Mnaosali kanisa la Mikocheni B (Mlima wa moto) naombeni mnifahamishe hili

Step by step

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
1,164
1,289
Habarini wana bodi wenzangu.

Lengo langu ni jema kabisa hivyo naomba wanaojua wanijuze bila kashfa wala ushabiki.

Miaka kadhaa nyuma kupitia ch 10 kanisa la mlima wa moto lilituonyesha moja kati ya kazi zake njema linazofanya.

Kupitia tv tuliona wachungaji wakienda kijiji fulani na kuwakamata misukule waliofichwa porini huko kwa uchawi kisha kuwaleta kanisani.

Habari hii iliujenga mwili wa Kristo na kuinua kanisa.

Baada ya hapo ilipita changizo ili likajengwe kanisa kule kijijini na yote haya yalirushwa live kwenye tv hiyo.

Naombeni sasa mnifahamishe maendeleo ya wale misukule je nikija kesho j2 kanisani ntawakuta?

Na je kanisa lililoanzishwa mpaka sasa lina waumini wangp na linaongozwa na mchungaji nani?

Naombeni wanaosali pale mnipatie maelezo maana najua mpo..
 
Hicho kipindi nimekiona sana tu na pia kuna mshenga wa lowasa nae nimeona sina la kusema zaidi
 
Katika ulimwengu huu wa leo imani ni pesa tu hakuna ukweli kabisa niliona ktk kanisa la kakobe eti viwete wanaokuja kwa mara ya kwanza kanisani wanatembea hapo hapo wakati huo kuna viwete wapo kila siku hapo kanisanu hawatembei

Ukiuliza utaambiwa imani yao bado haijakuwa. ...
 
jamani mi natamani tu kujua wanaosali pale hawa misukule nakumbuka waliogeshwa na wakavalishwa nguo kabisa sa mnaosali huko tujuzeni bado wapo na kama hawapo wako wapi bado sijapata jibu
 
Mtaani kwangu hapo,siku hizi hata waumini wamepungua,ilikuwa kero kuulizwa lilipo kanisa,kweli biashara matangazo..
 
Katika ulimwengu huu wa leo imani ni pesa tu hakuna ukweli kabisa niliona ktk kanisa la kakobe eti viwete wanaokuja kwa mara ya kwanza kanisani wanatembea hapo hapo wakati huo kuna viwete wapo kila siku hapo kanisanu hawatembei
Iko hivi Mimi nasali pale anayeponya ni Yesu Kristo yeye anomba tu ila anakibali sana kwa Mungu kutokana anavyojitoa kuutafuta Uso Wa Mungu suala la mtu kupona aliye kanisani hapa unatakiwa ujue lengo la mtu kupokea uponyaji nini kiimani jibu ni ili tu azidi kumuamini kristo mf mgeni Anapopona ni rahisi kuwavuta wengi waliojua hali yake hapo mwanzo na yy imani yake kupanda zaidi ili akae na wokovu sababu hata akipona bado kufa kupo hivyo lengo ni roho yake mtu isipotee hata kama akipona
 
Habarini wana bodi wenzangu.

Lengo langu ni jema kabisa hivyo naomba wanaojua wanijuze bila kashfa wala ushabiki.

Miaka kadhaa nyuma kupitia ch 10 kanisa la mlima wa moto lilituonyesha moja kati ya kazi zake njema linazofanya.

Kupitia tv tuliona wachungaji wakienda kijiji fulani na kuwakamata misukule waliofichwa porini huko kwa uchawi kisha kuwaleta kanisani.

Habari hii iliujenga mwili wa Kristo na kuinua kanisa.

Baada ya hapo ilipita changizo ili likajengwe kanisa kule kijijini na yote haya yalirushwa live kwenye tv hiyo.

Naombeni sasa mnifahamishe maendeleo ya wale misukule je nikija kesho j2 kanisani ntawakuta?

Na je kanisa lililoanzishwa mpaka sasa lina waumini wangp na linaongozwa na mchungaji nani?

Naombeni wanaosali pale mnipatie maelezo maana najua mpo..
Ile ilikua sinema tuu hakuna cha msukule,mchungaji ana kesi za wizi wa umeme,walimu bila vibali wa kenya,kujenga bila vibali,kutolipa kodi za majengo etc
 
Mlima wa motoooooooo! Ndipo zinapotoka dhahabu zinazovaliwa na askofu mtukuka Lwakatare, ndipo ahadi za kuchukua na kusomesha watoto toka kilosa zinapoyeyuka kila baada ya uchaguzi, ndipo watu wanageuzwa misukule ili watu wazidi kuchanga pesa na kumwezesha gagura kijenga mahekalu wakati anaowahubiri wanauzakila kitu kumtajirisha. Kama kuna moto utaanzia kwenye mrima wa kichwa chake au ST. Marys zote. Msinihukumu ila ulizia kila mtu anayefahamu maisha yake wakujibu who is she?
 
Back
Top Bottom