mfalmeselemani
Member
- Sep 30, 2014
- 95
- 47
Na Ghati Chacha
MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Gachuma amekuwa ni mmoja wanaokipasua Chama kutokana na mienendo yao isiyokuwa ya kuleta umoja.
Hali hiyo inatokana na mtindo wake wa kupanga safu za viongozi na kuweka wabunge ili aweze kuendeleza ufalme wake anaousema kuwa yeye ndio mwenye sauti wa siasa za Mara na Mwanza.
Hii ni tabia ya ovyo na ndio sababu ya mgogoro mkubwa uliopo sasa hasa katika jimbo la Tarime Mjini na kule vijijini kusababishwa kuwepo kwa matatizo yaliyosababishwa na yeye hasa baada ya kutoa fedha za rushwa na kuwataka wachaguliwe wao huku na kushindwa kuona maslahi mazima ya Chama.
Chama kinapaswa kusimama mstari wa mbele na kuona watu wa namna hii wanakiharibu Chama kwa kuletea sintofahamu ambazo zinaleta mpasuko miongoni mwa wanaccm ambao wamekuwa pamoja na watu wenye umoja na mshikamano.
Uimara na uthubutu wa Rais na Mwenyekiti wa CCM Dk. John Magufuli unahitaji kuwa na viongozi imara na wenye nguvu ya kuleta mabadiliko kwenye na sio kuwa na viongozi ngazi ambao wamepata madaraka kwa ajili ya kuficha madhambi ya watu waliowapa madaraka kwa njia ya rushwa.
CCM ina haki na wajibu wa kuonyesha mfano wa kutokomeza rushwa kwa matendo na hasa kuwakemea viongozi aina ya Gachuma ambao wanatumia rasilimali fedha waliokuwa nao kukichafua Chama.
Hii tabia ikiachwa ndio tutarudi tulipotoka ambapo kunajenga matabaka ya watu wenye nguvu ndani ya Chama na sio Chama chenye nguvu kwa wanachama hasa kutokana na madudu yanayofanywa na watu waliopewa vyeo na Chama kusimamia siasa na wao wanakuwa sehemu ya ubadhirifu.
Yanayotokea au yaliyotokea kwa Tarime na maeneo mengine ni aibu sana kwa Chama kikongwe japokuwa nina matumaini makubwa inaelewa na itachukua hatua basi lazima kila mwanaCCM akemee kwa viongozi wa Chama kubeba wagombea kuwa sio kitu kizuri na kinaleta mpasuko.
Kila kiongozi anapaswa kuchaguliwa kwa ubora wa hoja yake na sio kwa ukwasi wake au kubebwa na kiongozi fulani mwenye nguvu katika eneo lake.
Siasa za kupandikiza viongozi zilishakwisha na wakati na sasa ni wakati wa kupata viongozi bora kama ilivyo kwa Rais Magufuli kwa kuwa walichokifanya kina Gachuma na wenzake sio siasa bali mchezo mchafu wenye kukichafua Chama na siasa zao za kimakundi ambazo zinaendelezwa na MNEC Gachuma.