PISTO LERO
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 2,819
- 1,454
Dar es Salaam. Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla jana iliingia dosari baada ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge na Diwani wa Kata ya Kimara, Paschal Manota (Chadema), kurushiana matusi mbele ya wananchi na nusura wakunjane mashati.
Tukio hilo lilitokea jana wakati wa mkutano wa wananchi wa Kata ya Saranga, Kimara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mavurunza ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya Makalla katika ukaguzi wa miradi maji ya Dawasco.
Vurugu hizo zilitokea baada ya Makalla kuagiza polisi kuwakamata wafuasi wa Chadema kwa madai kuwa walitaka kuvuruga mkutano huo. Baada ya Makalla kutoa agizo hilo, Diwani Manota na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika walisimama na kupinga uamuzi huo na walirushiana maneno na Mwenyekiti Madenge aliyesema wawili hao waache upumbavu.
"Unatetea nini? Acha upumbavu... Hatuwezi kuendesha mkutano na watu wanaofanya vurugu," alitusi Madenge huku Manota akiwa na jazba kabla ya viongozi wengine wa kisiasa kuwatuliza.
Hata hivyo, kabla ya Makala kuzungumza, Mnyika aliyekuwa ameongozana naye katika ziara hiyo alikuwa na wakati mgumu wa kuzungumza kutokana na zomeazomea kutoka kwa wafuasi wa CCM.
Makalla alisema kosa kubwa lililosababisha kutokea kwa vurugu hizo ni maandalizi mabovu ya wafuasi wa vyama vyote.
"Wafuasi walikuwa na itikadi zao zaidi kuliko kuja kusikiliza hoja za serikali kupitia ziara. Pia labda waliwakosa uvumilivu kutokana na ahadi ya maji kuwapo kwa muda mrefu, lakini kuvurugana wanasiasa ni kukosa uvumilivu," alisema.
Kwa upande wake, Mnyika alipendekeza ziara zote za kiserikali zisiwe na uhusiano na vyama vya kisiasa.
"Kama ingekuwa ni mambo ya kuzungumzia ilani ya chama, tangu mwaka 2005/10 ahadi ya maji ya asilimia 90 kwa Jiji la Dar es Salaam haijatekelezwa," alisema Mnyika.
Chanzo: Mwananchi

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo,
Wafuasi wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mhe John Mnyika akihutubia na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia katika mkutano huo.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mhe John Mnyika (Chadema), wakitofautiana jukwaani wakati Makalla akiamuru polisi kuwatoa wafuasi wa Chadema waliokuwa wakimzomea wakati akileleza Utakelezaji wa Ilani ya CCM JUU YA MAJI, HUKU mNYIKA AKITAKA WAENDEE KUZOMEA AKIDAI KWAMBA WAZIRI HAKUFANYA HAKI KWANI YEYE ALIPOKUWA AKIZOMEWA NA WANA CCM HAKUWACHUKULIA HATUA KAMA HIYO KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA SHULE YA MAVURUNZA, KATA YA SALANGA.