Nimemsoma mbunge wangu JJ Mnyika akihamasisha kupitia gazetini watu wachangie mfuko wa ukarabati wa barabara za mavurunza na bonyokwa na kwamba yeyebkeshakabidhi mchango wake kwa diwani wa kimara. Kwanza nampongeza kwa kusikia kilio chetu na kuwakwepa wanafiki waliokuwa wanamtetea kiuongouongo kwa sababu tu ya ushabiki wa kisiasa na kiitikadi. Kwa wazo hili sasa angalau nafuu ya miundombinu itakuwepo.
Tatizo ninaloliona hapa ni kile kitendo cha kutangaza harambee hii kupitia gazetini badala ya kuja jimboni, kuitisha mikutano na wananchi ambao nina hakika wana mengi ya kumwambia na kumshauri na hapo hapo michango inayohitajika ingepatikana. Angekuwa pia ameua ndege wengi kwa jiwe moja kwani hiyo ingekuwa pia ni fursa ya kukutana na wananchi wake, wamsikie na yeye awasikie. Sasa kazi ya kupitishia mchango kwa diwani ambaye naye hafahamiki kwa vile haonekani ni ngumu kidogo.
Hata hivyo tunakushukuru kwa kuuona mwanga!