Mnyama Mbwa zaidi ya umjuavyo ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyama Mbwa zaidi ya umjuavyo !

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Judgement, Feb 17, 2012.

 1. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Jf members,
  Jana nilitoka na Trade yenye headin' "MBWA NA RANGI"
  Trade ambayo bado iko kwenye upeo wa mboni zako, na kutokana na michango niliyoipata, kwenye Thrade hiyo ikanipelekea nimtafute Mzee mmoja ambae ni maarufu sana kwa ufugaji wa Mbwa, huwafuga kibiashara, mda wowote ukihitaji Mbwa wa kununua kwake hukosi.
  Aidha mzee huyu ni mtaalamu sana wa tabia za Mbwa ( kienyeji si kisayansi).
  Nilianza na swali kumuuliza inakuaje Mbwa mara nyingi hua wanakua na ugomvi na Paka tofauti na wanyama wengine ? Mf ukibahatika kufika/kukaa kwenye mji/nyumba ifugwayo Mbwa, Paka, with other domestic animals e.g Ng'ombe , Mbuzi hata siku moja hutoona ugomvi wa Mbwa & Ng'ombe/Mbuzi
  Yafuatayo ni sehemu ya majibu ya mzee.
  "Bw mdogo Mbwa humhofia Paka kwa sababu kubwa moja, hawa wanyama mbali ya kua hupewa chakula cha kutengewa na bwn wake (anaemfuga) lakini pia wana silka ya kushambulia, shambulio lawezakua la shabaha ya adui au chakula.
  Silka hii ya kila mmoja kua fighter hufanya kila mmoja awe na wasiwasi na mwenzie.
  Aidha mara nyingi Mbwa humtisha tu Paka , na hasa Mbwa huyo akiwa yuko mmoja ndiyo kabisa hawezi mdhuru Paka.
  Ukisikia Paka kashambuliwa na Mbwa , basi fahamu Mbwa hao walikua zaidi ya mmoja.
  Mbwa atakaekua uso kwa uso hufanya kazi ya kumhadaa Paka na atakaekua nyuma ya Paka ndiyo humdhuru paka husika.
  Sababu ya Mbwa kutomshambulia Paka , pale anapokua Mbwa huyo yuko peke yake ni,
  Kwanza fahamu inasemekana Mbwa ndiyo mnyama mwenye ulimi mwembamba sana kuliko wanyama wote !
  (hapa Babu ameufananisha ulimi wa Mbwa na gazeti !)
  Hivyo Paka kutokana na maumbile yake ni mfupi kw Mbwa, anachofanya Paka ni ku'time ulimi au pua ya mbwa.
  Pua ya Mbwa ndiyo mambo yote! Ndiyo sensa , au mkonga wa mawasiliano. Na vyote hivyo Pua na Ulimi ni vilaini sana, ambavyo vikifikiwa na kucha za Paka humuachia Mbwa kilema cha maisha.
  Ukichukua kitu kama waya ngumu ukamchapa Mbwa puani anapata uchungu sana, na harufu yako wewe uliemchapa ana kitengo cha ku'store (hifadhi) harufu yako hata mwaka mzima, na siku yeyote ama ukutane nae hapatatosha, au atakubwekea hadi uondoke eneo hilo.
  Kingine kama wewe unafuga Mbwa kwako, na pakawa kuna Mbwa jike aliye kwenye (heate) mda wa kupandwa, na ukasafiri toka kwako Morogoro, ukaenda Dar, na pale utakapofikia pawe na Mbwa dume, ni lazima atakuja akunusenuse, mkongo wa mawasiliano yake utampatia tu harufu husika.
  Aidha kama wewe unafuga Mbwa kwako, na ukawa unafatana na mtu ambae hana ukaribu na Mbwa kw njia yeyote, katika tembea yenu mkakutana na Mbwa wakali, basi wewe mwenye ukaribu na Mbwa hutoshambuliwa, timbwiri litakua kwa mwenzako asiye na ukaribu na Mbwa.
  Hii inathibitisha kua mfugaji au mwenye ukaribu na Mbwa siku zote hutembea/hubaki na harufu ya Mbwa."
  Mwisho wa maelezo ya Babu.
  Labda nimalize kwa mimi binafsi katika niliyowahi kuyaona juu ya uwezo wa Mbwa, siku moja nilikua nasafiri tukiwa kwenye pori tukakutana na kundi la Ng'ombe ambapo hatukuona binadamu anaewachunga Ng'ombe wale, zaidi ya kumuona Mbwa akiwabwekea Ng'ombe hadi wote wakatoka barabarani, bus yetu ilipopita Ng'ombe wakarudi barabarani wakaendelea na safari, huku Mbwa yule akiwa anawafatia nyuma yao kama vile mtu mchungaji.
  Ni hayo tu niliyofanikiwa kuyapata kwa leo.
   
 2. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huku Mufindi Iringa kuna mzungu ana mbwa wake wanachunga kundi la mbuzi na hawawadhuru kwa namna yeyote ile.

  Ni mafunzo tu mkuu, mbwa hata sokoni waweza mtuma..
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hukumuuliza kwa nini mwanamke akiwa kwenye siku zake mbwa anamng'ata......?
   
 4. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,724
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  preta hii ya kweli?
   
 5. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  sio thrade ni thread...lol
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  huwa ana ng'ata au unataka majambos hata kama ni kwa kulamba?!!
   
 7. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Pretta ! Hiyo umenipa new changamoto, nikijapata tena wasaa ntalifanyia kazi hilo pia.
   
 8. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Nakubali Mtalingolo, then nikupe pole coz recently saa 6 kamili nilikua naangalia ITV habari kwa ufupi, imeripotiwa huko Iringa kandokando ya msitu wa Sao hill na kandoni mwa barabara kuu iendayo Mafinga kumenyesha mvua iliyoacha theluji nyingi maeneo hayo. Na baadhi ya picha zimechukuliwa kuonesha tukio hilo ni theluji kibao kama vile tuonavyo kwenye nchi za Uropa (Ulaya)
  wakazi waliohojiwa wamethibitisha kutowahi kuona hapo kabla, tukio kama hilo.
  Mtalingolo karibu Lake Victoria
  Karibu Rock City
  Karibu Mwanza.
   
 9. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,064
  Likes Received: 1,200
  Trophy Points: 280
  hahaahaha..Sikia hii..Kisa cha Mbwa na Paka

  Hapo zamani mbwa alikua rafiki na paka na wote walikua wanaishi kwa binadamu..sasa siku moja paka alinyimwa chakula kwasababu ya tabia yake ya udokozi...paka akakasirika sana...

  siku moja alienda kutembea porini akakuatana na simba na chui..na kwakua wote ni jamii moja...basi simba na chui wakamuuliza paka ebwana eeh sisi tuna njaa inakuaje....pale kwenu hakuna msosi?...paka akajibu upo mwingi tu mimi na mbwa mbona tunakula kila siku...simba na chui wakasema ila sisi hawezi kutupa kwanza tunamuogopa...paka akasema yaani nyie na ukubwa wote huo mnamuogopa Binadamu?..wakati mimi yule nacheza naye na muda mwingine anipakata...hana lolote yule mbona...simba na chui wakauliza kweli akawathibitishia kua ni kweli

  basi bwana siku simba akamnyemelea Binadamu wakati huo mbwa kafungiwa katika banda na paka yeye anaranda randa tu pale nyumba....simba akafanikiwa kumla binadamu sehemu ya mwili wake binadamu alilia sana kwa maumivu mbwa naye akafoka sana lkn alikua bandani

  Baada ya siku tatu ikagundulika kuwa Paka alimsaliti Binadamu ..ndio maana simba akamjeruhi..mbwa alikasirika sana na akamfokea sana paka kwa tabia yake mbaya ya kumsaliti binadamu ambaye huwapa chakula kila siku

  Natoka siku hiyo paka na mbwa maadui...

  Hii niliisikia TBC kipindi cha watoto..mama anawahadithia
   
 10. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  sijajua mbwa huwa anagundua nini.......lakini hali ndio huwa inakuwa hivyo.........

   
 11. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Mbwa pia ni mgunduzi wa style pendwa ya mambo flani maarufu kama dog style!
   
 12. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Duuuh nashukuru mkuu, huku kwetu ni kawaida sana kukuta nguo uliyoianika jana usiku ikiwa imeganda kwa baridi, bt hali ya jana na juzi kuwepo kwa theruji kabisa imetuhamakisha wengi sana...

  M/mungu akijaalia nadhani ntafika tu pande hzo coz mie ni kijana na sina family so ktk utafutaji naweza fika huko mahali(inshaallah), nawe pia karibu ushuhudie maajabu ya baridi
   
Loading...