Mnyika aishukia serikali kuibeba familia ya Kingunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika aishukia serikali kuibeba familia ya Kingunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Serayamajimbo, Dec 20, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na Hellen Ngoromera


  [​IMG]
  MKURUGENZI wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameishukia serikali kwa kuendelea kuikumbatia familia ya mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale - Mwiru, kuendelea kuipa ulaji wa kukusanya mapato katika jengo la Machinga Complex wakati ilishavurunda ilipopewa tenda ya kukusanya mapato katika kituo cha mabasi Ubungo (UBT).
  Mnyika alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki wakati alipofanya ziara ya siku mbili katika Jimbo la Ubungo Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
  Alisema mwaka 2005 wakati anagombea ubunge katika Jimbo la Ubungo aliwahi kueleza kuhusu ufisadi na upotevu wa mapato katika kituo cha mabasi Ubungo, ambao ulikuwa ukifanywa na Kampuni ya familia ya Kingunge ya Smart Holdings Company na vigogo wengine katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
  “Wakati huo, CCM wakiwamo baadhi ya vigogo hao walikanusha. Lakini miaka michache baadaye Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amekwenda na kutaka ukaguzi maalumu (Special Audit), ambao umebaini mambo ambayo nilikwisha kuyasema mwaka 2005.
  “Hata hivyo, kama kawaida ya CCM ya kulindana; Pinda mpaka sasa amekalia ripoti hiyo ya CAG. Amesubiri mkataba wa Kampuni ya familia ya Kingunge (Smart Holdings) umalizike badala ya kuvunja mkataba na kuwachukulia hatua za kisheria.
  Pamoja na hali hiyo, serikali imeendelea kuihamishia kampuni hiyo katika ulaji mwingine kwa kupewa katika mazingira tata tenda ya kukusanya mapato katika jasho la wamachinga (Machinga Complex),” alisema Mnyika.
  Sambamba na hilo, kiongozi huyo wa CHADEMA alitoa wito kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuiweka hadharani mapema iwezekanavyo ripoti ya CAG kuhusu mradi wa kukusanya mapato katika Kituo Kikuu cha UBT ili baadaye ijadiliwe na kuchukuliwa hatua zaidi.
  “Natoa wito kwa Waziri Mkuu kuiweka hadharani mapema iwezekanavyo ripoti ya CAG ili iweze kujadiliwa na umma tukiwamo wananchi wa Ubungo ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa kampuni hiyo na wana familia hao ambao walikuwa wakidanganya kuwa mapato kwa siku ni sh milioni moja na ushei; wakati serikali ilipoanza kukusanya mapato imeweza kupata takriban sh milioni nne kwa siku,” alisema Mnyika.
  Pamoja na mambo mengine, alitoa wito kwa wafanyabiashara ndogondogo wamachinga kupaza sauti kudai jengo lao kwani hata wao wanavyo vikundi na vyama vyao ambavyo vinapaswa kuhusishwa kwenye ukasanyaji huo wa mapato.
  Aliongeza kuwa changamoto iliyopo sasa ni upotoshaji unaoendelea nchini, vikiwamo vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka kuitwa kuwa unafanyika kwa masilahi ya taifa.
  “Mfano, baada ya ripoti ya UN kutolewa, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, alijitokeza na kuikana yote kwa ujumla wake kwa maelezo kwamba analinda masilahi ya taifa.
  Waziri Membe katika hali hiyo, kama kweli angetaka kulinda kikamilifu masilahi ya taifa angetangaza kufanya uchunguzi juu ya watu waliotajwa ili kutetea taswira ya Tanzania kama nchi, badala yake, kuikana ripoti nzima ni kufisha watu waliofanya vitendo haramu kwa kutumia kivuli cha masilahi ya taifa,” alisema kiongozi huyo.
  Mnyika alisema badala ya kufanya hivyo ni muhimu kwa serikali kuchukua hatua, ikiwemo kuchunguza na kuchukua hatua badala ya kubeza na kufunika, hali ambayo inaweza kuiathiri zaidi nchi katika medani ya kimataifa.
  “Ni kama ukiwa na mtaro wa uchafu, wakati mwingine unawajibika kuingia ukachafuka, ukausafisha na baadaye ukajisafisha. Tanzania itasafishwa kwa serikali kuingia katika mtaro kusafisha uchafu uliofanywa na Watanzania wachache kwa masilahi yao binafsi si ya taifa, ili nchi na Watanzania wote kwa ujumla tuweze kusafishwa mbele ya jamii ya kimataifa,” alisema Mnyika.
  Aliwashukuru wananchi wa Dar es Salaam waliokiunga mkono kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwapongeza kwa ushindi uliopatikana. Alisema hali hiyo inatia matumaini katika kuelekea katika uchaguzi wa mwakani na kwamba lazima Jiji la Dar es Salaam kiwe kitovu cha mabadiliko nchini. Aliwataka wananchi wanaoweza kujiunga ama kuichangia CHADEMA kutuma neno CHADEMA kwenda namba 15710 na kwamba ujumbe huo mfupi watakaotuma utahusisha wateja wa Zain na Vodacom
  Mnyika aliwataka wanaotaka kuwasiliana na CHADEMA Jimbo la Ubungo kutuma ujumbe au wapige simu kwenda namba 0784 222 222.
   
 2. Mgosi wa Sui

  Mgosi wa Sui Member

  #2
  Dec 20, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii kampuni haikvurunda kitu.kampuni ilingia mkataba halali na iliwasilisha kiwango walichokubaliana sasa makosa yako wapi.Kama ni kuchemsha basi ni jiji.Jiji kabla ya kutoa kazi walipaswa kufanya utafiti kujua ni kiasigani kinapatikana .Kiasi hicho ndicho walipaswa kuwataka holding ipeleke.Kweli huyu Mnyika haeliwi au anataka kujitafutia ujiko kiasaa
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  lele lele Amba!
   
 4. b

  bigilankana Senior Member

  #4
  Dec 20, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  amba na lia.....
  ambaa, eeeh eeh amba
   
 5. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi hayo yalifanyika nayo ni ya mambo ya nje? :D

  Mnyika "MKURUGENZI wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa"

  Ina maana hawa wanafamilia ya Kingunge ni ya nje?

  Sijasikia lelote kuhusu la nje...labda nje ya mtandao hoi!
   
 6. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kaongea kama aliyekuwa mgombea mwaka2005, na ni mgombea mtarajiwa wa jimbo hilo hilo la ubungo 2010,na jimbo lake ambako kampuni hiyo imefanya hayo madudu. Anazunguka kuongea na wapiga kura wake.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu Kingunge kaolea na kusomea NJE YA NCHI.
   
 8. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kingunge ameshachoka kiakili na kimwili, hana mawazo mapya anasubiri kupumzika milele!
   
Loading...