Mnyika Akalia Kuti Kavu

Katika hali ya kuchanganyikiwa na sek seke za Nchemba, Mh. Mnyika alijikuta akijiingiza matatani bure kwa kudai kwamba Nchemba naye ni mhusika wa wizi wa EPA pale BOT. Sasa Nchemba laiingia BOT 2006 na tayari wizi ulikwishatokea, na Mnyika amepewa siku 7 kutoa uthibitisho. Atafanya nini masikini kijana huyu ambaye ni kama kachanganyikiwa kabisa sasa.
Nawashauri wabunge wa CDM kuepuka kushindana na Nchemba, watajikuta pabaya sana. Huyu jamaa ni bingwa wa ku provoke watu. .Achaneni naye, mtaumia

Source: Mnyika amhusisha Nchemba na EPA

Shetani utamjua kwa maneno anayoandika
 
Kifo chako uwa kinakuwa miguu juu kisha habari yako inakuwa imekwisha! Kamanda Mnyika afundishwi uoga.Hivi Unafikiri adhabu hatakayopewa hata ikidhibitika kuwa kasema uongo(Kitu ambacho siyo kweli) itakuwa kuwa kumvua ubunge?Laaasha!
Mnyika yupo ok kama ni kuchanganyikiwa nafikiri mleta uzi ndiyo anaelekea huko

uwa= Huwa??
afundishwi= Hafundishwi??
hatakayopewa= Atakayopewa?
ikidhibitika= Ikithibitika?


Nadhani ni wazi kwamba aliyechanganyikiwa ni yupi hapa...........rudi daras la kwanza kajifunze kuandika vizuri chundu wee
 
Kifo chako uwa kinakuwa miguu juu kisha habari yako inakuwa imekwisha! Kamanda Mnyika afundishwi uoga.Hivi Unafikiri adhabu hatakayopewa hata ikidhibitika kuwa kasema uongo(Kitu ambacho siyo kweli) itakuwa kuwa kumvua ubunge?Laaasha!
Mnyika yupo ok kama ni kuchanganyikiwa nafikiri mleta uzi ndiyo anaelekea huko

Kwa hiyo ikithibitika kasema uongo kutudamganya watanzani kwa maslahi yake ya kuuza sura wewe utaendelea kumuamini?
 
Kama Chemba aliingia baada ya wizi kufanyika, nae hakusema lolote baada ya kugundua wizi huo(lazima pengo aliliona) basi nae ni mtuhumiwa mmojawapo!! Hivo kinachohitajika ni ushahudi wa kuibwa kwa pesa za EPA na Chemba kufanya kazi BOT!!‏

Rahisi sana kwa Mnyika!! ‎
Acha kuchemka wewe,, asseme nini sasa wakati yalishasemwa na wakuu walio juu yake na hata magazetini na vyombo vingine vya habari yalikuwepo. Sasa wewe unataka Nchemba aseme kama nani? acha uvivu wa kufikiri wewe!!
 
Mbona hamna subira? Tusubiri hizo siku saba zifike! Na una uhakika gani hana ushahidi?
 
Mnyika ni mtu mzima anae jitambua na ww sijui huruma zako kwake umezitoa wapi na sidhani kama alikuomba Masada.
Unadhani mpaka anazungumza alikua ajitambui! ? Alijua ataambiwa adhibitishe ndo mana akaamua aseme ili akidhibitisha tuzidi kuwafahamu wanafiki wetu .

ACHA KUKURUPUKA WEWE

Alikuwa kaniaje cha Arusha mixer kiroba si ndio akajikuta anamu attack NCHEMBA kumbe bana siyo yeye ni vitajwa hapo juu akaona auze nyago ki bongofleva bongofleva
 
Sasa Nchemba laiingia BOT 2006 na tayari wizi ulikwishatokea, na Mnyika amepewa siku 7 kutoa uthibitisho......
Hivi ccm na makampuni waliyounda wakishirikiana na mafisadi wengine kukwapua mabilioni ya EPA nao waliingia BOT mwaka gani?
 
Hilo ni tatizo lako, mimi naongelea hili tatizo alilonalo Mnyika kabla hajaanza kupashana na Nchemba.

Namuonea huruma huyu kijana na nnatumai watu wazima wenzangu wanaomzunguka (walio karibu nae) wananisoma pia na watafata ushauri japo kwa kumtazama mwenendo wake kwa umakini (ndani na nje ya bunge) wala sileti hizi mada kuhusu Mnyika kwa ajili ya kujibizana kwake Bungeni au hoja zake, la hasha, mimi naongelea afya yake.
Pambaf afya yake wewe ni daktari dhaifu mkubwa wewe unataka avimbiane Kama wabunge wa ccm ndio useme Ana afya nzuri mdini mkubwa wewe
 
Alikuwa kaniaje cha Arusha mixer kiroba si ndio akajikuta anamu attack NCHEMBA kumbe bana siyo yeye ni vitajwa hapo juu akaona auze nyago ki bongofleva bongofleva
Mnywa viroba ni huyo bongolala muchemba mwiba jina la watu hureeeeeeee
 
Katika hali ya kuchanganyikiwa na sek seke za Nchemba, Mh. Mnyika alijikuta akijiingiza matatani bure kwa kudai kwamba Nchemba naye ni mhusika wa wizi wa EPA pale BOT. Sasa Nchemba laiingia BOT 2006 na tayari wizi ulikwishatokea, na Mnyika amepewa siku 7 kutoa uthibitisho. Atafanya nini masikini kijana huyu ambaye ni kama kachanganyikiwa kabisa sasa.
Nawashauri wabunge wa CDM kuepuka kushindana na Nchemba, watajikuta pabaya sana. Huyu jamaa ni bingwa wa ku provoke watu. .Achaneni naye, mtaumia

Source: Mnyika amhusisha Nchemba na EPA

Anaweza akahusika kwa kula masalia ya EPA vilevile, Mnyika hakurupuki, lakini kwanini kila kithibitisho magamba wanaweka chini ya kapeti? watoe wazi kama wana ubavu, cku zote CDM wako makini, viva CDM
 
Usikurupuke kuandika mambo bila kufikiri vyema .Kama una uhakika kuwa walioingia kazini mwaka 2006/2007 hawakuhusika na uwizi wa fedha za EPA una haki ya kuandika hayo unayosema .Unajua fedha za EPA zilianza kuibiwa lini na kukoma lini ?Unauhakika gani kuwa fedha za EPA kuwa ziliibiwa zote mpaka kufikia 2005,uandike kuwa aliyeingia 2006 hakuzikuta?,Unajua nini maana ya Fehda za EPA? Unauhakika gani kuwa a/c ya fedha hizo ilifungwa kufikia 2005 kwa hiyo walioingia 2006 hawakuweza kutoa ama kuweka fedha kwenye a/c hiyo?

Nilichogundua ni kwamba wengi mliomsikia Mwiguli akijijitetea hakuwa mkijua nini maana ya EPA.Jua nini maana ya EPA ndio uanze kumuhukumu Mnyika kwamba alikurupuka ,ila kama hujui uliza na usubiri Mnyika atakapotoa utetezi wake ndio tumuhukumu kuwa J. Mnyika ni mtu wa kukurupuka.

Mwakalinga .Y,
Naona na wewe unajichanganya kuweka hiyo miaka, alichosema Mnyika wakati wizi wa EPA unatokea Nchemba alikuwa mtumishi wa BoT na kusisitiza ni mtuhuimiwa sio kwamba alikuta wizi wa EPA umefanyika.
 
Jionee huruma wewe mwenyewe kwa kujaribu kupandisha maji kilimani kwa gunia

Sina haja ya kubishana kuhusu hili, ni ushauri wa bure tu. Nampenda Mnyika kama kijana wa Kitanzania machachari na anajitahidi sana kufanya kazi kazi zake kwa bidii ili aonekane na ajulikane kuwa anafanya kweli, kwa hilo sina shaka amepiga hatua kali kabisa.

Kwa mapenzi ya mtu mzima kwa mwanawe, nnapotoa ushauri kama huo ujuwe nimeona kitu ambacho pengine ni kwa umri wangu tu na maisha niliyopitia yamenifanya nikione ambacho wewe na wengine wengi hamjakitilia maanani.

Sitaki kubisha kwa hili, hii si siasa, huu ni ushauri wa bure.

Ngoja nikufahamishe kitu, nna wanangu watatu ambao kila mmoja wao ni mpenzi wa chama tofauti kisiasa, kila mmoja wao ni mpenzi wa klabu tofauti za mpira za Tanzania, kila mmoja ni mpenzi wa klabu tofauti za ligi ya Uingereza. Kwa ufupi, kila mmoja anashindana na mwenzake kuwa "nani zaidi". Hivyo ndivyo walivyo, na nnawapenda sana wote ingawa wote wana tofauti zao za kiitikadi, kimchezo, kimaisha na pia na mimi tunatofautiana nao hivyo hivyo. Juu ya tofauti zetu lakini mimi bado ndio mshauri wao mkuu wa kila siku.

Jee, niwache kutoa ushauri kwa Mnyika kwa sababu tu yeye na mimi kisiasa itikadi zetu tofauti? nikifanya hivyo ntakuwa simtendei haki Mnyika wala sijitendei haki mimi binafsi.
 
uwa= Huwa??
afundishwi= Hafundishwi??
hatakayopewa= Atakayopewa?
ikidhibitika= Ikithibitika?


Nadhani ni wazi kwamba aliyechanganyikiwa ni yupi hapa...........rudi daras la kwanza kajifunze kuandika vizuri chundu wee

Ujumbe umeupata na umeelewa hayo mengine madoido tu
 
ohooooo!! huyu Mnyika mbona hivi tena? anakurupuka bila data! Hivi adhabu ya mbunge anayeshindwa kuthibisha huwa ni ipi? maana ni dhahiri shairi kwamba hapa Mnyika atashindwa kuthibitisha.
Wewe unajuaje kama hana ushahidi?na hata kama atawaletea huo ushahidi mtaufanyia kazi?je ule ushahidi wa lema dhidi ya Pinda mliufanyia kazi?nawashauri magamba mhache porojo kwani uwezo wenu ni mdogo sana na hasa katika utendaji!
 
Huyu jamaa hana adabu ,tunaweza kusema ni mtovu wa nidhamu ,tokea siku ile alivyomwita Raisi kikwete dhaifu na wengine wazembe na juzi akawaita watu machizi nilimuonea huruma sana maana amekosa uadilifu na hana ujuzi wa kuzungumza kwa ufupi hana tofauti na vijana wa vijiweni au wazee wa migahawani.

Vipi utamwita Raisi wa nchi dhaifu tena kwa jina na wengine uwaite wazembe au machizi ndani ya kikao cha bunge ,yaani huyu jamaa anavyosema ni sawa na kelele za jibwa koko tena yule asie na kwao ,anabweka tu utafikiri amekoswakoswa na jiwe.

Kuna haja ya wenziwe kumshauri na asifikirie watu wote wanamtakia wema hata wenziwe wanaweza kuwa na choyo nae na kumwacha akizama katika ujinga.

unasems hana adabu kwa sababu anawagusa wezi wa mali za Watanzania. ndani ya Uongozi wa CCM kwa sasa hakuna aliye msafi kuanzia mkubwa kabisa hadi mdogo ndio maana hakuna mwenye uwezo wa kumuwajibisha mwenzake.
Mnyika is very correct maana huyo Nchemba si ndo aliyekuwa mtunza fedha za EPA kwa niaba ya CCM wenzake? so na yeye ni Mwizi/jambazi/kibaka/mkwepuzi tu
 
Wezi wa epa ni ccm kwani ccm aliingia mwaka gan?

Halafu Mnyika asijisumbue wala nini mbona yeye hajathibitisha kwamba chadema wanahusika na mgomo wa madaktari?

Na yule mama manyanya hajathibitisha chadema kumteka ulumboka?

Hivi kuthibitisha wanathibitishaga chadema tu? mkuki kwa nguruwe binadamu mchungu eee si anataka kupakazana matope akubali kuchafuka tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom