Mnasema mmesoma elimu yenu imetufikisha wapi?

Mnasema mmesoma elimu yenu imetufikisha wapi?

hapa tulipo na tunakoelekea.
ki ukweli hoja yako ni nzuri kama ingesimama bila dini kwa kuwazungumzia wasomi kwa ujumla wametufikisha wapi ingekuwa na mashiko zaidi harafu hili la dini lingejadiliwa ndani kwa ndani.
swala la nchi linatuuma wote na linatukela kwelikweli sijui inakuwaje/
hao wasomi wenyewe wamekuwa vilaza kila siku mawazo yao ni kujikita kujibu maswali rahisi (waibe wakagombee ubunge ) na matokeo yake wanatoka maeneo ya maana ya kuijenga nchi.
daktari mbunge -afya bora tunaipata wapi
mwandisi mbunge tatizo la maji na upangaji miji litaishaje
mwalimu pekee ndiye aliyebaki kwenye taaluma yake unategemea nini.

lakini paliko na ukweli lazima tukubali wakristo wengi tumepoteza maadili ya dini yetu na hapa tusiwe wabishi wengi wetu hatufanyi kwa ajili ya wengine tumekuwa warafi wezi wdhurumaji wenye tamaa ya mali na fedha bila kujali uhalali wake.
inauma lakin huu ndio ukweli wenyewe.
mikataba mingi yanchi kudhurumiwa imesimamiwa na viongozi wakristo kwa kujua walichokuwa wanafanya au kutokujua na kubwa zaidi ni ubinafsi wetu tu.
tubadilike hata waliotuletea shule hawakutegemea tungekuwa katika hali hii.
tubadilike tuikomboe nchi yetu inaliwa na mchwa wenye ukubwa wa simba.

Jakaya wakati anasimamia mkataba wa IPTL alikuwa mkristu?
 
Hivi segerea wanaruhusu kwenda na vifaa vya kielekroniki? Nahisi hii post ni ya Ponda.
 
Mkuu uliyeanzisha mada nakataa ulichoainisha hapa. Labda nikukumbushe tu kuwa ufisadi hauna dini.
Kila binadamu ambaye hana msingi mzuri wa mafundisho halisi lazima atakengeuka na kutenda isivyompasa kutenda. Angalia vizuri kisha urudi tena kama mafisadi wote unaowajua ni wakristo. Ukitaka kwenda njia hiyo utajikuta umekosea kwa kiasi kikubwa sana. Na mi sitaki kwenda huko kwa sababu umesema mwenyewe tujadili hoja.
 
Jakaya wakati anasimamia mkataba wa IPTL alikuwa mkristu?
imefika wakati na mimi nikubali sikueleweka vizuri au sikuelewa!
msingi wangu mkubwa wa kwanza ni kukataa kujadili mada hii kidini na nikasema dini iwe sehemu tu ya majadiliano.
lakini nikachukua nafasi hii kukubali kuwa kunaukweli kuwa maadili hata ya wakristo yamebadilika na wao kuwa wanyang'anyi na kwa kusema hivyo sina maana waislamu ndio wako safi hapana niliona nivizuri tuanze kujadili kwa kujiona wenyewe kwanza tumetumia vipi madaraka yetu.
kwa bahati mtoa mada alisha omba isilete ugomvi na matusi sasa wasiwasi unaoka wapi?
kingine lazima tukubali kuwa tumekuwa watu wazima na tumekomaa tunahitaji kushiriki vizuri kwenye mijadala migumu pia inayogusa interest zetu hata kama kwa kusema hivyo tutaumia.
kwa kufanya hivi tunaweza kuwa tayari hata kuwapeleka wajomba zetu baba zetu polisi kwa kuhusika na madawa ya kulevya.
kama tunataka kutoka hapa tulipo ni ukweli tu ndio utakaotutoa bila kuangalia mzani na kuangalia umeumizwa wapi
 
Moderator pleeeeeeese, fanya kazi yako, upuuzi huu toa hapa. Hakuna kujaza kurasa za new post na vitu duni kama hivi, vinapunguza hadhi ya jukwaa. Mtoa mada soma signature hapo chini.
 
Nafkiri Mods wanatakiwa kuifuta hii mada ili isiendelee kupata wachangiaji! Nasema hivyo kwa sababu inaonyesha mtoa mada anataka kuendeleza mijadala ya udini ambayo kwa kiasi kikubwa inaendelea kuleta mpasuko kwenye jamii ya Watanzania. Pia mada imekosa mashiko kwa sababu zifuatazo

1. Mtoa uzi katumia mawazo yake binafsi katika kutoa mada yenye ujumla kwa nchi za Kiafrika.
2. Si kweli kwamba nchi za kiafrika, ikiwemo Tanzania zina viongozi wengi wa kikristo kuliko waislam. Siamin kama kuna tafiti zilizofanyika kuhusu idadi ya viongozi na dini zao katika nchi zetu.
3. Suala la maendeleo si suala la wakristo au waislam peke yako! Ni suala mtambuka, linahusisha watu wa kila aina, jinsia zote! Hata kama wakristo wako kwenye nafasi ya kutunga sera na kusimamia, halaf waislam wako kwenye utekelezaji, wote wanawajibika kwa ajili ya kuleta maendeleo.
4. Dhana ya kwamba wakristo wamesoma kuliko waislam haina mashiko. Ni maneno ya mitaani tu!

Nimemaliza!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

I salute you.
 
Back
Top Bottom