vijiwe vya kahawa, kwenye daladala za kwetu huko
shamba, kwenye mikusanyiko yoyote ile ni juu ya Mnyika kutoonekana na kutojua nini kinaendelea juu yake.
Mara ngapi tumeawaona kina Prof Jay, Sugu, Zitto wako majimboni kwao, kama hujaingia bungeni njoo jimboni kaa na wananchi, waeleze nini kinaendelea kule, hawa hawa wananchi utakuja baadae kuwaomba kura
wakati walikupa ukakimbia?
Mshauri jamaa asipotee sana, tunauhitaji mchango wake na nina uhakika hata yeye anazihitaji kiura zetu.
Haya Mkazi wa Msumi atafika mpaka huko kwenu mana Mnyika hana makuu ni mtu wa watu
 
Tatizo la Mnyika hana washauri,washauri wake ni mdogo wake na vijana wa mtaani wengine redbrigade ambao maisha yameshawashinda na hawana mbele wala nyuma yaani ni wachumia tumbo pamoja na wazee wachumia tumbo wa
chadema,hana jopo zuri la washauri asipojiangalia ataondoka ktk ulimwengu wa siasa na akumbuke aliondoka ubungo baada ya kuona upepo c mzuri,hasa na huko
alikokwenda ajiangalie lisemwalo lipo kama halipo basi laja
Wewe unaewasema wenzio una mchango gani katika taifa hili au ni betri inayohitaji kuchajiwa na kuwekwa juani?
 
Haya Mkazi wa Msumi atafika mpaka huko kwenu mana Mnyika hana makuu ni mtu wa watu

Ha ha ha, naendelea kusisitiza kwamba kama kweli wewe ni mtu wake wa karibu mwambie kupotea kunapoteza kura. Habari za yeye kuwa mtu wa watu huku majukumu yake hatekelezi ni sifuri.

Aliomba kuwawakilisha wananchi, amechaguliwa, sasa anatakiwa kuwawakilisha kweli na siyo kutega. Bahati nzuri jimbo lake anaweza hata kulimaliza ndani ya siku mbili tu, achana na watu ambao majimbo yao yako masafa huko na bado wanahudhuria.
 
Mimi ni Mkazi wa jimbo la Kibamba, nilimpigia kura yangu Mh Mnyika bila hata ya kuzisikia sera zake, ni moja ya wabunge vijana niliokuwa nina imani nao sana sana hasa kutokana na michango yake bungeni (Bunge lililopita), harakazi zake za kisiasa akishirikiana na wenzake kipindi hicho kabla Chadema haijamkaribisha Lowassa.

Kiukweli toka Bunge hili jipya lilivyoanza kumekuwa na tetesi mbali mbali juu mwenendo wa Mh Mnyika kisiasa, wengine wakisema hashirikiani na wenzake kwa sababu hajamkubali EL, anataka kujitoa kwenye chama etc etc, huku yeye akiwa kimya.

Sasa basi toka tumemchagua Mnyika, hajawahi hata siku moja kuja jimboni either kutoa shukran kwa kura alizopewa, au hata kuhudhuria vikao vya madiwani, kufanya mikutano ya kisiasa jimboni, kufanya mikutano na wananchi wakamweleza kero zao ili angalau hata akazisemee Bungeni.

Mnyika ni wakati sasa wa kubadilika kama kweli anataka maisha yake ya kisiasa yaendelee, au ampishe mtu mwingine anayetaka kuwawakilisha wananchi Bungeni.

Mnyika popote ulipo, fanya shughuli za chama lakini kumbuka wananchi waliokuchagua ukawawakilishe, haututendei haki, sitaki kujuta kwa kutompa Dr Fenella Mkangara (CCM), lakini ninaamini kwa mwenendo huu watu tutaanza kujiuliza mara mbili mbili juu ya kama tulipoteza kura au la!
Sisi wana KIBAMBA tumemruhusu aendelee na shughuli zake
 
Wewe unaewasema wenzio una mchango gani katika taifa hili au ni betri inayohitaji kuchajiwa na kuwekwa juani?

Mkuu ninalipa mamilioni ya kodi kila mwaka, ndo maana ninamlilia mbunge aje jimboni tumweleze kutupelekea kero zetu kwa hao wanaokusanya kodi kwa ahadi ya kutupa maisha bora.

Hata hivyo mimi sijaenda kwa wananchi kuwaambia nitawawakilisha, yeye mbunge ana hilo jukumu, ni moja ya kazi zake.
 
Mmawia,

Kibamba ni kata moja, kuna kata zingine tano atazihitaji kwenye kura! Unakumbuka Kikwete aliwahi kusema hazihitaji kura za wafanyakazi? Unakumbuka nini kilitaka kutokea?

Kama unakumbuka hizi kauli utaachana nazo.
 
Mimi ni Mkazi wa jimbo la Kibamba, nilimpigia kura yangu Mh Mnyika bila hata ya kuzisikia sera zake, ni moja ya wabunge vijana niliokuwa nina imani nao sana sana hasa kutokana na michango yake bungeni (Bunge lililopita), harakazi zake za kisiasa akishirikiana na wenzake kipindi hicho kabla Chadema haijamkaribisha Lowassa.

Kiukweli toka Bunge hili jipya lilivyoanza kumekuwa na tetesi mbali mbali juu mwenendo wa Mh Mnyika kisiasa, wengine wakisema hashirikiani na wenzake kwa sababu hajamkubali EL, anataka kujitoa kwenye chama etc etc, huku yeye akiwa kimya.

Sasa basi toka tumemchagua Mnyika, hajawahi hata siku moja kuja jimboni either kutoa shukran kwa kura alizopewa, au hata kuhudhuria vikao vya madiwani, kufanya mikutano ya kisiasa jimboni, kufanya mikutano na wananchi wakamweleza kero zao ili angalau hata akazisemee Bungeni.

Mnyika ni wakati sasa wa kubadilika kama kweli anataka maisha yake ya kisiasa yaendelee, au ampishe mtu mwingine anayetaka kuwawakilisha wananchi Bungeni.

Mnyika popote ulipo, fanya shughuli za chama lakini kumbuka wananchi waliokuchagua ukawawakilishe, haututendei haki, sitaki kujuta kwa kutompa Dr Fenella Mkangara (CCM), lakini ninaamini kwa mwenendo huu watu tutaanza kujiuliza mara mbili mbili juu ya kama tulipoteza kura au la!
Akili zako changanya na za kuambiwa, Mnyika yuko ktk mgomo, hajawahi kumkubali Monduli.
 
Mkuu ninalipa mamilioni ya kodi kila mwaka, ndo maana ninamlilia mbunge aje jimboni tumweleze kutupelekea kero zetu kwa hao wanaokusanya kodi kwa ahadi ya kutupa maisha bora.
Hata hivyo mimi sijaenda kwa wananchi kuwaambia nitawawakilisha, yeye mbunge ana hilo jukumu, ni moja ya kazi zake.
Hiyo comment ilimhusu huyo kijana hapo juu anaesema Mnyika mshauri wake ni mdogo ake na redbrigede ila naona umeamua kumjibia
 
Mkuu mimi ni mpiga kura, Mnyika nimemchagua bila kushurutishwa na mtu, ni imani niliyokuwa nayo kwake, leo hii hakanyagi jimboni hata kidogo?

Wakati wa Kampeni Mnyika alipanga nyumba Mbezi, barabara ya kwenda Malamba Mawili, uchaguzi ulivyoisha tu akaondoka na hakurudi tena, unadhani tunajisikiaje? Kwa nini tu tusinung'unike? Huhitaji kuwa msemaji wa wananchi, mimi nimelalamika kama mimi.
Wewe ulimchagua fenela mkangala
 
Back
Top Bottom