Mnigeria ashinda shindano la urembo la kiisilamu

Mnigeria ashinda shindano la urembo la kiisilamu

Texas Tom.

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2013
Posts
510
Reaction score
273
View attachment 112572 548824-130919-indonesia-muslim-pageant.jpgimages.jpg




Mwanadada wa Nigeria ndiye mshindi wa shindano la urembo kwa wasichana wa kiisilamu mjini Jakarta Indonesia.
Obabiyi Aishah Ajibola, 21, alishinda shindano la kimataifa la wasichana wa kiisilamu kwa jina Muslimah mwaka 2013 siku ya Jumatano.



Washindani 20 walishiriki mashindano hayo kuonyesha mitindo ya kiisilamu pamoja na maadili ya kiisilamu wakati wa mashindano hayo.

Mashindano yalifanyika kabla ya shindano kubwa zaidi la mwanamke mrembo zaidi duniani, ambalo limeghadhabisha makundi ya watu wenye msimamo mkali nchini Indonesaia kwa kutaka kuandaliwa huko.
Waliofuzu kwa fainali ya mashindano hayo, walichaguliwa kutoka miongoni mwa watu 500 waliochaguliwa kwa kutumia njia ya mtandao.
Moja ya vikwazo vya kuruhusiwa kushirki kwenye mashindano ilikuwa kusimulia kisa chako na ambavyo ulianza kuvalia Hijab au mtandio, ambacho kilikuwa kikwazo kwa wote waliotaka kushiriki.
Washiriki walitoka Bangladesh, Iran, Malaysia, Nigeria na Brunei.
Kabla ya fainali, washindani walihitajika kuamuka kwa sala ya asubuhi na kuswali pamoja huku wakijifunza kusoma Koran.
Bi Ajibola, mwenye umri wa miaka 21, alilia na kusoma aya kutoka kwa Korani, jina lake lilipotajwa. Alituzwa dola 2,200, pamoja na ziara ya mji mtukufu wa Mecca na nchini India.
Kabla ya kushinda alisema kuwa nia yake ya kushiriki mashindano hayo ilikuwa tu kuonyesha dunia nzima kuwa dini ya kiisilamu ni nzuri sana.
Eka Shanti, aliyefutwa kazi kwenye televisheni kwa kukataa kuvua mtandio wake, ndiye alianzisha shindano hilo miaka mitatu iliyopita.
Aliambia shirika la habari la Agence France-Presse kuwa walifanya shindano hili siku chache kabla ya shindano la kimataifa la mwanamke mrembo zaidi duniani kuonyesha wasichana kuwa kuna njia zengine tofauti ambazo unaweza kuwa mrembo.
Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa ya waisilamu duniani.
BBC
 
Naomba kuuliza; hivi kuna imani inayoshabikia huu upuuzi wa miss this miss that? Isije ikawa watu wanachukua imani ki-enyeji na kufanya mambo ya ki-dunia kwa mzaha.
 
Swali lipi hp na unaona jibu hilo "shindano la kimataifa la wasichana wa kiisilamu kwa jina Muslimah mwaka 2013"au uko darasa gani?
 
Swali lipi hp na unaona jibu hilo "shindano la kimataifa la wasichana wa kiisilamu kwa jina Muslimah mwaka 2013"au uko darasa gani?

Kingtom kutumia jina la imani fulani haina maana hilo shindano liko sanctioned na imani husika. Wewe hujawahi kuona watu wanavaa kama watawa na kuigiza filamu za ngono (unafikiri kanisa katoliki limeridhia uchafu huo)?
 
PICHA ZAKE ZIKO JUKWAA LA PICHA KITAMBO SANA
 
Mambo haya hayajaswihi ndani ya Uislamu...wanajaribu kuuingiza Ufirauni wao kwenye dini ya mwenyezi mungu..Laana tullwah...!!!
 
wenyewe wanasemaga katokelezea!View attachment 112573
Mheshimiwa Lukindo upo okay? Sisi tunaita " DIN wa DUNIA " Yaani wakati mmoja Tunaitumikia Dini ya MwnyeEzzi Mungu na wakati huo pia tunaishughulikia Dunia kama tulivyo tandikiwa " bila kuvunja Amri na Utiifu wake muumba.(katupa timu ya kujifurahisha na timu za kumuabudu kikweli)
Sasa tatizo liko wapi..? Nafikiri kama tutakosea itakuwa baina ya sisi na Dini yetu...Ambayo Mwenyeezzi Mungu ni Msamehaji na mwenye rehema kwa viumbe vyake.AMIN
Tofauti na wenye Kumshirikisha Mwenyeezi Mungu au kumlinganisha !!
Ubarkiwe kuona haki na nuru.AMIN
Most welcom!

 
duh once in atime

Mheshimiwa Frank, Sisi tunaita " DINI na DUNIA " Yaani wakati mmoja Tunaitumikia Dini ya MwnyeEzzi Mungu na wakati huo pia tunaishughulikia Dunia kama tulivyo tandikiwa " bila kuvunja Amri na Utiifu wake muumba.(katupa timu ya kujifurahisha na timu za kumuabudu kikweli)
Sasa tatizo liko wapi..? Nafikiri kama tutakosea itakuwa baina ya sisi na Dini yetu...Ambayo Mwenyeezzi Mungu ni Msamehaji na mwenye rehema kwa viumbe vyake.AMIN
Tofauti na wenye Kumshirikisha Mwenyeezi Mungu au kumlinganisha !!
Ubarkiwe kuona haki na nuru.AMIN
Most welcom!

 
Back
Top Bottom