Mnyika amlilia Odira Ongara


Fredrick Sanga

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Messages
3,149
Likes
22
Points
135
Fredrick Sanga

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2011
3,149 22 135
http://1.bp.blogspot.com/-tg-SMJ670...hn+Mnyika+akiaga+mwili+wa+Marehemu+Ongara.jpg

Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika ametoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Mzee Odira Elizaphan Hamathe Ongara na kumweleza Marehemu kuwa alikuwa mtu mwenye msimamo katika nafasi za uongozi na utumishi wa umma alizowahi kuzishikilia wakati wa marais watatu wa Tanzania; Nyerere, Mwinyi na Mkapa.

Mnyika alisema hayo jana (Novemba 23, 2012) wakati akihutubia waombolezaji waliojitokeza nyumbani kwa familia ya marehemu kata ya Kwembe, jimboni Ubungo. “ Nilipopata taarifa za msiba juzi, nilimtumia ujumbe mfupi wa maneno Eric (mtoto wa marehemu) akiwa Afrika Kusini kikazi kuwa asihuzunike, mzee amekwenda kupumzika baada ya kazi. Sasa majukumu yamebaki kwa vijana kwenda mbele zaidi. Na huu ni ujumbe wangu kwenu leo, tumuombee apumzike kwa amani lakini tukumbuke tunao wajibu wa kulitumikia Taifa letu na jamii yetu”.

Marehemu Odira Ongara pamoja na mambo mengine atakumbukwa kwa msimamo wake katika masuala mbalimbali nchini hususan misimamo yake katika kipindi cha utumishi serikalini.

Moja kati ya misimamo wa Mzee Ongara ambayo ni ya mfano na yenye kutoa fundisho kubwa hasa kwa watumishi wa umma katika nyadhifa mbalimbali za kiserikali na pia kisiasa ni pamoja na ule wakati wa sakata la ununuzi wa kivuko cha Kilombero akiwa Katibu Mkuu wizara ya miundo mbinu ambayo wakati kwa wakati huo ilihusika na masuala ya ujenzi na mawasiliano kati ya mwaka 1978 na 1986. Marehemu Ongara alipinga mpango wa ununuzi wa kivuko kilichotumika.

Katika kupinga hatua hiyo ya kununua kivuko kilichotumika, Marehemu Ongara alikataa kusaini nyaraka. Lakini hatimaye ununuzi huo uliidhinishwa na waziri wa wakati huo Mustapha Nyang’anyi. Kivuko hicho baadae kilikuja kuzama na kuua. Kivuko hicho kilizusha mjadala mkali hasa baada ya kuzama kwake na kuua ambapo marehemu Odira Ongara kwenye mkutano wake na vyombo vya habari alieleza wazi kuwa hakukubaliana na ununuzi huo na kuahidi kutoa nyaraka za kuonyesha aliyeidhinisha ununuzi wa kivuko hicho kilichokuwa kimekwisha kutumika. Lakini siku iliyofuata usiku wa siku aliyozungumza na waandishi wa habari wizara hiyo ikaungua moto na nyaraka mbalimbali zikateketea.

Baada ya tukio hilo, marehemu Ongara aliondolewa wizarani na kupelekwa mikoani kati ya mwaka 1986 mpaka 1996 ambapo alitumikia kama Mkurugenzi wa Maendeleo nafasi inayoshabiana na afisa tawala mikoa.

“Kwa heshima ya mzee wetu na kwa ushirikiano nanyi kwa niaba ya wananchi na marafiki, nitaambatana nanyi katika maziko kijiji cha Utegi”, alisema Mnyika.

Marehemu Odira Ongara alizaliwa mwaka 1946 na anatarajiwa kuzikwa siku ya jumapili tarehe 25 Novemba, 2012 wilayani Rorya. Marehemu amewahi kulitumikia taifa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Morogoro, Pwani, Lindi, Tanga, Tabora na mingineyo. Aliwahi kuteuliwa pia wakati wa Hayati Mwalimu Nyerere kuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha. Marehemu alikuwa sehemu ya ujumbe uliotumika na Hayati Nyerere, Ufaransa kufanya majadaliano yaliyowezesha ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa ndege wa Dar es Salaam. Marehemu alistaafu kazi katika utumishi wa umma mwaka 1996 akiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, wakati huo akiwa na umri wa miaka 50.
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,601
Likes
3,951
Points
280
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,601 3,951 280
Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema Mzalendo Ongara.

Kipindi hiki ni kigumu kwa familia yake lakini tunawaombea faraja.
 
POMPO

POMPO

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
6,691
Likes
17
Points
135
POMPO

POMPO

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
6,691 17 135
Kuna mijitu minjine ipo kwenye utumishi wa umma hata zaidi ya miaka30, lakini hakuna kitu cha kumkumbuka,
mfano Liwalo na Liwe tutamkumbuka kwa lipi? safi sana JJ kwa kuwafariji, RIP Ongara
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,601
Likes
3,951
Points
280
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,601 3,951 280
Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema Mzalendo Ongara.

Kipindi hiki ni kigumu kwa familia yake lakini tunawaombea faraja.
 
sosoliso

sosoliso

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Messages
8,145
Likes
3,448
Points
280
sosoliso

sosoliso

JF-Expert Member
Joined May 6, 2009
8,145 3,448 280
RIP mzee wetu..
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,528
Likes
11,225
Points
280
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,528 11,225 280
R.I.P... ila sijawahi kumsikia
 
N

Nawaluzwi

Member
Joined
Oct 14, 2012
Messages
20
Likes
0
Points
0
N

Nawaluzwi

Member
Joined Oct 14, 2012
20 0 0
Mungu ameto,na amempenda zaidi,ampumuzike kwa amani mzee wetu Ongara,amina
 
B

Ba'mdgo

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Messages
230
Likes
0
Points
33
B

Ba'mdgo

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2012
230 0 33
RIP MZEE, alikuwa jasiri sana huyu ni gwanda kabisa
 
Z

zamlock

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Messages
3,846
Likes
57
Points
145
Z

zamlock

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2010
3,846 57 145
poleni sana wapendwa na Mungu yuko pamoja na nyie wote mpaka safari ya mwisho pale utegi mtakapo mzika baba yetu mpendwa ongara kwenye nyumba ya mapumziko .
 
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
5,600
Likes
6
Points
135
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
5,600 6 135
#Uungwana ndo huo hata kama siyo wa chama chako unaenda kumzika huo ndo uanasiasa,
apumzike kwa amani.
 
M

Mkomawatu

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
253
Likes
75
Points
45
M

Mkomawatu

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
253 75 45
Tumuenzi kwa matendo yake mema! R.i.p mzee wetu.
 
Mikael P Aweda

Mikael P Aweda

JF Gold Member
Joined
Dec 17, 2010
Messages
2,934
Likes
40
Points
0
Mikael P Aweda

Mikael P Aweda

JF Gold Member
Joined Dec 17, 2010
2,934 40 0
Salamu zangu za pole zimwendee rafiki yangu Erick Ongara mtoto wa Marehemu pamoja na ndugu na jamaa wengine wote.
 
U

Ubungo

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2012
Messages
1,238
Likes
14
Points
0
Age
38
U

Ubungo

JF-Expert Member
Joined Apr 7, 2012
1,238 14 0
RIP Mzee wetu Odira Ongara. Poleni sana ndugu, jamaa na marafiki wote mlioguswa na msiba huu.
 
Fredrick Sanga

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Messages
3,149
Likes
22
Points
135
Fredrick Sanga

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2011
3,149 22 135
Poleni sana ndugu na jamaa.
 
BASHADA

BASHADA

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Messages
506
Likes
24
Points
35
BASHADA

BASHADA

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2011
506 24 35
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake libarikiwe. Tulishiriki msiba wake hapa Iringa siku aliyofariki na kesho yake walisafirisha kwenda Dar. Mungu awafariji wafiwa wote akiwemo dada (mdogo) wa marehemu Zilpa Nyaucho. We pray for you always, Amen
 
G

golii

Member
Joined
Nov 13, 2012
Messages
48
Likes
0
Points
0
G

golii

Member
Joined Nov 13, 2012
48 0 0
mi huyu mzee namjua vuzuri ni mzee ila alikuwa rafiki yangu. alitelekeza familia pale segerea na alioa wake watatu. mwisho wa maisha yake alikuwa tapeli mkubwa sana nna ushahidi nnaouficha ya kuwa amewahi kuwauzia eneo lake watu watatu tofauti kwa mda tofauti. Ila Busara zilikuwepo ila maisha yalikuwa yanampeleka sana. Anyaway, kila marehemu huwa anapewa sifa nzuri tuu.
 
Kaa la Moto

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
7,701
Likes
205
Points
160
Kaa la Moto

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
7,701 205 160
Mungu awatie nguvu na uvumilivu ndugu na wana wa marehemu
 
Fredrick Sanga

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Messages
3,149
Likes
22
Points
135
Fredrick Sanga

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2011
3,149 22 135
Hili ni somo, wengine watakumbukwa kwa uchafu na ufisadi. RIP
 

Forum statistics

Threads 1,273,205
Members 490,323
Posts 30,473,954