Hii ni katiba isiyoandikwa…
Unwritten constitution. Hatumtambui, yeye na genge lake la kina kikwete. Kama unamtetea kapande naye ndege nendeni zenu Oman. Tunaelekea ikulu sasa na hatupoi…
Tanzania tuna katiba iliyoandikwa.
Usiseme katiba, sema kitu kingine, sema habari ya Samia kukosa uhalali kwa sababu ya haki, kwa sababu ya kuvunja social contract, kwa sababu haungwi mkono na watu wengi, kwa sababu kashindwa kuongoza.
Huna uhaba wa vitu vya kumkosoa Samia. Kwa nini unamtungia habati ya katiba ambayo haipo na haina ukweli?
Ukisema katiba, Tanzania ina katiba iliyoandikwa.
Na uhalali wa kikatiba si uhalali wa kisiasa na kijamii. Kwa hivyo huhitaji kuongelea sana uhalali wa kikatiba kama rais hakubaliki na watu, anashindwa kuzuia au anapanga mauaji.
Samia mwenyewe kasema katiba ni kijitabu tu.
Wapinzani wake wanataka mabadiliko ya kikatiba kwa sababu hawaitaki katiba iliyopo.
Sasa unaingiaje katika mtego wa kulazimisha uhalali wa kikatiba kama tuna katiba inayokubalika sana?
Kwa nini unajiona unahitaji kudanganya habari za katiba wakati Samia mwenyewe kashasema katiba ni kijitabu tu na wapinzani wake wanataka mabadiliko ya katiba?
Unaelewa kuwa hata makaburu wa Afrika Kusini walitawala kwa katiba, lakini katiba yao ilikuwa haina uhalali kwa sababu ilisimamia ubaguzi wa rangi?
Kwa nini unaingia katika mtego wa ku litigate katiba wakati katiba yenyewe haina uhalali kwa sababu haijawekwa na watu imewekwa na Nyerere na chawa wake tu?