Kuna watu wanapinga lockdown bila kuwaza kwa mapana na marefu wengine hili jambo wanalichukulia la kisiasa badala ya kutazama athari kwa nchi na maisha ya wanyonge.
Hapa vijana wengi wanakuja na hoja mfu kwamba tutakufa kwa njaa wakati wanajisahau wanazunguka kila kona kusaka hizo hela ambazo zinapelekea kulieneza hili gonjwa anbapo sasa yawezekana mtaa, kijiji,wilaya au mkoa utokao waweza kukumbwa na maambukizi mengi kupitia wewe kisha shughuli nyingi zitakwama wote mkawa wagonjwa mkajipiga lockdown ya ugonjwa bila kujijua na kupelekea vifo jambo ambalo ni hasara kwa nchi maana pesa wanazo kusanya kipindi hiki zikatumika ktk kuwakimbiza nyie wabishi mahospital.
Nafikir tuvumilie kidogo kuliko kuendelea kuusambaza huu ugonjwa serikali iamue sasa ktk hili hambo ##LOCKDOWN haikwepeki
Kungekuwa na mantiki ya kuacha wazi bila lockdown kama kungekuwa na upungufu wa maambukizi sasa yanazidi kupanda hapa tunafanya nini?
Hata hizo pesa zinazokusanywa sasa hivi zitaishia kwenye mafuta na kuhudumia wagonjwa ambapo mambo mengine bado yatasimama tu.
Vijana tuokoe watoto wazee ndugu na jamaa na sisi wenyewe tuache ubishi.