"Mnapanda Basi la Makabila Karne hii 21?" Mwl. Nyerere. Basi la Makabila Limepaki Ngomeni Kuelekea 2020

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,038
487
Mwasisi wa taifa hili alikemea kwa ukali siasa za kuwagawa watanzania kikabila, kikanda nk. Lakini kwa sasa, kama alivyodokeza Waziri Mkuu Mstafu Jseph Sinde Warioba nchi imesambalatika, siasa za ukabila na ukanda (zilijionesha wakati wa zoezi la bomoa bomoa); miradi ya maendeleo kusogezwa eneo moja; watu wa mikoa minne kwa uwingi wao wanasema ni zamu yao sasa; na hata waandishi wazuri wanajifuja kutetea ukanda na ukabila (hawakuwa hivyo awali); na watu wa itikadi fulani wanafanya chochote cha kukera na kudhuru watu wanaofuata itikadi tofauti na ya watawala.

Taifa la amani limeshuhudiwa watu wanatekwa na kupotezwa, wanashambuliwa kweupe hakuna hatua za kiuchunguzi na kisheria zinazochukuliwa. Raia wanabambikiwa kesi kubwa kubwa ili kuwakomesha ama kuwanyamazisha.

Aidha, Kuokotwa maiti mitoni, ufukweni, majiani yote haya si dalili wala ishara njema kwa mustakabali wa taifa letu.

Upendeleo wa wazi unafanyika ili raia fulani walio wengi wajione wamoja na 2020 wawezekuimarisha matokeo ya chaguo la kanda ya ziwa, tuko wengi tukiamua kukandamiza tunaweza mwanawane.

Kwa jumla, hizi ni siasa na sera mfu. Watanzania tujifunze kwa wanyarwanda ilivyokuwa kabla ya 1994. Ukabila, upendeleo, ukanda vilikuwa petroli tosha kuanzisha moto. Tusiombee mtu mmoja au kikundi fulani kichoke kiamue kuchomoa betri, moto utalipuka.
 
Hii ni awamu ya Wakolomije. Kaskasini msibiri kwanza....JPM Iringa




 
Hakuna kitu kama Kabila la Kanda ya Ziwa Dunia hii, isitoshe Nyerere hakuzuia huo unaouita ukabila kwani hata huyo uliyemtaja anatokea sehemu moja na Nyerere na ndicho kilichomfikisha hapo, Nyerere alimpendelea kwa kuwa wanatokea eneo moja.
 
Back
Top Bottom