Mnyika hilo sawa lakini .........

Kiswigo

Member
Aug 9, 2012
56
22
Nimemsoma mbunge wangu JJ Mnyika akihamasisha kupitia gazetini watu wachangie mfuko wa ukarabati wa barabara za mavurunza na bonyokwa na kwamba yeyebkeshakabidhi mchango wake kwa diwani wa kimara. Kwanza nampongeza kwa kusikia kilio chetu na kuwakwepa wanafiki waliokuwa wanamtetea kiuongouongo kwa sababu tu ya ushabiki wa kisiasa na kiitikadi. Kwa wazo hili sasa angalau nafuu ya miundombinu itakuwepo.

Tatizo ninaloliona hapa ni kile kitendo cha kutangaza harambee hii kupitia gazetini badala ya kuja jimboni, kuitisha mikutano na wananchi ambao nina hakika wana mengi ya kumwambia na kumshauri na hapo hapo michango inayohitajika ingepatikana. Angekuwa pia ameua ndege wengi kwa jiwe moja kwani hiyo ingekuwa pia ni fursa ya kukutana na wananchi wake, wamsikie na yeye awasikie. Sasa kazi ya kupitishia mchango kwa diwani ambaye naye hafahamiki kwa vile haonekani ni ngumu kidogo.

Hata hivyo tunakushukuru kwa kuuona mwanga!
 
Nimepita Bonyokwa juzi nikienda kuona mgonjwa. Yale si makorongo bali ni balaa mpaka unajiuliza kama eneo lile lina mwakilishi wa wananchi. Mawe yanayotishia kutoboa tairi ni kama mikuki. Mnyika hebu waonee huruma wenzio wanateseka sana!
 
Ni mapema sana kumsifia maana kukitokea suala la M4C Karagwe anaweza kukimbilia huko akawaacha mkishangaa. Nimecheka kusoma stori hiyo, naye akijigamba kutoa laki 2.
 
Napata fikra kwamba huyu bwana mdogo jimbo linamshinda na inawezekqna majukumu haya ni makubwa sana kwake na sasa yanamuelemea. Na hili ndilo linalowatokea wabunge wengi sana waliongia madarakani kwa euphoria na hasira za wananchi kwa chama tawala.
 
Hiki mnachokiona ni rasharasha tu, wakipewa madaraka makubwa zaidi kwa staili hii tutasaga meno!
 
Kwa lipi? Maana barabara zinatengenezwa na halmashauri, sasa Mbunge anapoongeze nguvu zake kinakuuma nini?
 
wananchi wengi hudhani kuwa mbunge ndio anaetoa hela za huduma za wananchi. mbunge yeye sio decision maker yeye ni mashauri na msimamziiz tu .serikali ndio kila kitu si ajabu ukiona majimbo hata ya wabunge wa upinzani yakawa na hali mbaya zaidi kwa sababu ya kubaniwa fund na serikali ili kumshusha mbunge kisiasa. kumbe yeye anasimamia ila hawezi kuingia jikoni wanakopikia chakula .kaziyake ni kuuliza tu kama vile ,jamani njaa chakula bado tu, au wewe kula vizuri mbona unakomba mboga,au yule jamaa amekula chakula chakula peke yake kwahiyo naomba baba umchukulie hatua. mkitambua hili hamtakuwa mnawalalamikia wabunge.yeye si mtendaji. yeye ni msimamizi mshauri na mtunzi wa sheria.
 
Napata fikra kwamba huyu bwana mdogo jimbo linamshinda na inawezekqna majukumu haya ni makubwa sana kwake na sasa yanamuelemea. Na hili ndilo linalowatokea wabunge wengi sana waliongia madarakani kwa euphoria na hasira za wananchi kwa chama tawala.
Wewe ni miongoni mwa watanzania ambao hamfahamu kazi ya mbunge sasa acha tukufahamishe.Kazi ya mbunge kupeleka kelo na MALALAMIKO YA WANANCHI SERIKALINI KUPITIA VIKAO VYA BUNGE NA KWENYE ALIMASHAURI,siyo kutengeneza wala kujenga barabara mbunge ni kiunganishi kati ya wananchi na serikali yao kama unalaum ubovu wa miundombinu uilaumu serikali yako ya MAGAMBA
 
Ni mapema sana kumsifia maana kukitokea suala la M4C Karagwe anaweza kukimbilia huko akawaacha mkishangaa. Nimecheka kusoma stori hiyo, naye akijigamba kutoa laki 2.
Usishangae wabunge wa CHADEMA ni wabunge wa kitaifa,hakuna kulala mpaka kieleweke.Mtajibeba mpaka kufika 2015
 
Nimemsoma mbunge wangu JJ Mnyika akihamasisha kupitia gazetini watu wachangie mfuko wa ukarabati wa barabara za mavurunza na bonyokwa na kwamba yeyebkeshakabidhi mchango wake kwa diwani wa kimara. Kwanza nampongeza kwa kusikia kilio chetu na kuwakwepa wanafiki waliokuwa wanamtetea kiuongouongo kwa sababu tu ya ushabiki wa kisiasa na kiitikadi. Kwa wazo hili sasa angalau nafuu ya miundombinu itakuwepo.

Tatizo ninaloliona hapa ni kile kitendo cha kutangaza harambee hii kupitia gazetini badala ya kuja jimboni, kuitisha mikutano na wananchi ambao nina hakika wana mengi ya kumwambia na kumshauri na hapo hapo michango inayohitajika ingepatikana. Angekuwa pia ameua ndege wengi kwa jiwe moja kwani hiyo ingekuwa pia ni fursa ya kukutana na wananchi wake, wamsikie na yeye awasikie. Sasa kazi ya kupitishia mchango kwa diwani ambaye naye hafahamiki kwa vile haonekani ni ngumu kidogo.

Hata hivyo tunakushukuru kwa kuuona mwanga!

Amefanya maamuzi mazuri, nafikiri pia angefanya mikutano sehemu hizo na kufanya harambee ya nguvu na michango kama ambavyo wananchi walichangia kampeni za mnyika ndivyo wasivyoona tabu kuchangia maendeleo yao wenyewe, tatizo ni mipango tu mh mnyika hebu fikiria tena, kama serikali ya ccm haifanyi wananchi tunafanya wenyewe
 
Shida yenu mnafikiri mbunge kazi yake ni kutengeneza barabara au ana fedha za kutengeneza barabara. Mikutano yake ni ya uhamasishaji na kuangalia juhudi za wananchi na madiwani wao zinakwamia wapi na zinakwamishwa na nani.

Kama wananchi wanafahamu wajibu wao, anayetakiwa kusimamia shughuli za halmashauri ni diwani na endapo kuna ugumu ndio jambo hilo huripotiwa kwa mbunge ili naye akaliseme mbele.

Kesho Mh.Mnyika atakuwa katika kata ya Makuburi kuzungumza na wananchi na nyinyi jisikieni huru mkumuita endapo mna la kushirikiana naye lkn kama mnadhani itatokea siku awatembelee nyumba moja baada ya nyingine kuwasalimia na kunywa chai na wake zenu basi mmekosea kuwaza
 
Ni wakati sahihi wa kuweza kurudisha nguvu jimboni, watu wanahitaji barabara. Serikali haipo tayari kutimiza- unachotakiwa Mnyika ni kufika, fanya mikutano, fanya uchangishaji wekeni usimamizi makini ili kuhakikisha mnafikia lengo. Barabara ya Msakuzi kutokea mbezi ni tatizo jingine, kwa kuwa watu wana utayari work it out right away, do not waste more time kwa kuwa 'washtaki wako- kama joka kuu' wanatafuta kila njia wakumeze.
 
Wewe ni miongoni mwa watanzania ambao hamfahamu kazi ya mbunge sasa acha tukufahamishe.Kazi ya mbunge kupeleka kelo na MALALAMIKO YA WANANCHI SERIKALINI KUPITIA VIKAO VYA BUNGE NA KWENYE ALIMASHAURI,siyo kutengeneza wala kujenga barabara mbunge ni kiunganishi kati ya wananchi na serikali yao kama unalaum ubovu wa miundombinu uilaumu serikali yako ya MAGAMBA

Hoja finyu na isiyo na mashiko. Kama ingekuwa hivyo basi wabunge wasingeng'olewa madaraka baada ya vipindi vyao kwa madai kwamba hawakufanya lolote majimboni kwao. Hoja ya kutofanya chochote hulinganishwa kwa ahadi zao na hali mbaya na wingi wa kero majimboni. Mnyika aliahidi kutatua kero zote hizi na ndiyo maana watu wanamlalamikia. Wananchi hawataki kujua kama mbunge kapata wapi msaada as long as yale yanayohitaji kufanyika yamefanyika.

For your information, hakuna anayehitaji chochote binafsi kutoka kwake, tena kinyume chake, kwenye mikutano yake ya kampeni yeye ndiye alikuwa akiomba toka kwa wananchi na walimchangia. Wanachohitaji ni kumuona wamueleze kero zao na kupanga namna boraya kushirikiana kuzitatua na huo ndiyo uongozi. Siyo kuitisha michango kupitia magazetini as if yuko India kwa matibabu, kumbe anashinda Kinondoni. Huo ni udhaifu na anayeutetea hamtakii meme Mnyika.
 
Shida yenu mnafikiri mbunge kazi yake ni kutengeneza barabara au ana fedha za kutengeneza barabara. Mikutano yake ni ya uhamasishaji na kuangalia juhudi za wananchi na madiwani wao zinakwamia wapi na zinakwamishwa na nani.

Kama wananchi wanafahamu wajibu wao, anayetakiwa kusimamia shughuli za halmashauri ni diwani na endapo kuna ugumu ndio jambo hilo huripotiwa kwa mbunge ili naye akaliseme mbele.

Kesho Mh.Mnyika atakuwa katika kata ya Makuburi kuzungumza na wananchi na nyinyi jisikieni huru mkumuita endapo mna la kushirikiana naye lkn kama mnadhani itatokea siku awatembelee nyumba moja baada ya nyingine kuwasalimia na kunywa chai na wake zenu basi mmekosea kuwaza

Mimi napata fikra kwamba wengi wenu hamjui hii concept ya uwakilishi wa ubunge ikoje. Mnyika, kama mbunge yeyote alikuwa na platform yake aliyoitumia kushinda ubunge wake. Platform hii ndiyo mkataba wake na wale waliomchagua na, by extension, jimbo zima analoliwakilisha. Anapokuja baadae kugeuka na kudai kwamba kazi hizo siyo za mbunge ni kuvunja ahadi maana alipaswa kujua kazi za mbunge ni zipi na kuelewa kwamba anachoahidi hakipo kwenye mamlaka yake ya kiutendaji.

Kwa kesi ya jimbo la ubungo na hasa maeneo yanayolalamikiwa kuhusu miundo mbinu, wengi wa wananchi wake ni watu wenye uwezo wao na wanaomiliki magari. Hawatarajii wala kuhitaji chochote binafsi kutoka kwa Mnyika au kiongozi yeyote. Wana maisha yao mazuri tu, tena kumshinda Mnyika. Wanachohitaji ni hamasa na mamlaka yake viwaunganishe wanachi hao na kutekeleza majukumu ya kujiletea maendeleo. Ndiyo maana tunadhani huyu bwana anahitaji kulielewa hili na atashangaa atakapoona kwamba michango itakayotolewa inazidi hata kile alichokitarajia yeye.

Wachangiaji humu waache kujigeuza ngao itakayomlinda Mnyika dhidi ya constructive criticism ambayo ina lengo la kumuamsha na hata kumjenga kisiasa. Waache kumchochea usaliti dhidi ya watu walimpandisha kufika hapo. Ndiyo hawa walikuwa wakikesha pale Loyola kwa siku zote zile wakati sintofahamu ilipotanda kuhusu matokeo ya uchaguzi. Hawa wanaolalamika ndiyo wale waliombeba na kuandamana pale mahakama kuu alipombwaga Hawa Ng'umbi. Sasa kama kuna watu humu, ambao hata Dar es Salaam hawaijui wanachekelea hili wakidhani kila mkosoaji ni mwana CCM basi wajue wanajipiga risasi mguuni bila kujua.
 
Hii ndiyo shida ya kuwa na watu waliojawa na ushabiki bila kuangalia hili kwa picha pana. Mkuu Tiote umetoa shile lakini kuna vipofu hawataliona hili. Mnyika jiondoe kwenye wingu hili na tekeleza yanayokuhusu.
 
Amefanya maamuzi mazuri, nafikiri pia angefanya mikutano sehemu hizo na kufanya harambee ya nguvu na michango kama ambavyo wananchi walichangia kampeni za mnyika ndivyo wasivyoona tabu kuchangia maendeleo yao wenyewe, tatizo ni mipango tu mh mnyika hebu fikiria tena, kama serikali ya ccm haifanyi wananchi tunafanya wenyewe
Nimeyapenda maneno yako yanatia moyo kwa mtendaji.
 
Bado uelewa wako unakuwa finyu kama kukutana na wananchi kazi hiyo anaifanya isipokuwa wewe hutaki kuelewa na kazi ya mbunge ni kuunganisha watu kwa kutumia njia tofauti tofauti kulingana na teknologia zilizopo_OPEN UP YOUR MIND
Hoja finyu na isiyo na mashiko. Kama ingekuwa hivyo basi wabunge wasingeng'olewa madaraka baada ya vipindi vyao kwa madai kwamba hawakufanya lolote majimboni kwao. Hoja ya kutofanya chochote hulinganishwa kwa ahadi zao na hali mbaya na wingi wa kero majimboni. Mnyika aliahidi kutatua kero zote hizi na ndiyo maana watu wanamlalamikia. Wananchi hawataki kujua kama mbunge kapata wapi msaada as long as yale yanayohitaji kufanyika yamefanyika.

For your information, hakuna anayehitaji chochote binafsi kutoka kwake, tena kinyume chake, kwenye mikutano yake ya kampeni yeye ndiye alikuwa akiomba toka kwa wananchi na walimchangia. Wanachohitaji ni kumuona wamueleze kero zao na kupanga namna boraya kushirikiana kuzitatua na huo ndiyo uongozi. Siyo kuitisha michango kupitia magazetini as if yuko India kwa matibabu, kumbe anashinda Kinondoni. Huo ni udhaifu na anayeutetea hamtakii meme Mnyika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom