Mnaotarajia kuandamana someni hii...

Mnaotarajia kuandamana someni hii...

Epuka fujo, kimbia vurugu, acha choko choko, kubali kuwa mjinga mwenye faida, kuliko kuwa mjanja mwenye hasara. Kwa mwoga huenda kicheko, lkn kwa shujaa huja kilio.

Baadhi ya watu wamo gerezani, pasipo kutarajia, kwa sababu tu, walisukumana na mtu mgonjwa, akafa kwa kuanguka.

Idadi kubwa ya watu ambao hawajasoma, si kwamba walikua hawana akili shuleni, lkn chanzo ni wazazi wao, walifanyiana vurugu, wakatengana, na watoto wakaambulia hasara.

Angola ni nchi tajiri sana, lkn haina wataalamu wengi, kwa ajili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, iliyo dumu kwa miaka 35, pia vilema ni wengi, kwa ajili ya land mines, mabomu ya ardhini, yaliyo achwa wakati wa vita hivyo, na serikali inatumia fedha nyingi sana kuyaondosha, maana wakulima wanashindwa kuzalisha, ingawa ardhi ina rutuba.

Hayo ni baadhi tu ya athari za vurugu, choko choko na fujo. Tanzania ni nchi nzuri mno, watu wake ni waungwana pia serikali haina dini, raia wana uhuru wa kuabudu, katika dini yoyote, mradi tu ufuate sheria na kanuni zilizopo, oa na olewa na yeyote umpendaye, kwa dini yoyote, siku na saa yoyote, la endapo huko kwenye dini hawakutaki, lkn ukienda kwa mkuu wa wilaya atakufungishia ndoa yako.

Tanzania mnataka nini? waTanzania nyie, Mungu awape nn? Kila mtu, kila kiumbe kina mapungufu yake, ndiyo maana, tunakula samaki lkn miiba yake, tunaitoa, samaki ana shombo, tunamtia ndimu, lkn je si tunamla? Basi na maisha, na watu, wapo ivyo ivyo, tuangalie mazuri yao, na mapungufu yao, ni kawaida hiyo, Mungu mwenyewe, ameumba viumbe vyote vipo hivyo hivyo.

Je, hili nalo linahitaji mahubiri ya padre, shehe na mchungaji? Hebu fikicha ubongo, Mtanzania, ili ujifikirie, kama wakimbizi wa DRC, Burundi, wanakimbilia Tanzania, je ww mTanzania ukifanya fujo utakimbilia wapi?

Nawakilisha nikiwa mpakani kabisa na msumbuji huku,[HASHTAG]#Mtajijua[/HASHTAG] wenyewe..
Wamekutuma!
 
Hakuna atakaye andamana hususani Humu Jamiiforum, Wataweka nukuu nyingi ila Nina hakika hakuna, nasematena hakuna mwenye kuandamana. Izi ni mbwembwe kama zilivyo za UKUTA.
Ona ulivo huna akili,UKUTA mlichezewa akili na MBOWE,na mkajaa kwenye kuminanane zake.
 
1.Rais ni mwongo maana aliongea tarehe 14/10/2017 kuwa kuna Watumishi wa Umma 59,000+ watapandishwa madaraja mwezi Novemba lakini hadi sasa hajapanda hata mmoja.

2.Rais alisema baada ya uhakiki kumalizika kutakuwa na maslahi bora kwa Watumishi wa Umma lakini hadi sasa wamepewa za uso.

Waandishi wa habari hizi hazifai kupamba kwenye front page maana sijawahi kuziona.

Kutoka hifadhi ya misitu ya Madihani
Mwanachama wa CCM.

Mwana CCM mwenzangu kidumu cha Mapinduzi!! Tutafakiri kwa makini fikra za viongozi wetu wa chama.

Kuna suprise nyingine inakuja kwa wafanyakazi wa umma. Baadhi watanufaika na wengine wataumia...mishahara kupunguzwa ama kuongezwa. Hili ni jamabo jema ktk utumishi wa umma maana kuna taasisi za umma mtu ana majukumu machache ila anapokea mshahara mara nne ya anayepigika kwenye Halmashauri zetu.
 
Nilisoma sehemu kuwa kuna jamaa wanataka kwenda kwenye sayari ya Mars. Kilichonifurahisha ni kuwa katika kukamilisha mpango wao hawatarajiii kurejea duniani bali ni safari isiyo na marejeo, cha msingi zitakuwepo rekodi jinsi walivyoenda na walivyokufa. Naamini historia itawatambuka zaidi ya sisi tutakaobaki hapa na baadae kufa kwa njaa, mafuriko au hata kuuawa na wasiojulikana.
Wanaotutia woga huu ni wenye chaneli za kula na kushiba daima wanakuwa wakali kwa wenye njaa ambao nao wanakihitaji chakula hicho hicho wanachokula wao. tatizo linakuwa kubwa pale wenye shibe wakiwa ni chini ya asilimia 2% huku wenye njaa wakifikia zaidi ya asilimia 80%.
 
Hili litapita na Tanzania itaendelea kuwepo
Hakuna atakaye weza kuisambaratisha nchi hii
 
1.Rais ni mwongo maana aliongea tarehe 14/10/2017 kuwa kuna Watumishi wa Umma 59,000+ watapandishwa madaraja mwezi Novemba lakini hadi sasa hajapanda hata mmoja.

2.Rais alisema baada ya uhakiki kumalizika kutakuwa na maslahi bora kwa Watumishi wa Umma lakini hadi sasa wamepewa za uso.

Waandishi wa habari hizi hazifai kupamba kwenye front page maana sijawahi kuziona.

Kutoka hifadhi ya misitu ya Madihani
Mwanachama wa CCM.
Hili litapita na Tanzania itaendelea kuwepo
Hakuna atakaye weza kuisambaratisha nchi hii
 
Wewe watu wote wangekua na akili kama yako wala uhuru tusingepata. Bora ungejenga hoja ya msingi ya kwa nini unadhani haya maandamo hayana tija kitaifa wala kiuchumi, ungeeleza matarajio mema ya mbeleni yatokanayo na utendaji wa serikali kuliko kujenga hoja yako katika woga. Ingekua hivyo hata rais angeogopa kuchukua hatua azichukuazo kuhusu ufisadi. Uwoga na ubinafsi haujengi nchi
I agree! Hata maendeleo hayaji kwa kuwa kama makondoo!

Hata US wamwfikia hapo walipo kwasababu ya kukataa ukondoo! Wakachapana na mwisho wakatia akili na nchi ikafikia hapo ilipo!
 
Sio kwa kichaa anaetuongoza
Mwana CCM mwenzangu kidumu cha Mapinduzi!! Tutafakiri kwa makini fikra za viongozi wetu wa chama.

Kuna suprise nyingine inakuja kwa wafanyakazi wa umma. Baadhi watanufaika na wengine wataumia...mishahara kupunguzwa ama kuongezwa. Hili ni jamabo jema ktk utumishi wa umma maana kuna taasisi za umma mtu ana majukumu machache ila anapokea mshahara mara nne ya anayepigika kwenye Halmashauri zetu.
 
Hivi kuzuia katiba kutenda kazi yake si kosa pia? Na kuzua habari za taharuki na kuiogofya jamii katika kutekeleza haki zao za msingi zilizoainishwa na kutajwa kwenye katiba si kosa pia?
Kama ni makosa ni kwanini watu wa aina ya mleta hoja na wale wakuu wa polisi wasishtakiwe kwa kuzuia katiba kutekelezwa?
Ni kwanini wanaachwa kuwatisha wananchi kwa kutanguliza vurugu kabla ya amani?
Vyombo vya dola vyenye mamlaka ya kuzuia na kuilinda katiba ni kwanini isiwakamate hawa wanaotishia uwepo wa vurugu ili waseme yalipoo makundi yanayojipanga kufanya vurugu siku hiyo na ni nani anayeratibu vurugu hizo pamoja na zana wtakazozitumia kutekeleza vurugu hizo hasa wakizingatia maandamano ya amani ni njia na haki ya kiraia inayotajwa na kusomwa kwenye katiba ya jmt?
Ujinga wa wananchi ulikuwa wakati wa kuchagua na sio kutenda! Acheni kuwatisha wanapotumia haki yao ya kikatiba badala yake wapewe ushirikiano mkubwa!
 
Kuna watu ni wajinga kweli.

Hivi watu wanaoandamana kudai haki za kirai wakiwa hawana silaha wala vurugu, mabomu yatatoka wapi? Acheni kutisha watu.

Jambo muhimu ni kuwaacha watu waandamane kwa amani, na ikiwezekana Rais apokee maandamano, achukue malalamiko yao, na kisha atoe majibu.
 
Woga wetu ndio umaskini wetu, Mandela amgekuws anafikra km wewe umgekuwa huru leo? Wacha tufe kwa ajili ya watoto zetu, ili waishi sehemu yenye demokrasia
 
Hivi Mbona haya maandamano yanawanyima usingiz[emoji23]
ddac3bbf9651cd5c29552bda855da4dc.jpg
 
UMETUMWA. LAKINI KAMWAMBIE ALOKUTUMA KACHELEWA. SI TUNAANDAMANA
 
Waache waandamane ,hio ni haki yao...lkni msidhuru wala kusimamisha shughuli za watu..nadhani kuna sensa itafanyika hyo tarehe 26,,wakijiona wako wachache hawataendelea...mnavyowazuia ndivo mnavowapa nguvu ya kujihisi wapo wengi..


Waacheni ..naisihi Serikail iwaache.
 
Nyie jiongelesheeeeennnnn, lakini mwisho nataka muandamane nione utamu wake.
 
Ni aibu sana wananchi kwa wingi wanapokuchoka mpaka kujipanga kukugomea. Kiongoz makini atajitafakari lakini mwingine atajiandaa kivita kupigana na raia wake walompa iyo kazi! Hapo ndipo utapogundua Afrika inapitia wakati mgumu na inaviongozi wa ajabu.
Kiongozi wa ajabu dalili zake ni:
1. Kubagua watu wake,wengine kuwaona bora zaidi na kuwapendelea hku wengine akiwabana. Mf. bomoabomoa.
2. Kuwa kigeugeu wa kauli zake mwenyewe,anaahidi lkn hatimizi na anafanya yasiyoafikiwa hasa na vyombo wakilishi vya wananchi (bunge) mil 50 kila kijj na ujenzi kulekwake
3. Kunyima watu haki za msingi na kutopokea ushauri wala hoja zilizo tofauti na zake. Pengine kutukana watangulizi/wazoefu pale watoapo mawazo mf.kuwashwawashwa!
4. Kudhulumu haki za raia wake mf. walimu kunyang'anywa barua stahili za kupanda madaraja na kutakiwa kusubiri kiongozi atapojisikia,zoezi la katiba mpya kutokamilishwa
5. Kutoonekana karibu na raia wake pindi matatizo yatokeapo.mf. tetemeko.
6. Kutumia vitisho,ubabe,unyanyasaji wa haki za wengine mf. uchaguzi zenji
6. Kushindwa kutetea na kulinda uhai wa raia wake hususan wanaompinga/wenye hoja tofauti. Mf. Lissu,nape,kileo nk.
7. Kuua demokrasia na kuchanganya siasa za vyama na shughuli za kiserikali ikiwamo kuhamasisha hamahama yavyama. Mf. shughuli ya kijesh arusha,mkutano wa chama ikulu nk.
8. Kupendelea kibinafsi kusikozingatia sheria,kanuni za kazi,maadili ya kazi na utamaduni. Mf makosa ya mnyeti na bashte.
9. Kushindwa kuboresha sekta muhimu na zinazogusa wananchi wengi mf. Kilimo,elimu,afya nk. badala yake kulazimisha viwanda vitokee.
10. Kujenga mahusiano tata na nchi jirani,wahisani na nchi washirika kibiashara. Mf. Kuchoma vifaranga toka Ke,ndege kuzuiliwa canada,Usa kukata misaada nk.
Mambo yakujitafakari ni mengi kuliko kujiandaa kisilaha ili kutisha watu na kujidanganya kuwa ETI tuna amani.
 
Back
Top Bottom